Nionavyo mimi: Pinda si mtoto wa mkulima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nionavyo mimi: Pinda si mtoto wa mkulima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Negrodemus, Jan 12, 2011.

 1. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #1
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  inasemekana mtoto wa mkulima anayejiita hivyo anamiliki hisa kunako kampuni ya sumry kwa kiasi kikubwa sana kupitia kampuni moja hiv iliyoko arusha
   
 2. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Nafikiri Nick name hii mpya itamfaa huyu PM wetu maana anatumikishwa na hana msimamo wake mwenyewe.

  Pinda anaweza akawa safi, ila mafisadi waligundua Jamaa hana msimamo na anayumbishwa sana wakaamua kumuacha aendelee kwani hana madhara kwao zaidi anakubaliana na matakwa yao.

  Ameshawahi kukiri kwamba mafisadi wana nguvu kuliko serikali, hakika kwa sasa ni mtumwa wa mafisadi ndio maana anaongea kwa kutumwa bila kuwa na utashi wake mwenyewe.

  nasikitika sana Toka Mtoto wa Mkulima sasa amekuwa Mtumwa wa Mafisadi.
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Suala la kuwa eti ni mtoto wa mkulima ndio angeweza kupambana na mafisadi sio kweli, toka mwanzo jamaa ameonyesha hana uwezo wa kupambana na mafisadi, labda kwa kuwa chama chote kimejaa watu wengi wenye tabia za kifisadi!
   
 4. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ameanza kuyumbayumba,,,,,sijui amekosa support au amepoteza muelekeo!!!!
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Vyote tu...kakosa support na uelekeo pia.
   
 6. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,262
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Majuzi juzi wakati mkwere anawasili airport kutoka AU, pinda akiwa pamoja na makamu wa rais, mwema, mkuu wa majeshi etc. pinda alipomuona mkwere anashuka kwenye ngazi ya ndege alianza kupiga makofi kama enzi zile za chama kinajenga nchi, sasa viongozi wengine wote hawakufata alichofanya pinda, Akajishtukia akaacha. Nilikuwa najua huyu jamaa hana meno lakini then and there nikapata uhalisia wake kuwa ni mtu anayemnyenyekea mkwere sana kuliko nilivyodhani awali. Hawezi ku dare hatofanya jipya la aina yeyote.
   
 7. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  ni jambo la kuhuzunisha sana, yani yeye analeta usanii tu hamna maamuzi magumu anayochukua, zaidi ya kujifanya ana huzuni kwa mateso ya watanzania, unafiki mtupu..
   
 8. C

  Commitment Member

  #8
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawasalimu ndugu zangu tena poleni kwa uvumilivu na nstaaratu mkubwa kutokana na majanga tuliyo nayo.

  Binafsi nimekuwa najiuliza kama Pinda ni mtoto wa mkulima kama ambavyo wengi

  wanamuita. Nimegundua si mtoto wa mkulima baada ya kuangalia utendaji wake dhidi

  ya wakandamizaji wa watoto wa wakulima

  1. Kashindwa kama waziri mkuu kusimamia suala la vyuo.
  Vyuoni ndipo watoto wa wakulima wanapatikana, hawana fedha za kujikimu,

  hawana ada za kulipa.

  2. Kashindwa kuhakikisha usanii ndani ya wizara ya nishati unafutwa na suala nyeti

  kama umeme kushughulikiwa. Watoto wa wakulima walioko vyuoni hawasomi

  usiku mana umeme hamna na badala yake wanabakia kuandama kudai hela huku

  mda ukisonga na ujinga mwingi kichwani.

  3. Pinda huyu wanaemwita mtoto wa mkulima ndiye anyeshabikia mauaji wa watoto

  halisi wa wakulima kule arusha. Hawa ndio wakulima halisi ambao haki zao

  zimeporwa.

  4. Ni huyu pinda ndiye aliyesema anaeua alubino nae auawe. Ni waziri mkuu anyejiita

  mtoto wa mkulima mwenye sheria ya njia pinda na shahada ya sheria ya chuo

  kikuu cha Dar-Es-Salaam.

  5. Pinda kama waziri mkuu ameshindwa hata kujua wakati gani wa kutoa ahadi na

  wakati gani wa kushughulikia maswala nyeti. Kila jambo la kitaifa anatoa majibu

  mepesi na ambayo yananifanya nimwite zao la mafisadi.

  Nionavyo mimi:

  Pinda ni mtu anayejua jinsi ya kupooza mambo kwa uwezo wake wa kunyenyekea.

  uwezo wake wa kukiri mbele ya uma na mabosi zake pia cha kutisha yu tayari kulia

  ili kuonyesha kuwa kaguswa.

  Nionavyo mimi pinda hafai kuwa waziri mkuu kwani si mtendaji hana power of

  command ila anaweza akawa katibu wa kuratibu kitu.

  Karibu ndugu tumchambue pinda
   
 9. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ni mtoto wa mkulima kweli. Hajajilimbikizia mali (siyo fisadi). Ni mfumo (system) wa serkali ya CCM ndiyo unamfanya atende atendavyo. Hata wewe ukiingia na kubaki humo utafanya afanyayo Pinda, ingawa kwa shingo upande.
   
 10. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono . Sio mtoto wa mkulima. kisheria ana powers lakini hawezi. Kumbukeni Mrema ndani ya Ccm ya Nyerere
   
 11. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu kuna tofauti kubwa kati ya ccm ile na ccm hii ya wezi, kweli pinda ni mtoton wa mkulima ila mfumo aloukuta una matatizo kubwa kwani umeshikiliwa na mafisadi!!!
   
 12. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Pinda ni Fisadi tu hana mpango wowote hana akili zake hazina tofauti na Makamba:coffee:
   
 13. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Pinda ni nguzo iliyopinda katika mhimili wa nyumba. Hivyo ni lazima nyumba ipinde. Nguzo ya aina hiyo haifai.
   
 14. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ki-a.k.a ni mtoto wa mkulima. Ki-asili pia aweze kuwa mtoto wa mkulima. Lakini yeye ktk nafasi ya PM na hali ilivyo hivi sasa, na utendaji kazi wake ulivyo, binafsi naona si mtoto wa mkulima. Naweza mfananisha na mbwa asiyekuwa na meno, unategemea alarue kitu chochote!
   
 15. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Pinda hana lolote la kijivunia, kiutendaji kwa kuchambua, kufuatilia na kusimamia, heri mara mia mpiga deal Lowassa. Lowassa alikuwa anawakimbiza mchwa wa kwenye halmashauri za miji. Wakurugenzi na Wakuu wa wilaya na vigogo uchwara wa wilayani, walikuwa wanapata shida wakikumbana uso kwa uso na fisadi huyo.

  Pinda yeye ni mtu wa kulalamika, mtoa ahadi na mipango isiyo na tija kwa wakati, pia ni mtu wa kulia lia kama mtoto! Hafai kuwa PM kwa nchi yenye changamoto nyingi kama hii.
   
 16. P

  Paul J Senior Member

  #16
  Mar 3, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Baada ya waziri mkuu kutangazwa, jina la mtoto wa mkulima lilikuwa maarufu sana ikiashiria kuwa yuko pamoja na wananchi wengi wa Tanzania, nilidokeza hapa jamii forums kuwa ili neno mtoto wa mkulima kama tunavyomuita PM liendane naye atalazimika kujiuzuru kama waziri mkuu ili kuonyesha uadilifu wake kwa watoto wa wakulima wenzake. Kwa sasa tunaelekea mwezi wa nne sasa tangia ashike wadhifa huo, je bado anazo sifa za kuitwa mtoto wa mkulima au Mtumwa wa mafisadi?
   
 17. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kujilimbikizia mali siyo kigezo cha kuitwa mtoto wa mkulima. Ukweli ni kwamba Pinda ni msanii anayewahadaa wananchi kwa kutoa kauli safi asizoweza kuzitekeleza. Hebu jiulize, hadi sasa ni jambo kubwa lipi unaloweza kusema kuwa Pinda atakumbukwa na umma wa watanzania kuwa kalisimamia ipasavyo? Alisema mashangingi yasinunuliwe lakini hadi leo ni mashangingi mangapi yamenunuliwa tokea aseme hivyo? Ni tatizo sugu lipi aliloweza kulipatia ufumbuzi kwa kushirikiana na mawaziri wengine? Yeye kama Waziri Mkuu, mbona hatuoni matokeo ya utendaji wake kama ambavyo tumekuwa kukishuhudia kwa Magufuli kila anapopewa wizara, tena yanaonekana ndani ya muda mfupi tu?
  Mimi ninavyojua kwa kiongozi makini kama Magufuli akisema jambo hili lifanyike hivi anapaswa kulisimamia na kuhakikisha linafanyika hivyo hivyo ndani ya muda mfupi.
  Pinda ni msanii na wala siyo mtoto wa mkulima. Hata mali alizowatajia watanzania kuwa anamiliki pia aliwadanganya kwani mshahara wake wa mwezi mmoja ni mkubwa sana na hajawaambia ni wapi huwa anaupeleka ukizingatia kuwa yeye anagharamiwa na serikali kwa kila kitu. Iweje aseme kuwa akaunti yake haizidi hata milioni 30 na awe na vijumba hivyo vichache kama hawekezi sehemu nyingine tatanishi kama wanavyofanya viongozi wengine?.
   
 18. t

  tambarare Senior Member

  #18
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu ndo msanii namba moja kwani ni mnafiki sana kwanza ana hisa nyingi katika kampuni ya sumri
   
 19. N

  Nanu JF-Expert Member

  #19
  Mar 7, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Basic Question: Mtoto wa Mkulima by Definition Kwa Mleta Mada ni Nani?
  Kabla hatujaanza kusema ni mtoto au si mtoto wa Mkulima lazima tujue maana yake.
  Nionavyo mimi: Pinda alisema yeye ni mtoto wa Mkulima kwa maana ya kuwa amezaliwa na mkulima wa Kitanzania (peasant) ambaye kilimo chake ni cha kujikimu hivyo hawana mali na kwa maana nyingine ametoka katika familia ya kimaskini. Sasa kama kuna maana nyingine mlivyoelewa ninyi kwa jinsi alivyojiita mtoto wa mkulima basi tuelezeni lakinis tusipotoshe mambo. Ni vizuri kuwa na "correct heading" katika mada/hoja zetu tunazozileta kwa mjadala.
   
 20. N

  Nanu JF-Expert Member

  #20
  Mar 7, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tupe facts ana hisa ngapi? Tuwekee na nakala kama ikiwezekana ili kuthibitisha hoja yako!!
   
Loading...