Nini umuhimu wa bima ndogo gari yangu ikipata ajali?

Kwa maana nyingine hiyo inaitwa third party insurance! Faida yake hasa ni pale unaposababisha ajali kwa mtu mwingine, mtu huyo aweza kugharamiwa matibabu na fidia ya ulemavu au kifo kwa wategemezi!
 
naomba nieleweshwe kabla sijaenda kukata nimeskia watu wengi wanasema kama una bima ndogo gari ikipata ajali hulipwi kitu,sasa ni ya nini na tunakata ili iweje?
Hio inaitwa third party insurance. Mnufaika sio wewe ni mtu utakaemsababishia madhara yeye au mali yake.

Mfano ukimgonga mtu insurance itamlipa huyo mtu. Au ukigonga gari lingine na wewe ukiwa na makosa insurance yako itamlipa huyo mtu ila wewe binafsi utajigharamia.

Ikitokea wewe umegongwa na gari ingine insurance ya aliokugonga itakulipa. Balaa lake wewe ugongwe na mtu asie na insurance umekula hasara.

Pia kuna third party fire and theft hii gari likiibwa au likiungua moto utalipwa.
 
Hii ni vema watu wenye uelewa wa kina kutueleza umuhimu na hata gharama za bima kubwa. Itasaidia sana.
 
Okey, kwa hiyo nikigonga kama sijapelekwa mahakamani trafic wakashauri tu ntengeneze gari ya watu, ndio naweza kwenda kuwaona, au hadi upelekwe mahakamani?
Kimsingi bima halipi fidia ya traffic accident bila kupata hukumu ya mahakama kuthibitisha wewe (mbima wao) ndio umesababisha ajali hiyo! Kuna kiwango maalumu cha kulipwa, huoneshwa pale chini kwenye form ya policy ya kampuni ya bima husika!
NB: make sure ukisababisha ajali, unaripoti kwa mbima wako ndani ya saa 24!
 
Habari za saa hivi wapendwa
Kiukweli nimependa sana hili mada na ombi langu kwa members ni kuhusu kama kuna mtu ambae ana uwelawa na haya mambo ya bima za magari basi aweza kuelezea kiundani yaani aekezee kwa ujumla wake
Bila shaka litakuwa somo zuri kwa members woe
Tafadhali naomba kuwasilisha
 
Waache mambo ya ajabu kama umevunjika umelazwa utoke baada ya mwezi itakuaje, nimeuliza hivyo bz nlipata ajali nkalazwa siku 4 mm ndio nligongwa sikuona msaada wa bima bz gari ya sarikali ndio ilinigonga so yule Dereva ndie aliambiwa anlipe
Ni sahihi kabisa, kama hakuripoti! Lakini mtu sahihi wa kutoa report hapo alikuwa mmiliki wa gari husika!
 
Back
Top Bottom