Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,658
- 22,255
Kila mwaka polisi huandaa wiki ya usalama barabarani lakini hali ilivyo barabarani ni ileile ya siku zote zaidi ya kuuziwa stika ambazo hazipunguzi ajali! Vurugu za bodaboda na daladala ziko vilevile na pacha wao ajali.
Mimi naona lengo si kudhibiti ajali kwa kuwakumbusha madereva juu ya matumizi sahihi ya barabara, wiki ikiisha hatujulishwi polisi wamekusanya pesa kiasi gani na zimeingizwa kwenye akaunti gani ya serikali.
Ipo haja ya kuubadili mwenendo wa wiki hii ya usalama barabarani isilenge mapato ila ilenge matumizi sahihi ya barabara.