Nionavyo Tena kwenye operation ya Urusi dhidi ya ukraine

Baadhi ya watu wanadhani Urusi imekurupuka.

Ukweli Urusi kila hatua kwa op hii ilipangwa.
Urusi inaijua Marekani nje ndani kama ambavyo Marekani inaweza kuwa inaijua Urusi,kwa sababu ya historia ya nchi mbili hizi.

Wengi hawajasoma juu ya "cold war".

Kabla ya kuivamia Ukraine Urusi ilikua inajua Ukraine inafanya Nini,imeficha silaha wapi na askari wake wanafundishwa na nani(USA na baadhi ya NATO).

Kabla ya vita Urusi ilikua inajua nikiingia kuipiga Ukraine USA ama NATO wataingia kuisaidia Ukraine ama watampatia silaha.

Kabla ya op Urusi ilikua inajua USA au NATO watafanya Kila liwezekanalo kurefusha vita ili kumchosha Urusi na hatimae kumdhoofisha kijeshi na kiuchumi.

Kabla ya op Urusi alijua atawekewa vikwazo mbalimbali ili adhoofike kiuchumi.

Kwa Nini nayasema haya,

Nayasema haya kwa sababu Urusi iliwahi kuipiga Afghanistan,
Kilichotokea ni kama hiki
USSR ilijikuta inapigana na mataifa yote makubwa Duniani.
Kama kawaida hawakuingiza majishi lakini waliwasaidia Afghanistan kwa silaha na Intelijensia ya vita.
Nchi zilizoisaidia Afghanistan ni USA ,UK,German,China,saud Arabia, Pakistan, na NATO wengine pamoja na vikundi vya akina Osama bin laden.
Urusi ilikua inapigana na Mujahedeen waliokua jeshi la Serikali ya Afghanistan iliyoondolewa na Urusi.
Hawa walisaidiwa kwa silaha na fedha kuikabili Urusi.

Hivyo Urusi inajua tabia za USA na west pale inapoingia vitani na nchi nyingine.

CHECHEN na Putin
Wachechinia ni wakazi Urusi wanatokea katika Jimbo la Chechen.
Hawa jamaa Wana Mila na desturi za tofauti na Warusi wengine,ila sehumu kubwa kama sio 100% ni waislam.
Hawa wakati wa utawala wa Boris Yeltsin walikua na mawazo ya kujitenga,nadhani mawazo hayo yalipandikizwa na Adui namba moja wa Urusi,USA.Ushahidi upo.
Walipewa misaada ya fedha kwa Siri kutoka USA ili wajitenge.

Kweli bana.
Wakianzisha vita kutaka kujitenga na Urusi,Rais akiwa Boris Yeltsin.

Kama mnavyojua Boris alikua sio kiongozi makini sana,alikua mlevi mbwa na mpuuzi ingawa alikua ana akili sana.
Jeshi la Urusi lilipuuzwa sana,halikupewa kipaumbele,kulikua Kuna ufisadi,askari ahawana morale,mahitaji ya wanajeshi hayakutiliwa maanani,na hawakuheshimika kabisa ,hivyo wanajeshi hawakua na moyo kabisa kwa Kila jambo.
Basi bana vita kati ya waasi wa Chechen na wanajeshi wa Serikali ilipigwa vikali sana,matokeo yake askari wengi wa Serikali ya Urusi walikufa sana na maiti kuzagaa mitaani.

Vladimir Putin.

Boris Yeltsin aliteua na kutumbua mawaziri wakuu wa Urusi kama wanne hivi na wengine walihudumu kama kwa mwezi hivi.
Na hatimae akamteua VVP.

Vladimir Vladimilovic Putin alipoingia kwenye nafasi ya Uwaziri Mkuu akakuta jeshi la Urusi linasumbuliwa na waasi wa Chechnya.
Putin akapanga safu yake akaongea na wanajeshi wakaelewana.

Jeshi la Urusi likaenda mara nyingine kukabiliana na waasi wa Chechnya.
Aisee kipigo walichokipata hao wachechen Mungu ndio anajua.
Walipewa kipigo Cha paka mwizi na wakashindwa vibaya sana na majeshi ya Urusi.
Wakadhibitiwa vibaya sana na wakashindwa vita hiyo,na makamnda wao wengi wakakamatwa na kufungwa magerezani.

Sasa kilichotokea, ni wakaachana kabisa na vita dhidi ya Ujeshi imara la Urusi,wakaanzisha mapambano kwa njia za Ugaidi.
Wakaanza kulipua majengo,kuteka kumbi za starehe mfano ule ukumbi wa maigizo moscow,kuteka shule za vitoto vidogo kule Beslan,na kulipua njia za usafiri.

Kutoka kuwa makamanda wa jeshi Hadi kuwa Viongozi wa Ugaidi wa Chechen.

Baadae Putin akaja kuwa Rais

Hapa Putin akaanza msako mkali kwa Hawa Viongozi wa Ugaidi ndipo kiongozi wa Chechen wakati huo Aslan Mashkadov kiongozi Mkuu, na Bashir Yanayev kamanda Mkuu wa chechen walipokua wakisakwa vikali na putin na hatimae GRU na FSB Spetsnaz walipofanikiwa kuwaua kwa nyakati tofauti na kwa mahali tofauti.
Walikuwa wakiwasaka wapiganaji magaidi wote walikua chini ya hawa na kuwauwa na wengine kufungwa.Hatimae wakasalim amri baadae Putina akakaa na waliobaki akawapa mpango wake wa kuwa na uhuru kamili lakini chini ya Serikali kuu ya RF nao wakaupenda mpango huo na wakakubaliana, na Sasa Leo unawaona wanampenda na kumtii putin.
Urusi hakuna Ugaidi Tena na nchi Iko salama sababu ya Putin.
Hii OP ilimpa Putin umaarufu mkubwa na kupendwa sana Urusi.

Operation ya Sasa ya ukrine.

Urusi kama ilivyo USA Ina majasusi Dunia nzima.
Wanajua Kila kitu USA au NATO wanafanya juu ya Urusi.

Ukiacha majasusi watu Urusi Ina vyombo vya kuweza kuona chochote Cha kijeshi USA anachofanya Dunia nzima.

Urusi anajua uwezo na udhaifu wa USA.

Urusi peke yake imeweza kuwafukuza USA,UK na FR nchini Syria, na kuvunja mpango wao wa kutaka kumtoa Assad madarakani,
Urusi imeweza kuzuia mpango wa USA kutaka kumtoa Maduro madarakani.

USA inapoenda kuzivamia nchi dhaifu kama Iraq ama Afhanistan ama hata Libya huenda na kundi la nchi nyingine kuisaidia USA ,wakati hiyo n hi inayokwenda kupigwa (Iraq na Afhanistan)Huwa imewekewa vikwazo ama imepelelezwa kwa mgongo wa UN mfano Iraq.
Mifano IPO.

Kinyume chake Urusi ikipigana na nchi,nchi hiyo hupewa misaada ya silaha na Kila kitu itakachohitaji na safari hii tumeona pia Urusi imewekewa vikwazo vizito mno..

Pia ikumbukwe Ukraine ni nchi yenye Nguvu kijeshi mara Tano kuliko ilivyokua Iraq kabla ya kupigwa na USA .
Ukraine Ina viwanda vya silaha,mitambo,magari na Kila aina ya bidhaa.
Ukraine Ina jeshi zuri kabisa na zaidi kabla ya hii Op ilikua inafundishwa na USA ,UK,fr na wengieo,pia ikipewa Silaha.
Na hata Sasa hivi inafundishwa na hai na inapewa silaha.,lakini Cha ajabu Urusi inaipiga taratibu bila kujali misaada hiyo.
Je?
Urusi ni dhaifu?
Urusi ni maskini?
Urusi ilikua inakuzwa?
Urusi imekurupuka?
Kwangu mimi Urusi nchi yenye jeshi kubwa kabisa hapa duniani.
Kama alivyosema Biden "hatuwezi kupeleka jeshi letu kupigana na Urusi moja kwa moja,safari hii tuna Dili na moja ya jeshi kubwa kabisa hapa duniani,hatudili na magaidi"

Kama Rais wa USA kasema hivyo,Mimi ni nani Hadi nipinge?

Sore tunajua NATO walichokifanya kwa Yugoslavia,Yugoslavia waliwapiga wakosovo,Bosnia and Herzegovina,NATO walikwenda upande huo na kuwasaidia Kosovo ambae sio mwanachama wa NATO kwa kumpiga mabomu Yugoslavia na hatimae Yugoslavia kusambaratika Hadi kutokea mataifa ya Croatia,Serbia na Kosovo.
Sasa NATO wanashindwa Nini kisaidia Ukraine kwa kuweka hata no fly zone TU?
NATO waliwasaidia waasi wa Syria wakawaita waasi moderate,waasi walichukua miji yote kasoro ilibakibi miji miwili TU,mji Mkuu na Alepo tu.
Alipoingia Putin akarudisha miji yote na waasi kufutwa kabisa..

Vikwazo.
Kwa kawaida vikwazo huwa vinawekwa na UN ama nchi moja binafsi inaweza kuacha kushirikiana na nchi nyingine,lakini USA na EU
Wanazilazimisha nchi ambazo hazina ugomvi na Urusi ziiwekee vikwazo hii sio sawa.
Mbona wao wakati wa ubaguzi wa South Afrika,UN waafrika walipotaka.SA iwekewe vikwazo mbona wao waliendelea kufanya biashara na SA na hatukuwalazimisha?

USA ana kile anachokiita Allies wake lakini anataka kulazimisha Allies wa Urusi wamtenge mfano BRICS.
kulaani ama kuweka vikwazo ni hisia,kama Sina hisia za kulaani usinilazimishe kulaani,kama Nina maslahi usinilazimishe niweke vikwazo.

Matokeo ya vikwazo yamekua kinyume kabisa,wanasema vitaanza kufanya kazi miezi au miaka kadhaa baadae,je Urusi wakipata.ufumbuzi wa vikwazo hivyo nani atakua ameumia?
Putin Hana shida mkuu hata akifa Leo tayari hatajutia miaka 70 kwisha habari yake . Na sidhani kama anajua anapigana vita . Hichi kibabu
 
Huwa sipendi kujibu koment zako ila acha nikujibu
US alienda kuivamia AFGHANISTAN kwakigezo chakwamba analinda usalama wataifa lake
Kati ya US na RUSSIA nani alikua anahaki hakumvamia alomvamia kwakigezo chausalama je US alokua maelf ya KM kutokea AFGHAN ama RUSSIA alokua KM zero tokea UKRAINE

Sent using Jamii Forums mobile app
HAya tuelewane:
huna jibu hata kidogo kuhusu maswali yangu:

Hujajibu swali lake kuhusu Wanazi huko Urusi. Ukraine inahatarisha usalama wa urusi kivipi??
Nchi ndogo kuvamia nchi kubwa zaidi ikiwa na makisio ya kijeshi ya asilimia 10 ya Urusi ???
Nani anaweza kuamini hayo?
Kwa hiyo unakimbia mada tofauti.
Sitaingia sasa kulinganisha kwamba Marekani ilishambuliwa kutoka kambi la Osama ndani ya Afghanistan na hakuna aliyeshambulia Urusi . . . .
Lakini ninapokea bendera yako nyeupe!
 
Back
Top Bottom