Nini unachokikumbuka kwa mtu ambaye hayupo leo duniani

Von Bismarck

JF-Expert Member
Jul 11, 2018
3,073
6,251
Tulio wai kupoteza watu waliochangia leo kuwa kama tulivyo.

Wana Jf.
Katika kuishi tunakutana na watu wengi sana lakini wapo watu ambao kamwe hatuwezi kuwasahau pindi wanapo tangulia mbele ya haki (kifo).

Hii ni kutokana na sababu nyingi zikiwemo ukaribu, urafiki, undugu pengine Mahusiano yetu na matendo yao.

Nakumbuka Anko alifariki wiki 1 tu baada ya kuanza matibabu ya mkono wangu uliokuwa umevujika! Aliniacha bado sijapona ukweli niliumia na kulia sana japo haikubadili uhalisia.
nakukumbuka Anko X!

Japo nilipona badae ashukuliwe Mungu!

Karibuni wanajamvi kwa kile ulichowai kutendewa au kutenda kwa mtu ambaye hayupo duniani! Kupitia hilo ndio linakufanya umukumbuke!
 
Baba yangu mkubwa nakumbuka mara ya mwisho kumuona alinifurahisha sana endapo alikuwa anaumwa but huchoki msikiliza kwa ucheshi wake pia alikuwa ni maana nzima ya mtu mshuhulikaji ila yote kwa yote rest in peace..
 
Pumzika kwa Amani, Baba yangu rafiki yangu mpenzi, pumzika kwa Amani Kaka yangu ndugu yangu na rafiki yangu .

Pumzika kwa Amani Kaka yangu, pumzika kwa Amani Mama yangu .

Mmeniacha Mpweke ila Mungu ndiye Tumaini langu, najua ni mpango wake juu yangu KUNIACHA PEKE YANGU.

NIna mke, watoto 3 hawa ndiyo Faraja yangu.

Naandika haya nikitiririka Machozi kwenye macho yangu yote Mawili.

Baba Yetu ,Uliye Mbinguni .
Jina lako Litukuzwe,
UFALME WAKO uje, Utakalo Lifanyike

Duniani , kama Mbinguni,Utupe leo mkate wetu wa kila siku, Utusamehe makosa yetu, Kama tunavyowasamehe na sisi wale waliotukosea.Usitutie katika vishawishi lakini Utuokoe na yule mwovu

Kwakuwa UFALME ni Wako na Nguvu na Utukufu hata Milele Ijayo Amina.
 
Naikumbuka kauli moja aliniambia marehemu baba yangu mdogo aliyenilea toka nikiwa na miaka 6 na yy akiwa bado bachelor..

Ilikuwa likizo fupi ya July nikiwa Form6 tukiwa tunatembea "ALINIAMBIA RAFIKI YANGU MWEZI HUU WA 7 NI MGUMU SANA KUPATIKANA HELA ILA CHA KUMSHUKURU MUNGU NI KUWA TUMESHAMALIZA DENI LOTE LA ADA HUDAIWI HATA 100 HIVYO HATA IKITOKEA MUNGU AKANICHUKUA GHAFLA NAAMINI UTAMALIZA SHULE,KAMA WATAKAOBAKI DUNIANI WATASHINDWA KUKUPA POCKET MONEY MM JUKUMU LANGU HAPA DUNIANI NITAKUWA NIMEMALIZA" Ikumbukwe nilikuwa nasoma Private tena Boarding Midlands high school.

Ilikuwa kama mazungumzo tu but usiku wa September 2006 yaani miezi 2 baada ya kauli ile baba yangu mdogo kweli alifariki ghafla usiku wa kuamkia J2 huku nikiwa na appointment ya kuonana naye nyumbani kwa ajili ya kwenda kuchukua Pocket money so nilienda msibani.

Naumiaga sana kila nikikumbuka kauli hii lakini zaidi nikikumbuka mapenzi na malezi aliyonipa baba yangu mdogo kunilea mpaka nimekuwa mtu mxima wa kumaliza kidato cha 6...

Ndugu zangu sio kazi ndogo kumlea mtoto wa kaka yako ukiwa bachelor na akiwa mdogo wa miaka 6 huku baba na mama yake wapo hai..Ni mapenzi mazito sana.

Mola akufutie madhambi yote baba yangu mdogo S.A.R Huko kaburini na kesho siku ya kiama.Amin.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshkaji wangu alinitolea mchango kwenye group la whatsapp ambalo huwa siingii mara kwa mara, iyo siku Nimeingia nnaona jina langu limetoa mchango siku tena siku hiyo hiyo, nikajua tuu ni mwanangu katoa nikamtext thanks bro, akajibu usiwaze bro...usiku wa siku hiyo akafariki kwa ajali akiwa yupo njiani kuja kukutana na mimi

I miss you bro

jaribu kusahau ndgu. Maisha ni safari isiyokuwa na mwenyewe.
 
Mshkaji wangu alinitolea mchango kwenye group la whatsapp ambalo huwa siingii mara kwa mara, iyo siku Nimeingia nnaona jina langu limetoa mchango siku tena siku hiyo hiyo, nikajua tuu ni mwanangu katoa nikamtext thanks bro, akajibu usiwaze bro...usiku wa siku hiyo akafariki kwa ajali akiwa yupo njiani kuja kukutana na mimi

I miss you bro

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakika alijitengeneza hazina binguni
 
Naikumbuka kauli moja aliniambia marehemu baba yangu mdogo aliyenilea toka nikiwa na miaka 6 na yy akiwa bado bachelor..

Ilikuwa likizo fupi ya July nikiwa Form6 tukiwa tunatembea "ALINIAMBIA RAFIKI YANGU MWEZI HUU WA 7 NI MGUMU SANA KUPATIKANA HELA ILA CHA KUMSHUKURU MUNGU NI KUWA TUMESHAMALIZA DENI LOTE LA ADA HUDAIWI HATA 100 HIVYO HATA IKITOKEA MUNGU AKANICHUKUA GHAFLA NAAMINI UTAMALIZA SHULE,KAMA WATAKAOBAKI DUNIANI WATASHINDWA KUKUPA POCKET MONEY MM JUKUMU LANGU HAPA DUNIANI NITAKUWA NIMEMALIZA" Ikumbukwe nilikuwa nasoma Private tena Boarding Midlands high school.

Ilikuwa kama mazungumzo tu but usiku wa September 2006 yaani miezi 2 baada ya kauli ile baba yangu mdogo kweli alifariki ghafla usiku wa kuamkia J2 huku nikiwa na appointment ya kuonana naye nyumbani kwa ajili ya kwenda kuchukua Pocket money so nilienda msibani.

Naumiaga sana kila nikikumbuka kauli hii lakini zaidi nikikumbuka mapenzi na malezi aliyonipa baba yangu mdogo kunilea mpaka nimekuwa mtu mxima wa kumaliza kidato cha 6...

Ndugu zangu sio kazi ndogo kumlea mtoto wa kaka yako ukiwa bachelor na akiwa mdogo wa miaka 6 huku baba na mama yake wapo hai..Ni mapenzi mazito sana.

Mola akufutie madhambi yote baba yangu mdogo S.A.R Huko kaburini na kesho siku ya kiama.Amin.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wachache katika karne hii
 
Namkumbuka sana mtotonwa dada yangu aliyezaliwa akapewa jina langu sababu alifanana sana na mimi. Watu walikuwa wanasema kama ningekuwa mwanaume basi wangesema nilizaa na dada yangu yule mtoto na mimi tulikuwa kama mapacha wanaofanana kabisa na alikuwa ananipenda sana.

Alivyofikisha miaka 2 na nusu aliungua na maji ya moto yaliyopelekea kuchukua uhai wake ni miaka 3 imepita ila bado nakukumbuka sana mwanangu nakumbuka ulivyokuwa unaniita "adodo" akimaanisha mamdogo sauti yako haijawahi kutoka masikioni mwangu.
Nakukumbuka mwanangu kwangu ulikuwa kama first born wangu sasa hivi nina mdogo wako mngekuwa mnacheza pamoja. Uendelee kupumzika kwa amani malaika wangu

Alikuwa ni zaidi ya zawadi kwako.lkn Mungu ni zaidi ya mwanadamu
 
Back
Top Bottom