Nini ukweli kuhusu tuzo hizi?: JK atuzwa Jamaica, Mkapa atuzwa Uganda

Kapwani

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
672
110
Source: Nipashe 27 November 2009 na mwandishi maalumu:

"Gavana Mkuu huyo alisema Jamaica imeamua kutoa nishani hiyo kwa kutambua uongozi imara na uliotukuka wa Rais Kikwete katika nyanja na masuala mengi.
Naye Rais Kikwete ameishukuru Serikali na wananchi wa Jamaica kwa heshima ya kutunukiwa nishani hiyo yenye kuheshimiwa mno katika Jamaica"

Mkapa amepewa tuzo la uongozi bora na mfano wa kuigwa Africa, tena hapa Jamaica imetambua uongozi imara na uliotukuka wa JK....hapa kuna mawili either sisi wa Tz hatutambui mchango wa viongozi wetu kwa sababu nabii hakosi heshima isipokuwa kwao AMA hawa watu wanaowatunukia wanafanya hivyo bila tathmini ya kweli wanapenda tu kuwafurahisha hawa watunukiwa.
Inakera sana kuona mtu huyo huyo katika dunia hiyo hiyo na kazi hiyo hiyo anapata sura mbili tofauti zenye kukinzana sana!

Jamaica: Uongozi imara na uliotukuka kwa JK
Tz: kuna malalamiko kuwa kuna ombwe la uongozi....

Uganda: Uongozi bora na mfano wa kuigwa kwa Mkapa
Tz: Ametumia nafasi yake ya uongozi kujinufaisha na familia yake/ ametuingiza katika mikataba mibovu isiyojali maslahi ya wananchi
Tz: huyu mcha Mungu


Kaaazi kweli kweli


NANYI MTAIFAHAMU HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU

 
Back
Top Bottom