Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,623
- 154,972
Mwanadamu yeyote kitu anachotarajia kabisa maishani ni furaha na amani. Utataka upate mpenzi mzuri, mrembo kuliko wote ili akupe furaha.
Mwanamke atataka mpenzi mwenye hela, mcha Mungu, mpole, etc akitarajia furaha. Utataka gari Kali sio kwamba likusafirishe tu, Bali pia likubebee jina lako mbele ya jamii, watu wakuheshimu na upate furaha. Furaha limekuwa jambo adimu sana kwa raia wa Tanzania 🇹🇿. Tanzania 🇹🇿 ni ya nne duniani kwa kukosa furaha.
Je, nini ufanye ili uwe na furaha siku zote unapotumia mitandao ya kijamii? Kwanza usitegemee kupewa au kupata furaha kutoka kwa mtu mwingine.
Mitandao ya kijamii imejaa watu wenye msongo mkali wa mawazo, watu wenye chuki, watu walioumizwa na maisha, watu dhalimu kabisa. Je, watu wa namna hii ambao wao binafsi hawana furaha watawezaje kukufurahisha wewe?
1. Jifunze kuongelesha utu wako wa Ndani kwamba wewe una nguvu ya kuvumilia changamoto zozote bila kupoteza furaha.
2. Tegemea matusi, kashfa, kejeli, dharau etc Kisha ujiambie "mbona hamna kitu kipya hapa"?
3. Mpuuze yeyote mwenye kukutusi, usimjibu, au ukimjibu mwambie hilo tusi lako ni la kizamani sana, limeshapitwa na wakati na wala haliumizi tena, nitafutie tusi jipya huenda likaniumiza kidogo. Kwa jibu hilo utamfanya mtukanaji wako apoteze nguvu za kutukana zaidi na ajione mpumbavu. Pia, unaweza kumuuliza, kwa kunitukana account yako bank imeongezeka kiasi gani? Basi leo nitukane hadi uwe tajiri kama Mzee Mengi.
4. Mind your own business. Jukwaani usitegemee kumfurahisha kila mtu. Yesu mwenyewe aliyekuwa anafufua watu hakuweza kumfurahisha kila mtu, akaishia kuuliwa kifo Cha aibu, wewe ni Nani uweze?
5. Fuata kanuni, taratibu, masharti na sheria zinazoendesha huo mtandao wa kijamii. Hii itakufanya uishi maisha mepesi na kujiepusha na adhabu za kupigwa ban etc kitu kinachoweza kukuletea stress. Huwa tunaona watu wakipigwa ban wanavyounda ID mpya na kuja na mapovu.
6. Usimtukane mtu, Wala kumshambulia yeyote. Hii itakuepusha na mifarakano. Hamna mfarakano uletao raha.
Hapa nimeorodhesha machache tu, na wewe unaweza kuongezea nyama na matango pori kidogo ya mbinu unazotumia kulinda furaha yako.
Mtu kama Mshana Jr, anaitwa majina mabaya, anasemwa mchawi etc lakini humuoni akikasirika wala kuhamaki kwenye majibu yake.
Pascal Mayalla amekuwa akishambuliwa Sana, akipewa tuhma nzito za kumchongea Eric Kabendera lakini kwenye majibu yake hukuona hamaki, taharuki, wala kashfa na matusi kwa waliomtuhumu.
Kila bandiko lake ni mlango wa yeye kusemwa vibaya lakini anayashinda yote.