Nini utofauti wa degree ya OUT na ya vyuo vya kawaida?

Sanyambila

JF-Expert Member
Jan 24, 2018
339
457
Nimekuwa nikivutiwa kusoma yaani kujiendeleza kimasomo ila kuna minong'ono kuwa digrii zinaweza tofautina ubora kutokana na chuo ulichosomea. Sasa je, nini tofauti ya degree ya chuo kikuu huria na vyuo vingine?

My interest ni kusoma OUT yaani chuo kikuu huria, naomba kujua ili aidha niende OPEN au vyuo vingine.

Naomba kuwasilisha
 
Nlitegemea ona sababu kwa nini mtu achague OPEN na sio vyuo vingine...ila kusema maprofesa wanafanya nini sidhani kama ni sababu yenye mantiki... unasahau kuwa vitu vingine ni personal characters
Mtu achague OUT kwa sababu ni chuo ambacho kwa asilimia kubwa sana unapambana mwenyewe na hii inakufanya uwezo wa kufikiria kuongezeka tofauti na huko kwengine ambapo kila kitu unaandaliwa wewe unaenda kumeza na kwa asilimia chache unapambana wewe, kidogo sana!
 
Sawaa...mawazo yako yaheshimiwe.. Ukija latika swala la kusoma personal nadhan vyuo vingi wanafanya ivo...lkn lazima kuwe na mtu wa kukuongoza
Mtu achague OUT kwa sababu ni chuo ambacho kwa asilimia kubwa sana unapambana mwenyewe na hii inakufanya uwezo wa kufikiria kuongezeka tofauti na huko kwengine ambapo kila kitu unaandaliwa wewe unaenda kumeza na kwa asilimia chache unapambana wewe, kidogo sana!
Sawaa...mawazo yako yaheshimiwe...

open university uses open academic policy... With minimal or no entry qualification.....sijui unaionaje hii policy...
Wanatoa nafasi kwa kila mtu kupata university education regardless the quality ....

personal learning si kipimo cha uwezo wa mtu kufikiri ...
Pia mtu anaye taka kusoma sayansi ya kilimo au uhandisi unafikiri kusoma mwenyewe ndio kutamjenga....

Fikiri tena ...
 
Nenda OUT(angalau kidogo) , kwengine utaenda jifunza ujinga tu hebu watazame waliopitia vyuo tofauti na OUT wapo kama wehu, tizama maprofesa bungeni, serikalini kila mahali yan ni kama walienda kusoma ujinga tu!
Kwani OUT hawana maprofessor? Maprofessor wa kwanza OUT walitoka wapi? Sioni mashiko kwenye jibu lako labda ufafanue zaidi kumsaidia msomaji wako anaetaka afanye maamuzi.
 
Kama OUT inafanya kazi kwa kiwango inachotakiwa kufanya kazi-kupambana mwenyewe sio issue kubwa sana kwani unapata subject guides pamoja na materials za kusoma na mazoezi. Useme kwa mazingira yetu kuna challenge ya kupata hivi vitu vingine kwa mfano vitabu, internet kwa dunia ya sasa, hivyo ukiwa mbali na vituo vya OUT au miji mikuu una kazi ya ziada.
Open University inalenga watu wenye mahitaji maalum au hali maalum vinginevyo inategemewa mtu aende chuo cha kawaida. Open University ipo kupeleka elimu iwafikie wale ambao ki kawaida wasingepata elimu ya kiwango kile na wanauhitaji wa hio elimu.
Challenge kubwa ya Open University education ni commitment na kujituma ili utumie muda vizuri-hili ukiliweza basi mafanikio hayako mbali.

Kuna masomo pia ni magumu kuyasoma kwenye chuo huria (e.g. medicine,engineering) hasa kwenye mazingira ya huku kwetu hivyo lazima uwe na sababu maalum ya kuchagua chuo huria na sio kupambana tu ambako kupo hata vyuo vya kawaida hata kama mpambano wao ni tofauti.

Sababu kubwa ya kuchagua chuo huria ni kuwa na majukumu mengine kwa hiyo unasoma wakati ule baada ya majukumu ya msingi. Kwa wenzetu walioendelea sababu nyingine ni kukosa vigezo vya kawaida vya kudahiliwa vyuo vya kawaida. HUKO NADAHARIA YA OPEN UNIVERSITY NI "MILANGO WAZI". Yaani ukijiona fit unaomba na hawana hiyana kubwa unadahiliwa-unapita kwenye tanuru ukitoka upande wa pili umeiva vinginevyo unatupwa nnje. Hapa kwetu kuna kizungumkuti kuhusu hili ndo maana unasikia mabishano kuhusu hata foundation course na "wanataka" entry qualifications ziwe kama zile za vyuo vya kawaida.
 
open university uses open academic policy... With minimal or no entry qualification.....sijui unaionaje hii policy...
Wanatoa nafasi kwa kila mtu kupata university education regardless the quality ....
Kwa ujumla hapo peusi ndo sababu kubwa (kinadharia) ya kuwa na vyuo huria dunia nzima. Hapo penye nyekundu unaweza kusomeka isivyo, "hawaangalii" unaingia na nini, lakini wanahakikisha wakikupa cheti chao umeiva itakiwavyo (hii ni nadharia).
 
Nimekuwa nikivutiwa kusoma yaani kujiendeleza kimasomo ila kuna minong'ono kuwa digrii zinaweza tofautina ubora kutokana na chuo ulichosomea. Sasa je, nini tofauti ya degree ya chuo kikuu huria na vyuo vingine?

My interest ni kusoma OUT yaani chuo kikuu huria, naomba kujua ili aidha niende OPEN au vyuo vingine.

Naomba kuwasilisha

Kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza ( Degree ) Chuo Kikuu Huria ( OUT ) hakipo vizuri na hata ukimaliza hapo na hiyo ngazi usithubutu kabisa kujiita Msomi pale ukikutana na Wasomi wa kweli waliosoma katika Vyuo Vikuu vingine.

Ila kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili ( Masters Degree ) na Shahada ya Uzamivu ( Doctorate Degree ) Chuo Kikuu Huria ni moja kati ya Vyuo Vikuu shindani, mahiri na bora kabisa kwani ' products ' zake nyingi za ngazi hizo mbili huwa ni nzuri na zilizotukuka kama ambavyo zinapatikana katika Vyuo Vikuu vingine.

Yangu ni hayo tu Mkuu.
 
kivipi mkuu???
 
Kama degree ya OPEN ni sawa na vyuo vingine, Ukienda OPEN jipange some time baadhi ya walimu wao ni wasumbufu sana na hawana muda na mtu. Mwalimu anaweza akakufelisha tu hata miaka 6 kwa somo moja tu. Kama Mwaka huu watajirekebisha wapo poa.

Ila kwa kweli OPEN ni wapuuzi sana, wanajitahidi sana kuifanya shule yao hiyo kuwa ngumu pasipo sababu yeyoye. Muda wote wapo kwa ajili ya kufanya maisha ya Wanachuo wao kuwa Magumu kuliko vyuo vingine.

Wasipo jirekebisha mwaka huu kufelisha pasipo na msingi watakwenda na maji kwa maana wengi wamedrop kusoma Open kwa sababu ya ugumu na comlications za walimu wake.

Utakuta mtu amesota kila kitu anajitafutia mwenyewe Lakini anakuja ku supp kwa marks 2 na wakati mwingi hata marks 1 inamrudisha mtu chuoni kwa mwaka mwingine, Vyuo vingine wapo poa kuna standardised kwa sababu ya maswali kutokueleweka na sababu zingine.

Wakiacha complications na kukifanya chuo kuwa kigumu, Kitakuwa poa.
 
Kama OUT inafanya kazi kwa kiwango inachotakiwa kufanya kazi-kupambana mwenyewe sio issue kubwa sana kwani unapata subject guides pamoja na materials za kusoma na mazoezi. Useme kwa mazingira yetu kuna challenge ya kupata hivi vitu vingine kwa mfano vitabu, internet kwa dunia ya sasa, hivyo ukiwa mbali na vituo vya OUT au miji mikuu una kazi ya ziada.
Open University inalenga watu wenye mahitaji maalum au hali maalum vinginevyo inategemewa mtu aende chuo cha kawaida. Open University ipo kupeleka elimu iwafikie wale ambao ki kawaida wasingepata elimu ya kiwango kile na wanauhitaji wa hio elimu.
Challenge kubwa ya Open University education ni commitment na kujituma ili utumie muda vizuri-hili ukiliweza basi mafanikio hayako mbali.

Kuna masomo pia ni magumu kuyasoma kwenye chuo huria (e.g. medicine,engineering) hasa kwenye mazingira ya huku kwetu hivyo lazima uwe na sababu maalum ya kuchagua chuo huria na sio kupambana tu ambako kupo hata vyuo vya kawaida hata kama mpambano wao ni tofauti.

Sababu kubwa ya kuchagua chuo huria ni kuwa na majukumu mengine kwa hiyo unasoma wakati ule baada ya majukumu ya msingi. Kwa wenzetu walioendelea sababu nyingine ni kukosa vigezo vya kawaida vya kudahiliwa vyuo vya kawaida. HUKO NADAHARIA YA OPEN UNIVERSITY NI "MILANGO WAZI". Yaani ukijiona fit unaomba na hawana hiyana kubwa unadahiliwa-unapita kwenye tanuru ukitoka upande wa pili umeiva vinginevyo unatupwa nnje. Hapa kwetu kuna kizungumkuti kuhusu hili ndo maana unasikia mabishano kuhusu hata foundation course na "wanataka" entry qualifications ziwe kama zile za vyuo vya kawaida.

Pitia prospectus ya OUT
Hivyo ulivyoongea ni uongo mtupu
Kwanza course za medicine na engineering hazipo OUT
Ushauri pitia prospectus ndo uje useme usitunge yako
Sifa unazoingilia vyuo unavyovipamba ndo hizo hizo wanazoingilia OUT
Kwa ushauri pitia prospectus
Afu OUT wako vizuri sana tofauti na unavyofahamu
Ukipitia prospectus utaelewa ila tatizo la watz wanataka majina na advertise kwamba niko mzumbe au udsm au udom hapo naona raha
Kumbe kumbe poor product
 
Kama degree ya OPEN ni sawa na vyuo vingine, Ukienda OPEN jipange some time baadhi ya walimu wao ni wasumbufu sana na hawana muda na mtu. Mwalimu anaweza akakufelisha tu hata miaka 6 kwa somo moja tu. Kama Mwaka huu watajirekebisha wapo poa.

Ila kwa kweli OPEN ni wapuuzi sana, wanajitahidi sana kuifanya shule yao hiyo kuwa ngumu pasipo sababu yeyoye. Muda wote wapo kwa ajili ya kufanya maisha ya Wanachuo wao kuwa Magumu kuliko vyuo vingine.

Wasipo jirekebisha mwaka huu kufelisha pasipo na msingi watakwenda na maji kwa maana wengi wamedrop kusoma Open kwa sababu ya ugumu na comlications za walimu wake.

Utakuta mtu amesota kila kitu anajitafutia mwenyewe Lakini anakuja ku supp kwa marks 2 na wakati mwingi hata marks 1 inamrudisha mtu chuoni kwa mwaka mwingine, Vyuo vingine wapo poa kuna standardised kwa sababu ya maswali kutokueleweka na sababu zingine.

Wakiacha complications na kukifanya chuo kuwa kigumu, Kitakuwa poa.

Sasa kaka unataka upewe huruma ata ukichemka
Mimi nilisoma Ardhi University aisee shule ilikuwa inapelekwa kigumu kweli pale na walimu hawana hiyo huruma unayosema
Sijui kwa private institutions kama Tumaini ,saut,rucu etc labda kama unasema uko sawa ila ivi vyuo vya serikali walimu hawana michezo ya kustanderdize kama usemavyo
Private wanafanya hivyo kwa sababu ni biashara
ila OPEN wako vizuri kuna jamaa yangu anafanya masters OUT saivi wame improve sana kiasi kwamba na mm nimekipenda
Afu si kwamba material unajitafutia hapana unafundishwa online kila kitu na lecturer, na unapewa materials na hand out zote kwa maana vitabu na lectures
Unauliza maswali na kufanya discussion online aisee shule ya OUT iko poa sana Mishe zingine zinasonga,chuoni unaenda kwenye paper tu
Unasoma ata uwe porini kiasi gani ,ingia pitia prospectus ya chuo
Na Mimi nataka nijoin nao MBA
 
Kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza ( Degree ) Chuo Kikuu Huria ( OUT ) hakipo vizuri na hata ukimaliza hapo na hiyo ngazi usithubutu kabisa kujiita Msomi pale ukikutana na Wasomi wa kweli waliosoma katika Vyuo Vikuu vingine.

Ila kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili ( Masters Degree ) na Shahada ya Uzamivu ( Doctorate Degree ) Chuo Kikuu Huria ni moja kati ya Vyuo Vikuu shindani, mahiri na bora kabisa kwani ' products ' zake nyingi za ngazi hizo mbili huwa ni nzuri na zilizotukuka kama ambavyo zinapatikana katika Vyuo Vikuu vingine.

Yangu ni hayo tu Mkuu.

Naunga mkono hoja hapo sina uhakika na first degree kuhusu kutokuwa na ubora kila postgraduate nakubaliana na ww na mm nimeshawika Nipige MBA tangu OUT
Ila kwa kusaidia wanaotaka kujoin undergraduate ni vizuri ungefafanua udhaifu wa OUT kwenye hiyo ngazi
Ahsante
 
Elimu ni kichwa chako mwenyewe tu Hamna cha chuo wala nini,wewe kapige shule usiangalie jina la chuo.Unajua kama unajua unajua tu na kama hujui hujui tu ata ungesoma Harvard University. Elimu ni maarifa sio jina la chuo.
 
Pitia prospectus ya OUT
Hivyo ulivyoongea ni uongo mtupu
Kwanza course za medicine na engineering hazipo OUT
Ushauri pitia prospectus ndo uje useme usitunge yako
Sifa unazoingilia vyuo unavyovipamba ndo hizo hizo wanazoingilia OUT
Kwa ushauri pitia prospectus
Afu OUT wako vizuri sana tofauti na unavyofahamu
Ukipitia prospectus utaelewa ila tatizo la watz wanataka majina na advertise kwamba niko mzumbe au udsm au udom hapo naona raha
Kumbe kumbe poor product
Ni vizuri usome kwa umakini michango ya watu kabla ya kuchangia. Mada ni Nini utofauti wa degree ya OUT na ya vyuo vya kawaida? Na mleta uzi amesema pia "My interest ni kusoma OUT yaani chuo kikuu huria, naomba kujua ili aidha niende OPEN au vyuo vingine". Sasa niambie ni wapi nimeandika uongo. Nimeeleza kuna masomo ambayo pia ni magumu kuyasoma chuo huria nikatoa mfano wa medicine na engineering. Ni kweli hayapo OUT kwani ni magumu kwa chuo kuyafundisha, hivyo kama mtu anataka kuyasoma hayo chuo huria ni vigumu kuyapata. Sioni uongo hapo ni upi. Kuhusu sifa za kuingilia chuo nimeanza kwa kuelezea dhana ya chuo huria kidunia (marsharti machache ya sifa za muombaji) nikamalizia kusema kwa hapa kwetu mambo si hivyo wanataka entry qualifications ziwe kama za vyuo vya kawaida. Na hii ndo ilivyo na wewe ulicho andika hakina tofauti na nilichoandika. Hukusoma kwa umakini uliotakiwa. Sasa hapo nimedanganya nini?
Nimetoa sababu za watu kusoma vyuo huria-wanamajukumu mengine au hawana vigezo vya kuingia moja kwa moja vyuo vya kawaida, hii ni kweli kwa nchi zilizoendelea na nikasema kwa sasa OUT siyo hivyo. Nimeelezea ugumu unaweza kutoka wapi ukisoma OUT, nionyeshe wapi nimeongopa. Kitu ambacho sikufanya nikumwambia aende wapi kwani sijui anataka kusoma nini na mchango wangu naamini utamuwezesha kuamua aende wapi.
 
Back
Top Bottom