Nionavyo kuhusu uteuzi wa mbatia kuwa mbunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nionavyo kuhusu uteuzi wa mbatia kuwa mbunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makame, May 8, 2012.

 1. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  R
  ais ameonyesha ukomavu kisiasa. Wapinzani wako represented kwenye Bunge, na wapo miongoni mwa Watanzania. Ili Rais awe rational, ni vyema akateua mbunge/wabunge kutoka kambi ya upinzani. Aidha, Mbatia ameonyesha ukomavu kisiasa; kafuta kesi against Mdee kule Kawa, ili kuyamaliza kiutu uzima. Na kwa kuwa alipata shauku ya uongozi, kuwatumikia Watanzania, akawania EALA. Kwa kuona hayo, Rais wa Jamhuri ya Muungano kamteua kuwa Mbunge, ili aweze kutoa michango yake katika Bunge. Mheshimiwa Mbatia ni mwanasiasa, ambaye ameanza carrier yake kwenye opposition. He believes in a strong opposition ambayo ina nidhamu. Aliamua kuachia ya Kawe ili ku introduce concept ya solidarity among opposition parties. Kwa hekima ya Rais, aliona kuwa Mbatia anahitajika atoe michango yake kwenye chombo cha kutunga sheria. Atoe michango kwa uhuru, kwani kutoa upinzani sahihi kunaongeza uwajibikaji na utawala bora. Mheshimiwa Rais amezingatia kuwa yeye ni Rais wa Watanzania wote, Wana CCM na Wasio kuwa CCM. Na amemteua Mbatia kwa kigezo hicho. Rais akishafanya uteuzi wa Mbunge, huwa harudi tena nyuma, na hawezi kumbadilisha mbunge huyo hadi muda wa bunge (Term) uishe.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mimi nadhani JK amefanya makusudi kwa yote alofanya kuijaribu katiba yetu, kuonyesha mapengo yaliyomo na kwamba hakuna kisichowezekana juu ya jua. Sielewi anataka kujenga kitu gani zaidi ya kuvunja nguvu ya upinzani hasa Chadema wanapoongeza hesabu ya wabunge kukihama chama cha ke na hivyo kuipa nguvu NCCR - Mageuzi kimtindo.
   
Loading...