Nini ufanye ili uwe na furaha siku zote unapotumia mitandao ya kijamii, hasa JamiiForums?

Mla Bata

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
5,273
2,000
Simply tu sijawahi kuchukulia maisha ya humu mitandaoni serious though wapo watu wengi wanapata michongo ya pesa, kazi, wenza wa maisha n.k lakini lengo langu kuu kuingia JF ni kuburudika & kurefresh na ndio maana kuna majukwaa hata kwa bahati mbaya huwezi kunikuta humo na hata nikipita basi ni kimyakimya pasipo kuacha hata alama ya unyayo.
 

Mla Bata

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
5,273
2,000
Kitu kingine kinachowaponza wengi humu hasa hawa upcomings ni kutaka recognition na cheap popularity, kwa muda mfupi tu mtu kaingia JF anakuja na speed ya ajabu kila sehemu utamkuta tena pasi na content yeyote ili mradi kaonekana tu, wengine wanaenda mbali mpaka kutukana watu ama ku spit shits ili mradi wapate kuonekana na kuongelewa, mwisho wa siku kinachofuata ndani ya muda mfupi mtu kashaingia kwenye fights na watu zaidi ya kumi πŸ˜….
 

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,529
2,000
Kitu kingine kinachowaponza wengi humu hasa hawa upcomings ni kutaka recognition na cheap popularity, kwa muda mfupi tu mtu kaingia JF anakuja na speed ya ajabu kila sehemu utamkuta tena pasi na content yeyote ili mradi kaonekana tu, wengine wanaenda mbali mpaka kutukana watu ama ku spit shits ili mradi wapate kuonekana na kuongelewa, mwisho wa siku kinachofuata ndani ya muda mfupi mtu kashaingia kwenye fights na watu zaidi ya kumi πŸ˜….
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚yani ni shida kuna watu inabidi wapimwa akili wakishambuliwa wanakuja na ID mpya kila kukicha wahusika ni walewale
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
172,932
2,000
Wee jamaa, eti ninavyokufurahia Kuna watu wanakereka, hivi Leo umevaa viatu gani nije kuvilamba mpaka vipungue size?
Buji tunafahamiana in person achana na watu wasiojua matumizi sahihi ya utambulisho bandia... Hao wana guts za kuandika vile kwakuwa hawako kwenye uhalisia wao... Ukikutana nao ni waoga wachovu waliopigika hasa kimaisha...
Kwa njia ile ya kuwachukia wengine bila sababu wanajitambulisha kwa sauti kubwa uhalisia wao na wanapata nafuu

Jr
 

Bujibuji Simba Nyanaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
61,726
2,000
Buji tunafahamiana in person achana na watu wasiojua matumizi sahihi ya utambulisho bandia... Hao wana guts za kuandika vile kwakuwa hawako kwenye uhalisia wao... Ukikutana nao ni waoga wachovu waliopigika hasa kimaisha...
Kwa njia ile ya kuwachukia wengine bila sababu wanajitambulisha kwa sauti kubwa uhalisia wao na wanapata nafuu

Jr
πŸ™πŸ™πŸ™πŸ‘
 

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
31,659
2,000
Mwanadamu yeyote kitu anachotarajia kabisa maishani ni furaha na amani. Utataka upate mpenzi mzuri, mrembo kuliko wote ili akupe furaha.

Mwanamke atataka mpenzi mwenye hela, mcha Mungu, mpole, etc akitarajia furaha. Utataka gari Kali sio kwamba likusafirishe tu, Bali pia likubebee jina lako mbele ya jamii, watu wakuheshimu na upate furaha. Furaha limekuwa jambo adimu sana kwa raia wa Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ. Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ ni ya nne duniani kwa kukosa furaha.

Je, nini ufanye ili uwe na furaha siku zote unapotumia mitandao ya kijamii? Kwanza usitegemee kupewa au kupata furaha kutoka kwa mtu mwingine.

Mitandao ya kijamii imejaa watu wenye msongo mkali wa mawazo, watu wenye chuki, watu walioumizwa na maisha, watu dhalimu kabisa. Je, watu wa namna hii ambao wao binafsi hawana furaha watawezaje kukufurahisha wewe?

1. Jifunze kuongelesha utu wako wa Ndani kwamba wewe una nguvu ya kuvumilia changamoto zozote bila kupoteza furaha.

2. Tegemea matusi, kashfa, kejeli, dharau etc Kisha ujiambie "mbona hamna kitu kipya hapa"?

3. Mpuuze yeyote mwenye kukutusi, usimjibu, au ukimjibu mwambie hilo tusi lako ni la kizamani sana, limeshapitwa na wakati na wala haliumizi tena, nitafutie tusi jipya huenda likaniumiza kidogo. Kwa jibu hilo utamfanya mtukanaji wako apoteze nguvu za kutukana zaidi na ajione mpumbavu. Pia, unaweza kumuuliza, kwa kunitukana account yako bank imeongezeka kiasi gani? Basi leo nitukane hadi uwe tajiri kama Mzee Mengi.

4. Mind your own business. Jukwaani usitegemee kumfurahisha kila mtu. Yesu mwenyewe aliyekuwa anafufua watu hakuweza kumfurahisha kila mtu, akaishia kuuliwa kifo Cha aibu, wewe ni Nani uweze?

5. Fuata kanuni, taratibu, masharti na sheria zinazoendesha huo mtandao wa kijamii. Hii itakufanya uishi maisha mepesi na kujiepusha na adhabu za kupigwa ban etc kitu kinachoweza kukuletea stress. Huwa tunaona watu wakipigwa ban wanavyounda ID mpya na kuja na mapovu.

6. Usimtukane mtu, Wala kumshambulia yeyote. Hii itakuepusha na mifarakano. Hamna mfarakano uletao raha.
Hapa nimeorodhesha machache tu, na wewe unaweza kuongezea nyama na matango pori kidogo ya mbinu unazotumia kulinda furaha yako.

Mtu kama Mshana Jr, anaitwa majina mabaya, anasemwa mchawi etc lakini humuoni akikasirika wala kuhamaki kwenye majibu yake.

Pascal Mayalla amekuwa akishambuliwa Sana, akipewa tuhma nzito za kumchongea Eric Kabendera lakini kwenye majibu yake hukuona hamaki, taharuki, wala kashfa na matusi kwa waliomtuhumu.

Kila bandiko lake ni mlango wa yeye kusemwa vibaya lakini anayashinda yote.
Siasani asilimia kubwa take it as a joke...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom