Nionavyo mimi: CCM ya Rage, Nkhamia na Majimarefu

komredi ngosha

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
382
71
Ijumaa iliopita nilistuka sana wakati nasoma gazeti la Mwananchi. Kwanza kwa habari iliyotolewa na katibu mkuu wa chama tawala kua CHADEMA wamepeleka makomandoo 33 Igunga waliofunzwa Palestina, Libya na Afghanistan.

Nilikua na rafiki yangu komredi Mbasha, niliposoma nikacheka halafu nikadhani labda ni April mosi ! Ok, pia nikaangalia jibu la mwenyekiti wa CHADEMA lilikua laini sana ila katibu wake Dk Slaa alijibu vizuri hoja. Nikajiuliza, kisa cha Mukama kusema hivyo ni nini? Chama kinachomiliki dola kinaropoka ropoka tatizo nini? Chama chenye wabunge wengi nchini na kinachoamini kinapendwa sana mdomo wa nini? Nimekua nikisikia Chama hiki pendwa kuliko vyote kilivyokusanya wanachama wake kwenda Igunga kukipigia kampeni. Kimewakurupusha mpaka wastaafu, tena bila aibu mpaka Rais mstaafu nikashangaa na kujiuliza sana ina maana walio katika chama hawatoshi?! Chama hicho hicho kilichozindua sera ya Kuvua magamba mpaka mbunge wake akajiuzulu kwa tuhuma kikamuomba mtuhumiwa huyo huyo akakipigie kampeni, nikajiuliza tena ina maana tuhuma zake si za kweli au ndio wanamsafisha asifunguliwe mashtaka?

Basi nikahama hiyo habari ya mukama. Nikaona picha ya Rage, maandishi makubwa kua CCM NA CHADEMA SASA WAMEFIKA PABAYA aargh! Kuangalia vizuri he! mtu kajifunga toi kiunoni. Komredi akaniambia, Ngosha bastola hiyo, nikabisha. Mimi ni askari, na bastola haifungwi vile. Nikaona tena kapandisha shati makusudi watu waione he he hee! Kuangalia sura tena, kumbe Rage!

Hawa wanaoitwa waheshimiwa wa CCM wasio na haiba wala uwezo wa kua viongozi wataiharibu nchi. Kwa kutumia kigezo cha kupendwa CCM imeruhusu watu wasiohusika kushika sehemu nyeti za uongozi wa taifa leo tena kwa kutumia gharama kubwa kuwanadi kwa wananchi na hata njia za panya. Jimbo la Shinyanga mjini nilipo mimi Bw Masele hakushinda kura za Maoni, alikua nafasi ya 3. Ila ikatoka amri akawa mgombea. Sitaki kuongelea matokeo ya uchaguzi, kwa heshima ya komredi shelembi. Waulize wakazi wa Shinyanga kama wana Mbunge, watakujibu kwa gadhabu na hasira kali.

Yupo Bw Komba kaimba imba sana kusaidia kampeni za chama nae akapewa ubunge. Sikushangaa kusikia alichofanya Arusha kuvamia mkutano wa chama kingine na kufanya vurugu. Anakuja Rage, kwanza ashukuru angekua jela wala siafiki kua alishinda dhamana kirahisi hivi. Huyu ni mtu wa mpira, tena Simba na Yanga timu zenye malumbano na zisizo na maendeleo miaka nenda rudi. Wenzao Tp Mazembe wanafanya manunuzi ya ndege wao hata basi la wachezaji mpaka wapewe msaada hata uwanja binafsi wa mpira hawana. Nae akapewa zawadi ya ubunge! Unategemea nini zaidi ya propaganda za kichochezi na kuleta uvunjifu wa amani? Niliwahi kupata nae lunch pale Nyerere square mjini Dodoma mwezi mei mwaka huu akiwa na wapambe wake wawili, aliyokua anaongea ni aibu! Nikajiuliza huyu alipataje ubunge? Ndo huyu utasikia kesho waziri?

Katibu mkuu mukama na Rage kama mapacha, huyu kamtuma mwenzake akaropoke uwepo wa makomandoo mwingine akajifunga bastola kiuoni kuonyesha watu kua hali si shwari, chadema wanaleta fujo! Mbaya zaidi wakafanya hila hata habari haikuandikwa zaidi ya picha tu(naamini walitaka picha itoke bila maelezo, kwani wanashindwa nini).

Yupo Nkhamia, wale wale Simba na Yanga. Nilisikia mahojiano yake na BBC akitoa hoja na Zitto kuhusu Posho nikashika kichwa kwa kusikitika, pumba tupu. Nae amepewa ubunge!

Yupo Majimarefu, naogopa simsemi sana asije akanigeuza chura! Wapo pia kina Lady flani walikua wanamziki, wengine huko Bariadi mwaka jana walipokosa ubunge wakapiga ngwara OCD na hawakufunguliwa kesi.

Nachotaka kusema ni kua, kwa kuruhusu watu wasio na sifa kushika nafasi nyeti za nchi, CCM inahatarisha usalama wa taifa hili. (nilitaka kusema wahuni, nikaogopa ban afu ni tusi).

Chonde chonde wazee wa chama tusaidieni wenyewe mashahidi nchi ilipo sasa. Hawa vijana ni misifa tu na kuropoka, wengine kama mukama hawajui siasa. Nadhani mmenisikia, tunaijua nguvu yenu hamuwezi kuachia nchi kirahisi basi rekebisheni hizi kero amani iendelee kuwepo.
 
Na hapo hujataja zile siri za jeshi ambazo Kapuya alizivujisha kwa balozi wa Marekani.
 
Maji mafupi hajui analolifanya bungeni,mi nashangaa magamba walimpitishaje awe mbunge wao,tatizo la mukama kuropoka hovyo kamanda mbowe alishasema tatizo ni kuanza siasa uzeeni.
 
Komredi wewe ni muandishi mzuri sana, style yako ya kuwakilisha ujumbe ni unique ila tu jaribu kuweka paragraphs, iwe ki academic zaidi,tuweze kusoma bila kuchoka akili, muachie nape na capital letters zake yeye analengo la kutu umiza vichwa vyetu...asante kwa kutu letea habari!
 
Mkuu, pamoja na kugoma kuwelka maandishi vizuri, lakini nimejitahidi kusoama.
jibu langu la mshangao wako wa ''chama tawala na chenye dola kinaropoka ropoka''
ccm%2Bevap.jpg
 
Komredi wewe ni muandishi mzuri sana, style yako ya kuwakilisha ujumbe ni unique ila tu jaribu kuweka paragraphs, iwe ki academic zaidi,tuweze kusoma bila kuchoka akili, muachie nape na capital letters zake yeye analengo la kutu umiza vichwa vyetu...asante kwa kutu letea habari!

thanks kaka! Wakati mwingine nitazingatia hilo
 
Maji mafupi hajui analolifanya bungeni,mi nashangaa magamba walimpitishaje awe mbunge wao,tatizo la mukama kuropoka hovyo kamanda mbowe alishasema tatizo ni kuanza siasa uzeeni.

Hata mimi huwa najiuliza mtu kama SUGU alifikaje bungeni. Badala ya kusaidia wapiga kura wake lenyewe linafanya kazi ya kutunga nyimbo za matusi. Jamaa bichwa lake boksi kabisa.
 
KOMREDI NGOSHA ! Asante mkuuu kwa uchambuzi mzuri wa hawa "wahuni" (siogopi ban) hii ndio nchi ya ya hawa hahunii
 
hawa sisiem hawakubaliki kwa sababu za kudharau maamuzi ya watu wengi, kuanzia kwenye chaguzi za chama hadi kwenye mikataba ya limataifa ambayo tunaingia kama nchi wao wanachojali zaidi ni maslahi ya matumbo yao.
 
mkuu nimekusoma vizuri kabisa ,usiwe mwepesi kuvunjika moyo,huku kwenue mtandao tuna majuha kibao wa magwanda ukiwazingatia wata kuletdown.thanks kwa makala yako.
 
Mkuu, pamoja na kugoma kuwelka maandishi vizuri, lakini nimejitahidi kusoama.
jibu langu la mshangao wako wa ''chama tawala na chenye dola kinaropoka ropoka''
ccm%2Bevap.jpg

he he hee! Kweli umenipa jibu. Nimeipenda hii, thanks!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom