Nionavyo vita vya majambazi na Muungwana

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Katika kufuatilia mihangaiko ya Mh.Kikwete nimeona zile safari safari zake zilikuwa na lengo la kuwapa mwanya Mawaziri na alikuwa akipima uwezo wao wa kufanya kazi bila ya kuwepo yeye ,alichogundua ni kuwa hakuna linalofanywa zaidi ya ufisadi na wakitumia mwanya huo kujilimbikizia mimali bila ya kuogopa kumwaibisha Raisi.Hakuna alieweza kufanya jambo mpaka arudi ,hakuna harakati mpaka awepo yeye ,kwa kweli alikuwa amebeba mzigo na hakuwa na jinsi ya kuutua.
Ndipo niliposhituka nilipomsikia akitangaza kuwa kuna vita na majambazi,aliutangazia uma akiwepo Kagera kuwa hakuna msalie mtume ,vita ni vita huwenda wakaingia watakaokuwemo na wasio kuwemo ndugu jamaa na marafiki ,kila mtu aliona kuwa sasa majambazi yatakiona na nchi itakuwa salama ,kumbe dongo lile Mh.alilirusha mbali na sasa limeanza kuwa gonga majambazi na tayari limeshawagusa wengi wakiwemo wanafamilia ,ila alitowa wito kuwa asilaumiwe mtu.
Nionavyo bado dongo ni zito na ndio awamu ya kuanzia imekwisha anza ,kuna ya Mkapa ambayo alikuwa Jambazi sugu na bado anaendelea kupeta ,huyu nae anasukiwa ususi maalum ila anachungwa chungwa asije akakurupuka , mijisamaki hii mikubwa ikishakamatwa hapo kutafuatia wafanya biashara za unga na wateja wao ikiwemo Zanzibar ambako ndio kituo kikuu cha kusafirisha na kwenye wahusika wasiokamatika.
Je wewe unaona vipi ?
 
Back
Top Bottom