Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
huyu ni msanii, wengi ya watanzania wakuzaliwa wenye umri wake ni watoto wa wakulima, hivi utamuelewa mtu anayetoa vibali vya manunuzi ya magari ya serikali, anapiga marufuku ununuzi wa mashangangi kupunguza gharama zisizo za uhumimu, anajipitishia shangingi lake anapokabidhiwa analikataa, kutuhadaa sisi wananchi. Jiulize alikuwa amekusudia nini?, gari likishanunuliwa ukitaka kuliuza linauzwa kama second hand kwa bei ya chini, hapa ni kama mbinu, ni kutaka azuwe kwa bei ya chee kama ilivyombinu ya wakubwa wengi wenye element za kifisadi. Sasa ukulima hapo upo wapi? Au atueleze alilirudisha kwa wauzaji?inasemekana mtoto wa mkulima anayejiita hivyo anamiliki hisa kunako kampuni ya sumry kwa kiasi kikubwa sana kupitia kampuni moja hiv iliyoko arusha
Mimi kwa mawazo yangu Mh.Pinda ni kiongozi ambaye ni mkweli na mwenye msimamo, tusianze kumlahumu wakati hatujuhi ni kitu gani kinajili behind the SCENE. Msikilizeni kwa makini anapozungumzia maswala ambayo yamekaa ndiyo sivyo Serikalini, mara nyingi anachukua RISK ya kukubaliana na maoni ya wabunge na kuachilia mbali mambo ya collective readership-huu ni ujasiri mkubwa sana lakini hilo watu awalioni! Chukulia mfano wa kauri yake kuhusu sakata la Mh. Jairo nadhani hicho ndio kingekuwa kipimo cha kumtathimini Mh. Pinda kwamba ana uzalendo wa kweli kweli - we sema mambo mengi yako nje ya mamlaka yake, sasa afanye NINI?
Tusianze kumlahumu kwenye vitu ambavyo ni obvious, he can't move mountain SOLO - yeye ni binadamu kama sisi, sasa anapojikutaw yuko katikati ya ROCK and hard PLACE unategemea atafanya mihujiza GANI.
hivi lile v8 alilolikataaga ili kubana matumizi akasema la zamani bado jipya lilirudishwaga toyota eeh? Au bado linakula wese letu kama kawa hebu tupeni ripoti tujue huyu mkulima alitupiga fiksi au vp?pinda hana lolote la kijivunia, kiutendaji kwa kuchambua, kufuatilia na kusimamia, heri mara mia mpiga deal lowassa. Lowassa alikuwa anawakimbiza mchwa wa kwenye halmashauri za miji. Wakurugenzi na wakuu wa wilaya na vigogo uchwara wa wilayani, walikuwa wanapata shida wakikumbana uso kwa uso na fisadi huyo.
Pinda yeye ni mtu wa kulalamika, mtoa ahadi na mipango isiyo na tija kwa wakati, pia ni mtu wa kulia lia kama mtoto! Hafai kuwa pm kwa nchi yenye changamoto nyingi kama hii.
Niliwahi kusoma makala moja ktk gazeti la raia mwema iliyoandikwa na mjengwa, akisimulia kisa cha mfalme mmoja mwaminifu kwa nchi yake, ni kisa cha kuwasha na kuzima mishumaa. Kwamba mfalme huyo alitembelewa na mgeni nyumbani kwake, bila shaka mgeni huyo alikuwa ni mwandishi wa habari, hivyo alikuwa akimhoji mfalme maswali mbalimbali. Wakati mfalme akihojiwa maswali hayo alikuwa akiwasha mshumaa fulani, mara anauzima na kuwasha mshumaa mwingine kwa kipindi chote cha mahojiano. Kitendo hicho kilimshangaza sana yule mgeni, kwa kuwa hakuwa ameelewa mantiki ya mfalme yule kuwasha na kuzima mara mshumaa ule mara huu, na hatimaye swali la mwisho alimuuliza mfalme yule ni kwanini katika muda wote wa mahojiano alikuwa anawasha na kuzima mishumaa, kwamba ni kwanini baada ya kuwasha mshumaa wa kwanza hakusubiri uishe ndio awashe mshumaa mwingine. Mfalme yule alimjibu kwamba alikuwa akiwasha na kuzima mishumaa ile kulingana na maswali aliyokuwa akiulizwa na mgeni yule, kwamba alikuwa akiulizwa maswali ya kiofisi kama mfalme anawasha mshumaa wa serikali, na pale alipokuwa akiulizwa masuala binafsi yaani yasiyo ya kiofisi kama vile idadi ya watoto wake, wake zake na mifugo yake alikuwa akizima mshumaa wa serikali na kuwasha mshumaa wake, kwa kuwa haikuwa maadili kwake kutumia mali ya serikali kwa mambo yake binafsi.
Baada ya kueleza kisa cha mfalme huyo, sasa ngoja nieleze ni kwa vipi Waziri mkuu Pinda ni fisadi kama walivyo mafisadi wengine nchini. Nilitembelea wilaya ya Mpanda Mkoa mpya wa Katavi mwezi August mwishoni mwaka huu. Nikiwa huko nilishangaa kukuta magari mengi makubwa ya JWTZ yakibeba matofali kutoka Mpanda mjini kuyapeleka Mpimbwe kibaoni nyumbani kwa waziri mkuu. Nikamuuliza dereva mmoja wa magari hayo kama walikuwa wakijenga kambi ya jeshi huko.Akanijibu hapana, hawajengi kambi, wao wapo kule kwa ajili ya kubeba mahindi ya serikali toka Sumbawanga kuyapeleka Mpanda ambapo yanapandishwa kwenye garimoshi kwenda kwenye maghala ya akiba ya taifa kanda ya ziwa. Kwa hiyo wakifika mpanda wakishusha mahindi wanapakia matofari ya kuchoma ya waziri mkuu na kuyasusha kibaoni kwa waziri mkuu umbali wa kama km 100 toka mpanda mjini kisha kuendelea hadi sumbawanga kupakia mahindi, na wanaendelea hivyohivyo. Nilishangaa sana, na nikauliza kwanini basi hakufyatulia matofali hayo hukohuko kibaoni badala ya kufyatulia mjini na kuyabeba kuyapeleka kijijini, akanijibu kwamba kule kibaoni haikuwa rahisi rahisi kwake waziri mkuu kupata wafungwa wa kumfyatulia matofari yale. Hapo nikaelewa kwamba kumbe licha ya kutumia magari ya JWTZ kubeba matofali yake hata hayo matofari katumia rasilimali ya serikali kuyafyatua, na huu ni ufisadi mkubwa uliopitiliza. Kutumia wafungwa kufyatua matofali ya mtu binafsi ni ufisadi, na kutumia magari ya JWTZ kubeba matofali hayo ni ufisadi pia kwa kuwa hata kama magari yale yanapita pale kwa waziri mkuu, lakini bado yanakuwa yametumia muda mwingi wa kupakia na kushusha matofali yale na hivyo zoezi la kubeba mahindi litachukua muda mrefu zaidi kwa sababu yake. Kitendo hicho ni ufisadi mkubwa, na hamna namna yoyote ya waziri mkuu kujitetea kwa hili, na kama ingekuwa ni nchi ya maadili kama nchi za wenzetu hili pekee linatosha kwa waziri mkuu kujiuzulu kwa ufisadi.