Nionavyo Mimi: Hizi ndio Tabia Kuu za Watanzania [Sterio Type] | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nionavyo Mimi: Hizi ndio Tabia Kuu za Watanzania [Sterio Type]

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by DSN, Mar 1, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Previously:
  Taifa lolote utambulika kutoka na tabia za jumla za watu wake,yani zile tambia ambazo watu wengi wanazo ndizo ugeuka kuwa tabia za Taifa.

  Mfano wamarekani walio wengi wanatabia ya ushindani [Competitors] hivyo mpaka leo tabia hiyo ndio imegeuka kuwa alama ya taifa hilo. Waingereza wanatabia ya kujiona [Superior] basi ndiyo alama yao kote Mwingereza ujiona hivyo. Wajerumani wanaonekana kama wababe [Tough] na ndivyo tunavyowaona mpaka kesho, ukitizma ligi ya mpira ya Ujerumani ni ya kibabebabe.

  Hivyo kwa Watanzania tunazo tabia zetu ambazo kwa walio wengi zimekuwa ni tabia za jumla.Kwa mtazmo wangu nimezigawa kwenye makundi mawili.Kundi la kwanza waliozaliwa kabla na baada ya miaka kumi ya uhuru.Na pia kuna wale waliozaliwa baad ya mika kui ya uhuru na kuendelea.

  Tabia hizo ni kama ifuatavyo
  A: Kabla ya Uhuru na miaka Kumi baada ya Uhuru,
  Wazliwa wa kunid hilli wanavijtabia vifuatavyo ambayo kwa ujumla wake ndio tunapata taswila na muonekanao wa Taifa
  1: Unyenyekevu [Uliopitiliza]

  2: Uoga wa Kuhoji Mambo ya Msingi
  [Hasa Kuhoji Matendo Ya Viongozi,Serikali na Mambo Yote Ya Msingi Kwenye Jamii]

  3: Wazuri kwenye Nadhari [Theory]
  Mtanzania wa zama hizo akikijua kitu kwa kukielezea basi ni nadra sana kumtoa nje ya ulingo huo.Ndio maana kwenye makongamano ya kidunia walikuwa wanaheshimika kwa hilo.

  4: Unafiki na Fitina[Hypocrtism]

  [Kwa kuwa mfumo wa enzi za Mwalimu,ulijenga kujua nani anafanya nini na kwa sababu gani,Kwa wakti ule ilikuwa sawa kwa mujibu wa mahitaji ya wakti huo na zama hizo kwa kuwa ilikuwa ni ujenzi wa mwanzo wa Taifa].Lakini matokeo yake unafki huo umeendelea hata baada ya miaka hamsini watu wamekuwa na uchonganishi huo huo wa kuperekeana majungu kwa nia ya kuharibiana,Unaweza kuyaona haya kwenye ofisi za Serikali, Maofisi Mbalimbali ya Kijamii, na hata virabu vyetu vya mpira.Yani mfitinishi ananafsi kubwa ya kuwa na madaraka popote pale kuliko msemakweli.Hasa kwa lika hili la kizazi hiki cha miaka hiyo.

  5: Wavumilivu
  Kizazi hiki ni wavumilivu wa shida mbalimbali za kimaisha na kijamii, hasa wanawake wanaongoza kwa uvumlivu huo

  6: Wivu
  Kizazi hiki kinawivu mbaya sana kuanzia mapenzi, madaraka, maendeleo na mafanikio yoyote ya mwanajamii yoyote,ndio hapa chanzo cha cha wizi na ufisadi ulipoanzia.walianza na wivu wa mapenzi,na hata nyimbo zao nyingi za miaka hiyo zilikua na malalamiko mengi sana juu ya wivu mapenzi.

  7: Hawana Ndoto na Maono [Vision and Dreams]

  Kwa kizazi hicho watu wake walio wengi hawakuwa na ndoto,ndio maana mambo mengi yalikuwa yanaonekana kama vile yalikuwa na picha na usimamizi wa mwalimu na baadhi ya watu wachache na ndio maana, mambo mengi yalioanzishwa na Mwalimu kama viwanda, migodi na mashrika ya Umma yote yalikufa kwa kuwa hakukuwa na watu wenye maono au ndoto.Kwenye hili alijalishi wewe ni mjamaa au wewe ni beberu ndoto ni matamanio unaweza kuona kwa baadhi kuwa mpaka sasa ni watu wakubwa lakini wapo wapo tu.

  8: Hawajui Kusamehe na uwekeana nyongo na visasi
  Ni watanzania ambao hawana kauri ya nisamehe, samahani, yaishe,kwao n msamiati, ndio maana hata wazee wetu ujapata kuwasikia majumbani mwetu wakiambiana samahnai mbele ya Watoto.Hivyo wamekuwa wakihalalisha kuwa wao awagombani na wala hawakosani kitu ambacho ni uongo kwa jamii ya sasa ndio hapa dhana ya unafki unapozuka.Utwaona watu wako kwenye gari wamenuniana wakikuona wanajichekesha kana kuwa mambo yako sawa na hakuna tatizo.Hatima ya unafiki ni kulimbikiza chuki ya kukomoana na kulipiziana visasi.

  9: Wananidhamu ya Woga kwa Walio Na Dhamana Ya Dola.
  Watanzania wengi wa kundi hili ni watu walio na nidhamu mbaya sana ya woga,unyenyekea kwa kiongozi mpaka aibu,kwao wao kiongozi ni Mungu.Walikuwa wanacheka nae jana na kugonganae story za simba na yanga juzi juzi kawa kiongozi, mungu wangu huyu kawa sio Mtu tena kisa kawa kiongozi.Hapa dhana ya unafiki inasimama kiasi kuwa Kiongozi anpokosea hata rafiki zake waliokuwa wanaelezana ukweli kabla hajawa kiongozi hawezi tena kumwambia ukweli huo.

  10: Wanapenda starehe Japo Ujifanya Kwa kizazi cha Sasa Kuwa Si wapenda Starehe
  Ukitaka kmjua mzazi alikuaje angalia watoto wa kizazi hiki wa sasa wanavyopenda starehe, utajua kuwa zama za wazazi hawa walipenda sana starehe.Tena wanaume wa Tanzania wa Miaka hiyo waliongoza sana kwa kupenda starehe.Na walio wengi ndio chanzo cha nyumba ndogo za sasa.Wanawake wa Miaka hiyo kwa Uchache sana walishiriki kustareheka.

  11: Walikuwa na Ushirikiano kidogo walijali walikotoka [extended Family]
  Kwenye kada ya familia na kabila na kidogo ilijengwa mpaka ngazi ya Taifa.Na hata kwenye Mapenzi yao walikuwa na upendo wa kweli na hata nyimbo zao ukizikiliza zina imba mapenzi ya kweli [Real Love] na sio mapenzi ya wizi [Cosmetic Love]

  12: Walijituma kusoma Kwa bidii
  Kwa zama hizi Watanzania hawa kwa elimu walijituma kusoma kwa bidii sana.Na mfumo wa elimu yao ilikuwa kutumikia Serikali hasa ya mkoloni na sio kujenga Taifa.Ndio maana mpaka sasa wengi wao dhana ya Kutenganisha dola na Nchi haipo kabisa akilini mwao yani wanaamini Serikali ndio Nchi na Nchi ndio Serikali.Kumbe Serikali ni Mamlaka inayowekwa na Watu wa Nchi,hivyo Nchi ni Watu na maliasili zao kwa ujumla wake.

  13:Waoga sana Kwa Wageni

  Kundi hili ni kundi ambalo watu wake ni waoga sana kwa wageni hasa wazungu,wahindi na waarabu,ndio wanaoamini kuwa mzungu au mhindi au mwarabu nii tofauti nao [exceptional] hivyo hata wanapo wakuta kwenye maofisi ya umma au pengine popote uwahudumia tofauti kuliko jamii nyingine.Tabia hii imelifikisha hapa taifa kwa sababu ya woga woaga hasa wa kuabudu wageni kuliko wazawa.Na mbaya baba wa Taifa kwa nia njema akaweka zana ya kupinga ubaguzi wa kitabaka basi ikawa msaada mkubwa kwa wezi wa Taifa kuchuma kwa kivuli cha ubaguzi.Wezi wakubwa wa Taifa letu wamekuwa ni wageni,wakifuatwa na wenye uchungu watetezi ugeukia kauri ya baba wa Taifa ya Ukaburu,kumbe kweli makaburu ndio wanatukaburu.
  pengine woga wao umetokana na kutokuwa [exposed] na muingiliano wa wageni hawa labda kupitia televisheni na elimu ya lugha ya kiingereza kuwa kikwazo ch mawasilino kati yao na wageni hao.

  14: Wanamaadili

  Kwa Watanzania walio wengi wa kizazi hiki wanamadili lakini ,kwa baadhi hasa viongozi na watawala Serikalini walio katika kundi hili baadhi wamesaliti maadili yao na kuwafanya mamilioni ya Watanzania wenye maadili hayo kuonekana kuwa kama yamekufa.Japo sasa kuni la mamilioni ya Watanzania wanayataka maoni hayo.

  15: Wanapenda Utamaduni wao
  .
  Watanzania hawa walikuwa wanapenda utamaduni wao yani asili yao kwa kiwango cha kutosha kuweka heshima ya mtu kuheshimu alikotoka na ndugu na wana jamii wote wa eneo la utamaduni wake.

  16: Wanapenda Kazi Aina Yoyote Ya Kazi.
  Watanzania hawa wanapenda kazi na kuwajibika kwenye kazi,tatizo kuu ni kutokuwa na kipimo cha ufanisi wa kazi waifanyayo.


  B: Miaka kumi baada ya Uhuru:
  Kundi hili ni kizazi cha kuanzia miaka ya sabini [1970-mpaka sasa] ni kundi ambalo bado liko kwenye kada ya vijana wakubwa [Makaka], vijana na watoto yaani ndio kundi la kizazi kipya.

  1: Wamerithi Uvumilivu [Ulio na kikomo]
  Hapa unaweza kuona kizazi cha sasa kinavyoweza kuhoji Viongozi,Watawala, na hata familia ya kijana husika.

  2: Wavivu
  Hapa kumekuwa na uvivu mkubwa,ila kosa lake wametwishwa watangulizi wkwa kuwa ndio waliofikisha Taifa hapa lilipo.Lakini kwa hili mimi binafsi bado pamoja na kuwa wanastahi lawama,lakini mlango huo kwa vijana kuondokana na uvivu uko wazi kwa kuepauaka kuona kijana w miaka 24 yuko kwenye Pool Table saa mbili asubi na kiroba cha varuuu.

  3: Jeuri [Agggresiive]
  Kizazi cha sasa ni jeuri sana na kina hasira mbaya sana unaweza kuona kupitia pale wanapomakamata mwizi wao udiliki kumuua chini ya kivuli cha mauaji ya haraiki.Sio tabia nzuri kwa jamii lakini kwa mazingira ya Tanzania tuliyonayo vijana wengi wamegueka kuwa Mangaa kwa kuwa hawana jinsi kwa kuwa hawna sauti ya kutapika machungu yao kwa kuwa toka kwa mzazi amejifunza kuishi na vitu moyoni kwa kuwa hakupata kuona mama au baba anaomba msamaa kwa wanajamii.

  4: Wana Ndoto na Matumaini [Dreams & Vision]

  Kizazi hiki kina ndoto na matumaini makubwa

  5: Wanapenda Starehe

  Kama wazazi wao kizazi hiki kinapenda starehe

  6: Wabinafsi [Selfsh]
  Kizazi hiki wengi wetu ni wabinafsi,na silka hii imetokana na kuibuka kwa tabia ya wazazi wetu walipo anza kuibia umma,ndipo watato nao pia walipoamua kuwa sehemu ya ujenzi wa tabia hiyo.

  7: Hawana Mapenzi ya Ukweli au Ummoja
  Kizazi cha sasa hawana umoja japo kwa sasa wanautafuta kwa hali na mal kwa kuwa wanajua faida yake uko mbele ya safari.Lakini kwenye Mapenzi kizazi cha sasa kimebobea kwenye mapenzi ya uongo [Fake Love] na zaidi udanganyifu wenye hatima mbaya kwa jamii.Tamaa ya fedha imetawala sana kuliko mapenzi ya Kweli.

  8: Walevi
  Vijana walio wengi ni walevi wa kila aina ya kilevi unachopata chini ya uso wa dunia yetu hiii,kuanzia Gongo, bangi, cocaine, konyangi, beer, whisky, brand n.k.

  9: Hawana Uoga dhidi ya Dola au Serikali

  Si waoga kama baba zao kwa dola japo ni waoga swala la kupambana na Polisi kwenye mitafaruku ya kufukuzana na polisi kwenye mitafaruku ya misokoto ya Bangi na Gongo mitaani.

  10: Hawana Uoga dhidi ya Wageni
  Wamekuwa exposed na Mataifa Mengi kwa namna nyingi wakiongozwa na Television, Internet, simu na mengineyo wanajiamini ,sio kwa woga wa kukabilina bali kikwazo ni mawasilino yao na wageni hao hapo ndio tatizo lilipo lala kwa kizazi hicho.Kwa kuwa mamilioni ya Vijana wa Kitanzania walio wengi Kiingereza kimekuwa ni tatizo kuu,lakini kwa ujumla wao hawana uoga kama wa wazazi wao waliokuwa na woga toka huko nyuma.

  11: Hawana Unafiki au Majungu
  Hawana majungu kwa walio wengi ila jamii ya baadhi ya vijana kutokana na mazingira wamekuwa na bidii ya kuufanya mzizi wa majungu upate nafasi.Na hii unaweza kuona kwenye taasiisi mbili kubwa CCM na CDM.Kote huku kuna vijana lakini kila moja ina mfumo wake wa maadili na linapokuja swala la unafiki na majungu unaweza kuona picha ya jinsi taasisi hizi mbili zinavyopambana kila moja kwa namna yake.Zamani majungu yalikuwa mtaji lakini sasa majungu ni hasara.Japo kwa wazee wetu wanaamini kuwa unaweza kujenga jamiii kwa kusikiliza majungu [rumous] za mitaani,na kumbe Taifa litajengwa kwa Ukweli Fact za maisha ya watu Mitaani.

  12: Hawependi Kusoma

  Vijana wengi wa sasa hawapendi kusoma,wanatamani sana mafanikio kwa njia za kati,na si kujituma kusoma,ndio maana hata elimu yetu imekua na utata kwa kizazi hiki cha sasa.Na ukizingatia mitala ya elimu yetu, ni bomu kubwa linakaribia kuiva kwani vijana wengi wanaomaliza vyuo vyetu wengi wao wametoka vyuoni kwa tiketi za kuibia mitihani [Kudesa] na kwa baadhi ya watoto wa kike wamejitoa kwa walimu ili wafanikiwe kwenye mitaani yao.

  14: Wanapenda Njia Fupi [Short Cut]
  Watanzania vijana wa le o wamejifunza tabia mpya ya wazazi wao ya kupenda njia fupi kufikia mafanikio kwtika muda mfupi,kwa lugah ya leo wanasema magumashi.Yani wanatenda mambo ya kuchota au kukwapua kwa haraka chocote kilicho mbele ya maisha yao pasipo kujali jukumu lao kwa wanajamii wengine na maadili ya jamii.

  15: Hawana Maadili
  Kwa Taifa lilipofika kwa vijana kuiga watangulizi wao Vijana wa sasa hawana Maadili ya kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa.


  16: Hawapendi Utamaduni wao
  Kizazi cha sasa kinapenda sana tamaduni za mataifa ya kigeni [Hasa za Kimagharibi] kuliko tamaduni ya Taifa lao,Japo sio kosa lao ni kosa la Seriakali kutokujenga mifumo ya kuhamasisha Jadi na Utamaduni maalumu kwa faida ya kulinda Utaifa kupitia Utamaduni.

  17: Hawapendi Kazi Na Wanachagua Kazi Ya Kufanya.
  Kizazi cha sasa ambacho kimekuwa exposed na Television,Internet na mawasiliano ya Kidunia na kwa mazingira yalichangiwa na mfumo wa Nchi kutokuwa na mfumo wa ujenzi wa mbinu na mikakati ya ujenzi wa Taifa linalotayarisha vijana wake kuchapa kazi hasa sekta binafsi basi kila kitu kwa kijana wa sasa kimewafanya wakose mwelekeo kutegemea kudra za Mungu kukwamuka kwenye maendeleo yake binafsi na kwa Taifa lake

   
 2. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hujakosea hii hali na sababu zote hizi nadhani tulijengewa toka tukiwa mashuleni mfumo wa ujamaa umetuathiri sana cha muhimu ili tubadilike inabidi kubadilisha serikali kwanza kwenda chama kingine ila tukiwa na CCM wazee walewale hali hii haitokwisha man so tujitahidi kwa kampeni mpaka tupate mabadiliko ya kisiasa kwanza!
   
 3. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #3
  Mar 1, 2011
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  correct 99.99%
   
 4. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  tulifundishwa kumuanmini mwalimu na mfumo wake..... saivi watu wameanza kustuka kuwa mfumo wa mwalimu haupo tena!
   
 5. Mlimazunzu

  Mlimazunzu JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 420
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa
   
 6. m

  mwanafyale JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hizi ni tabia zako kima weeeeeeeeeeeeee !
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hizo ni tabia za uzawa wa Baba yako na Mama yako!
   
 8. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  leka amahelu mwalafyale.....
   
 9. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  .. tabia za Wakwere!!
   
 10. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 11. f

  fat faza Member

  #11
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwakfyale toa hoja usishambulie kikaragosi au imekugusa????
   
 12. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Watanzania wa sasa wameshabadilika sio hao uliokua unawajua baba! Tembea sasa hivi uone mabadiliko! freedon is coming soon!
   
 13. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #13
  Apr 25, 2013
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Jamani naomba tuorodheshe tabia zinazokera kwa watz:

  1) Kumpigia mtu simu haipoelewi, na baadaye wala hasumbuki kupiga au kutuma sms
  2) Kupigiwa simu za kila wakati na kukopwa
  3) Kuombwa Vocha
  4)Kukutana na mtu anayejifanya anakufahamu sana na baadaye kukupiga mzinga
  5) Kulalamikia ugumu wa hali ya maisha kila siku na kutochukua hatua yoyote
  6) Kushabikia siasa kama mazoea ya 1947
  7)Kuzaa watoto wengi ukitegemea kwamba ndugu na jamaa watakusaidia kulea
   
 14. Queen Kan

  Queen Kan JF-Expert Member

  #14
  Apr 25, 2013
  Joined: Dec 26, 2012
  Messages: 3,424
  Likes Received: 4,129
  Trophy Points: 280
  Aya mkenya
   
 15. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #15
  Apr 25, 2013
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  Mhhhh?????
   
 16. bubbs

  bubbs JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2013
  Joined: Feb 2, 2013
  Messages: 367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  -kurudia rudia kupiga simu wakati unaona haipokelewi
   
 17. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #17
  Apr 25, 2013
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Labda hajasikia?
  Au anakimbia deni?
   
 18. bubbs

  bubbs JF-Expert Member

  #18
  Apr 25, 2013
  Joined: Feb 2, 2013
  Messages: 367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  -salamu zisizokuwa na mwisho
  mf. Waoooh, mambo?? Za siku? Upo? Mbona umepotea? Uko fresh kabisa? Mambo yanaendeleaje?
  Dahh me huwa niko tu 'yeah yeah'
   
 19. bubbs

  bubbs JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2013
  Joined: Feb 2, 2013
  Messages: 367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  aaah. Ustaarabu ni kupiga simu twice, ile mara ya pili ni kama alikuwa mbali na simu. Other than that ni usumbufu. Wakati naosha vyombo siachagi kazi yangu kupokea simu nayojua si muhimu. Lakini mtu kakazaniiia vitu vyenyewe anavyotaka kukwambia umbea!
   
 20. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2013
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  Yaah naongea utafikiri yeye ndiye aliyepiga simu...
   
Loading...