Nionavyo mimi: Pinda si mtoto wa mkulima

Pinda ni Fisadi tu hana mpango wowote hana akili zake hazina tofauti na Makamba:coffee:

You are very right. Pinda si mtoto wa mkulima kama anavyopenda tumtambue, ni zao la mafisadi, mtetezi wa mafisadi, dictator mkubwa na mnafiki anayepuliza huku na huku ili mradi tuu matakwa ya mafisadi ( bwana zake ) yatimie. Hana muono wa mbali, anawaadaa wananchi kwa kulia na kujifanya anawatetea kumbe anawanyonga. I hate Pinda and his BOSS
 
kwa kweli mtoto wa mkulima ni kiongoz pekee ambaye Watanzania walikuwa na imani nae, lakin siku za karibun ameanza kuwatia watanzania wasiwasi, kuna tetesi kwamba katika maeneo ya nje ya mji wa Dodoma ana Ranchi yenye takriban ekari 50 na ina ng'ombe wasiopungua 400 na katika maeneo ya kigamboni ana shamba lenye takriban ekari 15 na amelizungushia ukuta wa matofali ambao ungeweza kujenga shule ya kisasa kabisa. je huu ni ubepari (ufisadi) au ndo sifa ya mtoto wa mkulima?
 
Unaweza ukahitajika kudhibitisha hayo unayoyasema; maana mtoto wa mkulima mwenyewe alikwisha zitaja mali alizonazo, hizi unazizitaja wewe hazikuwemo kwenye orodha hiyo, katika hali hiyo watanzania wanayo haki ya kujua ukweli ni upi.
 
kwa kweli mtoto wa mkulima ni kiongoz pekee ambaye Watanzania walikuwa na imani nae, lakin siku za karibun ameanza kuwatia watanzania wasiwasi, kuna tetesi kwamba katika maeneo ya nje ya mji wa Dodoma ana Ranchi yenye takriban ekari 50 na ina ng'ombe wasiopungua 400 na katika maeneo ya kigamboni ana shamba lenye takriban ekari 15 na amelizungushia ukuta wa matofali ambao ungeweza kujenga shule ya kisasa kabisa. je huu ni ubepari (ufisadi) au ndo sifa ya mtoto wa mkulima?

Sorry to say kwamba no research no right to speak! Mpaka sasa hapa unaonekana una habari za kusikia tu kwa watu. Kwa nini usifanye utafiti ukaujua ukweli ndio uanze kudiscuss topics kama hizi?

Kama vipi Mods drop this kwenye jukwaa la udaku/tetesi
 
Kwani mshahara wake anaupeleka wapi,hapaswi kumiliki 'assets'? Kwani umasikini ndio kielelezo cha kuwa msafi/mwadilifu? umasikini ni matokeo yasiyopendezwa na mtu yeyote,kila mtu anatamani kuwa na mali nyingi kadri inavyowezekana ili aishi vizuri hapa duniani.Mtoto wa mkulima kama ulivyo wewe na mimi tunapaswa kuwa na mali halali zinazotosheleza mahitaji yetu.Yaani waziri mkuu,andeleze woga eti ataonekana fisadi kwa kumiliki mali halali,haaa,acheni hizo jamani.
 
Huyu Pinda anae sema yeye ni mtoto wa mkulima ni kweli? Make matendo yake sio kabisa. Maisha anayo ishi na masalani leo anatetea posho za wabunge wakati mwalimu analipwa 120000 kwa mwezi?
MSAFARA WAKE WENYEWE NI MAGARI 40 YENYE THAMANI YA BILIONI NZIMA
 
Asante kwa kuliona hilo wahamasishe na ndugu zako walio vijijini ili itakapofika hiyo 2015 tuiondoe ccm madarakani tofauti na hapo tutalalamika sn bila matumaini yoyote
 
Asante kwa kuliona hilo wahamasishe na ndugu zako walio vijijini ili itakapofika hiyo 2015 tuiondoe ccm madarakani tofauti na hapo tutalalamika sn bila matumaini yoyote

mimi najitahidi sana kuwahamasisha usiku na mchana.
 
Mimi jana huyu jamaa sijamuelewa kabisa,maana posho sikana kwamba watu hawahitaji pesa ila kuchukua posho hizo wanaona hawajawatendea haki wananchi. Kitendo cha kusema kuwa posho hizo zinawasaidia kuwagawia wananchi wengine hiyo nidharau kwahiyo wanataka wananchi wengine wasiwe na maisha mazuri hili wao wapewe hizo posho ili watu wakawatukuze kwa kuona wamewasaidia kumbe ni kodi zao.
 
Ni mtoto wa mkulima kweli. Hajajilimbikizia mali (siyo fisadi). Ni mfumo (system) wa serkali ya CCM ndiyo unamfanya atende atendavyo. Hata wewe ukiingia na kubaki humo utafanya afanyayo Pinda, ingawa kwa shingo upande.
hebu acha upuuuzi wwe.................ka umekosa vya kuchangia tulia na utazame tu
 
lile jamaa nalo bure kabisa linajificha nyuma ya pazia la utoto wa mkulima wakati ni kiungo muhimu ktk maslahi ya mfisadi. kwanza sioni km ana powers zozote zile kazi yake ni kujibu maswali ya wabunge kwa longolongo zisizo na maana yeyote ile. heri hata lowassa alikuwa anaweza simama akagiza kesho nataka kitu flani kifanyike lkn huyu jamaa yeye ni kusikitika tu au kutoa michozi au longolongo tuu yaani porojo tupu. toka PINDA aingie madarakani kuna lolote analofanya likaonekana? yeye ni pokitics tuuu. ndo maana serikali imekuwa laiiini laiiiiiini hakuna utendaji yaaani ni UOGA TUUUUU kweli wa tz tunajuta kwa makosa ya watu waliochakachua matokeo ya uchaguzi
 
Wakuu,kwa maneno na matendo yake huyu jamaa,bado ana jeuri ya kujiita mtoto wa mkulima?
 
Kuzaliwa na mkulima huwa hakubadiliki hata ukifa! Watanzania sie ni wajinga! Pinda ni tajiri tena mwenye kuhodhi ardhi kwa mgongo wa madaraka! Sasa akijiita na kuitwa mtoto wa mkulima hajakosea kwa kuwa baba na mama yake ni wakulima pale sumbawanga!! Labda ulitaka kutueleza nini juu ya huyu binadamu?
 
Ni kiongozi mnyenyekevu na mwepesi kuonyesha sura ya huzuni ili sisi watanzania tumwonee huruma. yeye na spika wetu nawaweka kundi moja kuwa ni waoga na tusitegee maamuzi yoyote yenye maslahi kwa nchi yapitie kwa hawa watu.

 
Tuje kwenye Mashangingi (VX, GX, V8 e.t.c), nilipata imani nae baada ya kudai magari haya ni mzigo kwa serikali but ukweli nilikuja kusononeka kama si kuchanganyikiwa baada ya kumsikia eti alipopewa yeye akalikataa na kudai ''apewe mwingine'',kwa nafasi yake alitakiwa alirudishe lilikotoka au kulipiga mnada kisha amuwajibishe alielileta.ndio kusema unaweza ukaletewa rushwa ukaikataa na kushauri apewe mwingine kisha bado uendelee kujiita msafi
 
inasemekana mtoto wa mkulima anayejiita hivyo anamiliki hisa kunako kampuni ya sumry kwa kiasi kikubwa sana kupitia kampuni moja hiv iliyoko arusha

Haya mtoto wa mkulima ni Mbowe, kazi kujadili maisha ya watu hapa, Mkapa huita 'WIVU WA KIKE' huo, fanya kazi kijana acha unafiki
 
ana shamba ekri mia mbili kule kwao linasimamaiwa na mdogo wake SOSI TBC, huyo sio mkulima kama tulivyozoea ni bepari.......simpendi hana point eti posho wanazigawa mlangoni inasikitisha kama waziri mkuu anahalalisha omba omba badala ya watu kufanya kazi....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom