Mkereketwa_Huyu
JF-Expert Member
- Feb 19, 2011
- 9,217
- 6,348
Huku ni kukosa ustaarabu kabisa na kuingilia privacy za watu!
Huwezi kumpa namba yangu mtu mwingine bila kuniuliza.
Mkuu Sumba-Wanga, hayajakukuta haya na unaishi hapa Tanzania? Kitu privacy hapa Bongo hakuna yaani ni kama ziro tu, we umelala mtu kapata namba yako ya simu toka kwa mtu mwingine ambaye huna hata mpango naye utaona anakupigia simu na kuongea utumbo. Unashangaa hata na fulani ana namba yako, kaipataje? Mimi niliachwa hoi mwaka jana, yaani jamaa walikuwa wanabishania usajili wa wachezaji wa Yanga kijiweni tu. Katika hali isiyo ya kawaida, jamaa mmoja mlalahoi tu (anazoa takataka hapa mtaani na mkokoteni) kwa hasira akasema Yanga isipotwaa ubingwa mwaka jana angempigia simu Ridhiwani Kikwete amtukane kwani yeye Ridhi anahusika na usajili pale Yanga. Watu wakacheka sana na kumkashifu jamaa. Kwa kuondoa ubishi, jamaa akampigia Ridhiwani simu bahati nzuri Ridhi hakupokea. Toka silu ile mpaka leo jamaa anaitwa mshikaji, yaani kaacha kudharauliwa kisa anaijuwa namba ya simu ya Ridhiwani.
Last edited by a moderator: