Nini uhalali wa Mke wa Rais kutumia mali ya umma katika shughuli binafsi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini uhalali wa Mke wa Rais kutumia mali ya umma katika shughuli binafsi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Brooklyn, Apr 14, 2011.

 1. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hivi wadau mke wa Rais ni kiongozi wa serikali? Nimesoma vizuri katiba yetu ya JMT, hakuna ibara hata moja inayotamka kutambua nafasi ya mke wa Rais wa JMT na naamini hakuna sheria inayompa madaraka ya kusomewa taarifa za maendeleo ya mikoa, potelea mbali misululu ya magari ya serikali anayoambatana nayo pamoja na yale ya viongozi wanaokwenda kumpokea.

  Ninastaajabishwa na kuendelea kuchezea hovyo hovyo rasilimali za taifa hili katika mambo yasiyo na tija. Picha hapo chini zinaonyesha viongozi wa mkoa wa Lindi waliokwenda kumpokea mke wa rais. Naamini WAMA ni taasisi ya binafsi ya mke wa rais na maswahiba wake, ingawa anatumia nafasi na ushawishi aliyonayo pale ikulu ku solicit misaada kutoka kwa wafadhili ambayo hatujui nani ananufaka mwisho wa siku. Nasema hivi kwa sababu taasisi ya mke wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, tuliambiwa ni ya kwake binafsi. Kwa hivyo mumewe alipoondoka madarakani, naye akaondoka na taasisi yake.

  Wakati wa kampeni za kuwania Urais mwaka jana, Mama Salma alidiriki kutumia ndege za serikali kumkampenia mume wake Mh. Rais Kikwete.

  Wana JF mnalionaje hili? Binafsi linanikwaza sana!!

  [​IMG]

  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) mama Salma Kikwete akipokewa na viongozi mkoa wa Lindi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mkoani Lindi leo. Mama Salma Kikwete yuko mkoani humo kushiriki na kuhimiza shughuli za maendeleo ya wananchi.(Picha na Aron Msigwa – MAELEZO).


  [​IMG]

   
 2. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  He huyu mama amerudi tena, ngoja tuone vituko vyake sababu hii ndo ngwe ya mwisho
   
 3. d

  defence JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Aug 13, 2008
  Messages: 508
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 60
  Jamani nadhani kwa Dar amepunguza kidogo safari zake za kwenda kusuka na kumwangalia
  mjukuu wake mikocheni nadhani atakuwa anapita kimya kimya, au msusi anakuja mjengoni
  na mjukuu anapelekwa mjengoni,huko kwao maadam bado wako kizani ndiyo anayaendeleza haya
  2nayoyaona,na huyu askari anyampigia saluti yawezekana anatafuta fadhila za kupandishwa
  ka cheo maana sina uhakika wakati anasomeshwa kozi zake za ukamanda kuna mahali alionyeshwa
  nafasi ya mke wa rais na heshima anayotakiwa kupewa, la yawezekana ni askari wa voda fasta
   
 4. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  mnh si kulikuwa na thread mliyosema haonekani humu????
  akionekana kufatilia shughuli za maendeleo shida,akitulia nyumbani kwake bila kuonekana kny media napo shida,mama salma has difficult time haswaaa...:bored::noidea:
   
 5. k

  kakini Senior Member

  #5
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  We mwenyewe si waona wanaompokea ni mazuzu
   
 6. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Askari wa KK security nini? Siielewi uniform yake.
   
 7. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Afisa Uhamiaji.....
   
 8. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Wivu wa kike, mnajua muda anaoutumia kulala bila ya mumewe pembeni yake?
   
 9. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Nikina mama wangapi wenye shida hii au ni yeye tu?
   
 10. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  huko ni kufuja pesa za umma. hamna lingine zaidi
   
 11. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ushamba na ujinga wetu vinatugharimu sana kwa kweli!!
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ndio maana tunahitaji katiba mpya. Jukumu la first lady lazima lieleweke kama ilivyo katika nchi za wenzetu waliokwishapitia huko. Marekani huwezi kumwona mke wa Obama akipokelewa na wakuu wa jiji la Chicago anapokwenda kutembelea ndugu zake. na Shughuli zake za kiserikali zinaeleweka kabisa.
   
 13. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  katika hata itifaki huwa anawekwa tu lakini kimsingi hata katiba yao haionyeshi ni wapi na yy anaweza akapewa periority wat i know iz yy anapewa heshima pindi anapokuwa na mheshimiwa basi ss hili la yy kwenda Lindi harafu anapokelewa namna hy duh linaniacha hoi kidogo wadau fafanueni
   
 14. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Tafadhali wadau tufafanulieni, mi binafsi naona ni matumizi mabaya ya madaraka pamoja na rasilimali za taifa. Kwa mwendo huu katiba mpya inahitajika haraka; na anastahili kufunguliwa kesi.
   
 15. r

  rombo Member

  #15
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi yenu nyie humu ni majungu tu,hayatakaa yawasaidie,kama huyu mama anawakera oeni wa kwenu then gombeeni urais then mmweke ndani akisubiria misaada kutoka kwenu.Hivi ni lini waTz mtaendelea,yani unaweza kukuta mtoto wa kiume umekalia majungu tuuu,umbea tuuuuu kama mtoto wa kike unayesubiria kuchumbiwa!!!!!!!!!!!!!Mbona mama Maria Nyerere alikuwa anatumia vyombo vya Serikali,mbona mama Sity mwinyi alitumia,mbona mama Mkapa alitumia tena sana tu,yote hayo hamkuyaona,hebu kueni kiakili,hata mkifanya jungu la namna gani mama wa watu atendelea kulindwa na usalama wa Taifa,atatumia vyombo vya serikali kama kawa tena sana tuuu,kama nyie hamuoni matunda ya kazi zake basi kuna waTz wanaona afterall siyo lazima wote turidhike na kila anachokifanya.
  Kama imewauma sana kwa First Lady kutumia na kupokelewa na viongozi wa kitaifa,basi mpigieni kura huyo Slaa wenu mwenye Demu badala ya mke,yeye ndo hataruhusiwa kutumia hata ngao ya Taifa mana ni Demu tu na wala si mke.
  KA VIPI PASUKENI,BADALA YA UMBEA TUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU,MNAKERA SIKU HIZI,UCHAGUZI UMEKWISHA MMEKOSA VYA MAANA KUONGELEA MMEANZA KUWASAKAMA WENZENU,BADALA YA KUPOST TAKATAKA KAMA HIZO NI BORA MUENDE KJIJINI MKALIME NDUGU ZANGU.gO gO gO gO,Salma Kikwete GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOoo.Never lose focus.
   
 16. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  salma wa rombo, karibu sana jamvini!

  maoni haya ni uthibitisho mwingine kuwa ushamba na ujinga wetu vinatugharimu sana kwa kweli!!
   
 17. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #17
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,183
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  rombo SHUT UP PLS,WEWE INAWEZEKANA HUELEWI UPEPO WA DUNIA UNAVUMA VP DUNIA YA LEO
  *FIRST LADY CANADA ANAPELEKA WATOTO WAKE SHULE KWA PIKIPIKI.*FIRST LADY UINGEREZA ANAPANDA TRENI KWENDA KAZINI*RAIS KAGAME ANAENDESHA GARI KUPELEKA WATOTO SHULENI NA NDIO ANAENDA OFISINI BILA MSAFARA MKUBWÀ(MAGARI MANNE TU)
  *JE KWA UTAJIRI GANI TULIONAO HAPA KWETU HUYU MAMA ANAFANYA HAYOO??...
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Bado sijaelewa kwanini anapigiwa saluti!?
   
 19. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #19
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Akili yako imeishia hapo. Mbona waromba hawana akili mgando kama wewe?
   
 20. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #20
  Apr 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ni huu mfumo wetu wa kufanya kazi kwa kujikomba hovyo hovyo unakuwa kama zuzu!! Hao maaskari wanajua kabisa hapo wasipopiga saluti ujumbe ukafika kwa mzee kazi hawana...
   
Loading...