Ninja aongoza operesheni kamata mateja bonde la jangwani

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
741
1,000
picha kangi.jpg

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amefanya operesheni ya kuwasaka na kuwakamata mateja mbalimbali ambao wanatumia dawa za kulenya na kufanya uhalifu katika bonde la Jangwani, Ilala, jijini Dar es Salaam.

Lugola ambaye aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan Zungu, kuwasaka mateja hao ambao wanatumia aina mbalimbali ya madawa ya kulenya, baada ya kuona viongozi hao wanawasaka walikimbia katika maeneo ya vijiwe vyao.

Waziri Lugola wakati akiwa katika operesheni hiyo ambayo ilidumu kwa saa moja na nusu kwa kutembelea mitaa mbalimbali ya bonde hilo, alimpigia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala-RPC, ACP Zuberi Chembera, kufika katika eneo hilo huku akiwa na askari kwa ajili ya kuendeleza zoezi hilo.

Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo ya Jangwani, leo, Waziri Lugola alisema wahalifu hawa wanapaswa kusakwa kwa nguvu zote na kukamatwa, kwasababu walishampora mtu katika mitaa hiyo na kumuaa.

“RPC kuanzia muda huu, nakuagiza askari wako waingie mitaani, kuwakamata wahalifu hawa, na nitakuja saa 12 jioni ya leo, kuona wahalifu wote katika bonde hili wamejaa katika kituo cha Msimbazi, na muwakamate wahalifu na sio kuwaonea watu wasiokuwa na makossa,” alisema Lugola.

Lugola aliongeza kuwa, Serikali haiwezi kukaa kimya kufumbia macho matukio ya kiuhalifu ambayo yamekithiri katika eneo hilo na kuwafanya wananchi kutopata usingizi kuhofia kuvamiwa kwa muda wowote usiku au mchana.

Alimtaka Kamanda wa Polisi Mkoa huo, kuendelea kufanya operesheni ya mara kwa mara kuwasaka wahalifu hao ambao wengi
 
Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
7,416
2,000
Kwa hiyo hiyo kamera ilishindwa kunasa sura za mateja? au hao walio mstari wa mbele ndiyo mateja waliokamatwa?......uandishi wako wa ajabu sana. Subject ni mateja kisha unamuonyesha waziri na mbunge na maafisa wenzao tu.
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
1,896
2,000
Tanzania haiishi vituko,why watanzania wenzangu tumekuwa watu tunaofurahia mihemko?why hatufuati katiba yetu inasemaje?kwanza tujiulize ndani ya katiba yetu who got the power to arrest kisheria?hiyo picha inaonyesha baadhi ya watu wamevalia regalia za chama cha kisiasa,je hawa wana uwezo huo wa kukamata?halafu mtoa hoja unakuja na mapambo ya NINJA KUONGOZA KAMPENI YA UKAMATAJI!!!,wakati tunaelewa hawa ni small fish watakaokamatwa wakati underworld wa biashara hii wanakula maisha na serikali yangu inahangaika na watumiaji uchwara,why hawawakamati mapapa yanayoingiza tonnes za cocaine kwa kutumia mipaka yetu isiyolindwa?why nchi yetu imegeuzwa kuwa ni short cut ya human trafficking kati ya Asia na SA au kati ya North Africa na SA?,NINGEPENDA MY MINISTER utulie na wataalamu wako mfikirie jinsi ya kuifanya nchin yetu iendeshwe kiteknolojia katiak swala la kupambana na wahalifu ,when tutaweza kuzikusanya finger prints za watanzania wote na kuziweka ndani ya central data system?lini tutajitahidi kulinda mipaka yetu kikamilifu kwa kutumia techonolojia?,shame on us leo again tunaamka na kuona kituo cha polisi msimbazi kimejaa mateja!kabla ya waingizaji na wasafirishaji wa drugs .
 
cleverbright

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
1,779
2,000
View attachment 1159345

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amefanya operesheni ya kuwasaka na kuwakamata mateja mbalimbali ambao wanatumia dawa za kulenya na kufanya uhalifu katika bonde la Jangwani, Ilala, jijini Dar es Salaam.

Lugola ambaye aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan Zungu, kuwasaka mateja hao ambao wanatumia aina mbalimbali ya madawa ya kulenya, baada ya kuona viongozi hao wanawasaka walikimbia katika maeneo ya vijiwe vyao.

Waziri Lugola wakati akiwa katika operesheni hiyo ambayo ilidumu kwa saa moja na nusu kwa kutembelea mitaa mbalimbali ya bonde hilo, alimpigia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala-RPC, ACP Zuberi Chembera, kufika katika eneo hilo huku akiwa na askari kwa ajili ya kuendeleza zoezi hilo.

Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo ya Jangwani, leo, Waziri Lugola alisema wahalifu hawa wanapaswa kusakwa kwa nguvu zote na kukamatwa, kwasababu walishampora mtu katika mitaa hiyo na kumuaa.

“RPC kuanzia muda huu, nakuagiza askari wako waingie mitaani, kuwakamata wahalifu hawa, na nitakuja saa 12 jioni ya leo, kuona wahalifu wote katika bonde hili wamejaa katika kituo cha Msimbazi, na muwakamate wahalifu na sio kuwaonea watu wasiokuwa na makossa,” alisema Lugola.

Lugola aliongeza kuwa, Serikali haiwezi kukaa kimya kufumbia macho matukio ya kiuhalifu ambayo yamekithiri katika eneo hilo na kuwafanya wananchi kutopata usingizi kuhofia kuvamiwa kwa muda wowote usiku au mchana.

Alimtaka Kamanda wa Polisi Mkoa huo, kuendelea kufanya operesheni ya mara kwa mara kuwasaka wahalifu hao ambao wengi

Nilitegemea katika hiyo Picha Waziri Kangi Lugola a.k.a Ninja angekuwa mbele kabisa badala yake namuona Yeye ndiyo yupo nyuma kidogo ya hao waliopo mbele yake kabisa. Kulikoni?
 
Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
5,703
2,000
Kwa hiyo hiyo kamera ilishindwa kunasa sura za mateja? au hao walio mstari wa mbele ndiyo mateja waliokamatwa?......uandishi wako wa ajabu sana. Subject ni mateja kisha unamuonyesha waziri na mbunge na maafisa wenzao tu.
Kwani ujamuuuza Zungu apo. Hahaaaa hahaha hahaha hahaha hahaha
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom