mkiluvya
JF-Expert Member
- May 23, 2019
- 802
- 725
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amefanya operesheni ya kuwasaka na kuwakamata mateja mbalimbali ambao wanatumia dawa za kulenya na kufanya uhalifu katika bonde la Jangwani, Ilala, jijini Dar es Salaam.
Lugola ambaye aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan Zungu, kuwasaka mateja hao ambao wanatumia aina mbalimbali ya madawa ya kulenya, baada ya kuona viongozi hao wanawasaka walikimbia katika maeneo ya vijiwe vyao.
Waziri Lugola wakati akiwa katika operesheni hiyo ambayo ilidumu kwa saa moja na nusu kwa kutembelea mitaa mbalimbali ya bonde hilo, alimpigia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala-RPC, ACP Zuberi Chembera, kufika katika eneo hilo huku akiwa na askari kwa ajili ya kuendeleza zoezi hilo.
Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo ya Jangwani, leo, Waziri Lugola alisema wahalifu hawa wanapaswa kusakwa kwa nguvu zote na kukamatwa, kwasababu walishampora mtu katika mitaa hiyo na kumuaa.
“RPC kuanzia muda huu, nakuagiza askari wako waingie mitaani, kuwakamata wahalifu hawa, na nitakuja saa 12 jioni ya leo, kuona wahalifu wote katika bonde hili wamejaa katika kituo cha Msimbazi, na muwakamate wahalifu na sio kuwaonea watu wasiokuwa na makossa,” alisema Lugola.
Lugola aliongeza kuwa, Serikali haiwezi kukaa kimya kufumbia macho matukio ya kiuhalifu ambayo yamekithiri katika eneo hilo na kuwafanya wananchi kutopata usingizi kuhofia kuvamiwa kwa muda wowote usiku au mchana.
Alimtaka Kamanda wa Polisi Mkoa huo, kuendelea kufanya operesheni ya mara kwa mara kuwasaka wahalifu hao ambao wengi