Nionavyo: Azam Energy Drink ina madhara ukiitumia vibaya

Poa poa.
BARIKIWA.
Mkuu ulishanijibu labda nilikuwa sijakuelewa, punguza jazba! Niliuliza kwa kuona umetahadharisha kwa product hiyo moja tu (ya Azam) na wachangiaji wengi wanaiponda hiyo tu as if hizo nyingine ni tofauti na ni bora...!
 
Hiyo "Caffain" naona mnaiona kwenye hizo energy drinks lakini kumbukeni pia kwamba ipo pia kwenye Chai (tea leaves), na Kahawa.
 
Juzi bwana nilipita mahali kuhemea, mara nikaona "Azam Energy Drink", nikachukua moja kwamba wacha niijaribu...kama masiala bwana, nimepiga hivi baada ya kama 15 mins nikaanza kuhisi mabadiliko kama vile uchangamfu mkali kwenye mwili, dezaini nachajiwa dah!

Nikaigeuza chupa kucheki ingredients, si ndo nikaona: "do not drink more than 2 bottles per day", sasa nikaamua kufikiria upande mwingine wa shilingi, kwamba hii kitu ukiitumia wakati wa mambozi kitandani, inaweza boost nguvu za kiume? Sio kwamba nina upungufu, but in a sense of going more rounds bila mwili kuchoka sana nk.

Kuna ambaye kishajaribu?
 
Ingia ktk mtandao wao kisha cheki namba ya customer care uwapigie, waulize, watakujibu!
 
Kama unataka kufa kunywa mkuu,ile unatakiwa unywe after kufanya hivyo yani umechoka I boost mwili urudi ktk hali yake ya kawaida na sio kunywa then ukafanye tendo wee mapigo ya moyo yataenda kasi na utakufa kwenye kifua cha mwanamke Kama wale wazee wanao kunywa Viagra ili wakakomoe
 
MUHIMU KWA MUSTAKABALI WA AFYA YAKO (SOMA)!
Azam_Energy.jpg


Azam Company ni kampuni inayolisha Watanzania na nchi nyingi kusini mwa jangwa la Sahara. Mzee wetu huyu amekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania na nchi jirani zinazotuzunguka kupitia huduma mbalimbali anazotoa, kuanzia usafiri wa majini, vyakula hata vinywaji. Sitasita kumpongeza mzee wetu kwa huduma zako na Mungu atakulipa kwa hili.

Kilichonifanya nikujadili hapa mzee ni hiki kinywaji chako kipya. Watanzania wamekipokea na wanakitumia sana, kifupi kinauzika, huu ndio ukweli. Na mimi kama miongoni mwa wateja wako nikajaribu kukionja kutaka kujua kina ladha gani kinywaji hiki? Kinywaji hiki kinaitwa #‎ENERGY‬-DRINK‬.

Baada ya kufungua na kuonja kwa mara ya kwanza kilinishinda kurudia fundo la pili, nikajua labda huenda ni gesi ngoja nikiache kwa muda kidogo, lakini hata baada ya kukirudia tena bado kilinishinda.

Nikajikuta navutiwa kusoma kimeungwa kwa kutumia viungio gani (ingredients). Hiki nilichokiona ndicho kilichonifanya niandike haya.

Malengo sio kuharibu biashara yako la!, ni kuwajuza Watanzania ambao wengi wetu lugha iliyotumika hapa ni changamoto kuijua, lakini pia wengi wetu huwa hatuna utamaduni wa kusoma hivi vibandiko kabla ya kutumia.

NI NINI NILICHOKIONA NA KIKANISTUA? HIKI HAPA!

1. INGREDIENTS (VIUNGIO)
Water sugar, Carbondioxide, Citric acid (E330), Taurine, Acidity Regulator Sodiumcitrates E331, Colour plain, Caramel E150a,‪ #‎CAFFEINE‬, Inositol, Preservative Potassium Sorbate E 202, Flavouring, Niacin, Pantothenic Acid, Vitamin B6, B12
Baada ya kuandikwa hivi viungia ukiangalia katika chupa hii kilichofatiwa ni muda wa matumizi na mahali kinapozalishwa. Lakini bado sikupata mantiki kwanini kimekuwa kikali mno, kwanini!!

Ghafla katika kudadisi zaidi ndipo chini ya maandishi hayo nikakuta maandishi mengine mapya, tena yamewekwa juu ya wino‪ MWEKUNDU‬ kuashiria TAHADHARI bila kuandikwa neno lenyewe la TAHADHARI.

Maandishi haya yameandikwa katika lugha ya Kiingereza yanasomeka hivi:

"High caffeine content (31.5mg/m100) Taurine(0.03%). Do not Drink More than 2battles per Day, Not suitable for persons Sensitive to Caffeine, Children, Pregnant, Breast feeding women and Avoiding Drinking before sleeping".

‪TAFSIRI‬ YA MANENO‬ HAYA KWA TUSIOJUA!
Ina kiasi kikubwa cha CAFFEINE, Usinywe zaidi ya chupa 2 kwa siku, Haifai kwa watu wenye matatizo na CAFFEINE, haifai kwa watoto, wajawazito, wanamama wanaonyonyesha na mwisho Usitumie muda mfupi kabla ya kwenda kulala kinywaji hiki.

Kwanini usinywe muda mfupi kabla hujakwenda kulala?

Kiwango cha 31.5mg/ml100 za caffeine ni nyingi kwa matumizi ya kawaida hivyo kuna hatari ya blood pressure kushuka ukiwa usingizini na hatimaye ukapoteza maisha, hivyo ni hatari kunywa wakati unakwenda kulala, inaathiri ubongo pia kwa watoto na hata watu wazima, pia kwa wajawazito na wanaonyonyesha.

Sasa Mzee wangu Bakhress ni watanzania wangapi wanatumia kinywaji hiki pasipo kujua? Kuna wajawazito watoto, wazee wote wanakibugia tu hawajui kinachoendelea katika kinywaji hiki mzee.

Sina uhakika, lakini inawezekana kikapita hata kiwango cha kwenye Heinken. Caffeine drink kuna baadhi ya nchi kama Ufaransa, Marekani, Hispania, Uingereza wamepiga marufuku kutokana na athari zake, hasa katika ubong


Hakuna shaka Mzee baada ya muda mfupi wa matumizi ya kinywaji hiki, watanzania wengi hasa kina mama na watoto na hata wanaume watapata matatizo haya;

Mfumo wa ubongo kuathirika (hili halina shaka), Vidonda vya tumbo, kwa wanamama wajawazito wanaobugia pia watazaa watoto wenye matatizo hasa akili kutokana na Ubongo kuathiriwa, wanaonyonyesha pia!

Mzee, kama ujumbe huu utakufikia naomba tuondolee janga hili, maana haya matatizo tuliyonayo yanatushinda. Watanzania wengi wataumia SIKU CHACHE ZIJAZO na hazipo mbali.

Caffeine ni nini?
Caffeine is a central nervous system stimulant of the methylxanthine class of psychoactive drugs. It is the world's most widely consumed psychoactive drug, but unlike many other psychoactive substances,
 

Attachments

  • azm.jpg
    azm.jpg
    58.5 KB · Views: 496
Nashukuru sana mimi nulikua mtumiaji.mzuri sana wa enegy lkn kila.nikitumia nilikua.najisikia vibaya sana. Hata meno huniuma sana. Numejifunza kitu.kuwa nilazima nisome.maelezo kabla sijatumia
 
Mkuu umeongea kitu cha maana sana, ukiangalia jinsi vijana wanavyokunywa hiki kinywaji ni balaa, yaaani wale walevi wa mtaaani hiki ndio kishushio wanakunywa hata vitatu kwa siku. ni hatari sana kuliko tunavyofikiria. By the way uliyesema TBS na TFDA wameisha thibitisha utakunywa tu endelea kunywa, ni afya yako.
 
Nimekunywa twice, ila na mie ninatabia kama yako ya kudadisi, ila nilikuwa naangalia MFD and EXP. Dates ila nilichojifunza maandishi wanayafichaficha sana, yapo katika mviringo wa chupa tena kwa maandishi ambayo kutokana na u-bluu wa chupa ni nguuuumu sana kuyaona, hivi huwa na maana gani?
 
Back
Top Bottom