NINI UNAKUMBUKA MIAKA 17 YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MWL.JK NYERERE

Ng'wanamangilingili

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
5,705
4,739
Wana JF, leo ni kumbukumbu ya kifo cha MUASISI wa Taifa la Tanzania na waziri mkuu wa kwanza wa tanganyika hatimae rais wa kwanza wa Tanzania huru.

Si vibaya kuchangia chochote au kwa lolote unalolikumbuka au ambalo linakugusa wakati wa uhai wake au alipofikwa na mauti.

Kwa uchache sana binafsi nakumbuka yafuatayo:

*Ilikua zamani nakumbuka mwl akiwa ameshastaafu urais alitembelea kijijini kwetu, shughuli zote zilisimama kwa wiki kadhaa kikijiandaa kumpokea.ndege na wanyama walimwaga damu za kutosha.

*Baba yangu mdogo wakati anasoma shule alikuwa Kaka Mkuu, MWL.JK aliwahi kutembelea shule ni kwao na akashikana nae mkono (shake hands) aliogopewa na kuheshimiwa na kijiji kizima. hadi mikutano ya ndani ya kijiji alihudhuria kwa heshima.

*Nikiwa shule ya msingi (nakumbuka ndio mara yangu ya mwisho kumwona mwl.akiwa hai) alikuja mkoa niliokuwa nasoma, akiambatana na BW Mkapa akiwa raisi, wanafunzi wote Ana walimu tulifunga shule kuelekea eneo la tukio. watu walijipanga barabarani kumlaki, Mkapa aliongea Wageningen wote waliongea ila kila mtu alikuwa anamsubiri MWL.JK a ongee, cha kushangaza ilipofika zamu yake alisimama akaongea maneno machache sana, chini ya dk kama 4 hivi. watu wakapiga na kusambaa.

*La mwisho kabisa kifo cha mwl kilisimamisha mahafali yangu (LY) baada ya kutangazwa tu michango na maandalizi yote vikasitishwa.

Bandika hapa unachokumbuka......
 
Katuachia katiba mbovu kwa makusudi.
Sijui tulimkosea nini huyu mzee.
Nikikumbuka hili jambo nambakizia jina lake tu mengine yoote yanjifuta yenyewe.
 
Nakumbuka mwaka 1964 aliponea chupuchupu kupinduliwa na jeshi la Tanganyika akakimbilia zanzbari
Pia katika miaka ya 1970 yalitokea majaribio mawili ya kumpindua yakiongozwa na akina kambona, na akina Chipaka.
Najiuliza je ? Kama wakati ule watanganyika walikua hawajaelimika kwa kiwango kikubwa ktk maswala yote ya kijamii na kisiasa, kakoswakoswa kupinduliwa mara tatu, Leo hii ingekuaje kama angekua bado yupo madarakani ?
 
“Katiba hii imenipa madaraka makubwa sana, siku atakuja mtu ataitumia atakavyo na kuwa kama Mungu” – Mwl. J.K Nyerere ,
 
Nakumbuka Mwalimu alikuwa msikivu sana.

Alikuwa ana maono makubwa sana
.
Nakumbuka Siku anatoa hotuba mnazi 1 baada yakuongea maneno machache mazito yenye kuumiza mwalimu alilia mbele ya kadamnasi nakusababisha mnazi 1 yote kutawaliwa na vilio.

 
namkumbuka mwalimu mwaka 1987 tulishiikana mikono nilipomvisha skafu hayati Yasser Arafat uwanja wa ndege wa Dodoma na pia namkumbuka kwa mengi tu
 
namkumbuka mwalimu mwaka 1987 tulishiikana mikono nilipomvisha skafu hayati Yasser Arafat uwanja wa ndege wa Dodoma
nakumbuka mwaka 1979 kama c mwalimu Nyerere eneo la Kagera lililopatwa leo na tetemeko la ardhi lingekuwa kwa majirani zetu Uganda
 
Mie nakumbuka tu wachumia tumbo walivyofanya hila ili kumuondoa Mzee huyu
 
Back
Top Bottom