Rafiki, unapoongelea kuoa inamaana kuwa unataka kufanya hatua muhimu katiak maisha, kwa hilo unahitaji kutanya tafakali na kuamua kwa dhati. Mambo ya kupenda au kupendwa ni kawaida, na ni ubinadamu, lakini kujiingiza katika mapenzi au siyo ni busara, kwa maoni yangu, fanya tafakali na uone nani angekufaa maishani kama mke wako and then tuletee mezani washikaji zako hoja zilizokufanya umchague huyo ili tupeane mawazo. Angalia katika maswala ya mapenzi isianguke wala usimwangushe mpenzi wako bali kwa nia safi na moyo dhabiti fanya uamuzi utakaokufaa wewe na yeye, nikmaanisha familia yenu. Hoja sio tu kuwa tayari kuolewa au kuoa isipokuwa kuwa tayari kupokeana na kupeana kama wana ndoa, pole ole ndugu yangu dunia tambala bovu, vibaya ukilivaa litavurika hadhalani...