Nini umuhimu wa EAC anthem.


Jackbauer

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Messages
5,921
Likes
96
Points
145

Jackbauer

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2010
5,921 96 145
Baada ya kupingwa mara kadhaa,hivi karibuni wakuu wa nchi EAC waliidhinisha wimbo wa jumuiya hii.
Yafuatayo ndio maneno yaliomo:

Ee mungu twaomba uilinde,
jumuiya Africa mashariki,
Tuwezeshe kuishi kwa amani,
Tutimize na malengo yetu.

Jumuiya yetu sote tuilinde,
Tuwajibike tuimarike,
Umoja wetu ni nguzo yetu,
Idumu jumuiya yetu.

Uzalendo pia mshikamano,
viwe msingi wa umoja wetu,
natulinde uhuru na amani,
mila zetu na desturi zetu.

Viwandani na hata mashambani,
tufanye kazi zote kwa makini,
tujitoe kwa hali na mali,
Tuijenge jumuia bora.
 

Forum statistics

Threads 1,204,915
Members 457,584
Posts 28,175,597