Nini ufanye ili uwe na furaha siku zote unapotumia mitandao ya kijamii, hasa JamiiForums?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,605
154,916
Mwanadamu yeyote kitu anachotarajia kabisa maishani ni furaha na amani. Utataka upate mpenzi mzuri, mrembo kuliko wote ili akupe furaha.

Mwanamke atataka mpenzi mwenye hela, mcha Mungu, mpole, etc akitarajia furaha. Utataka gari Kali sio kwamba likusafirishe tu, Bali pia likubebee jina lako mbele ya jamii, watu wakuheshimu na upate furaha. Furaha limekuwa jambo adimu sana kwa raia wa Tanzania 🇹🇿. Tanzania 🇹🇿 ni ya nne duniani kwa kukosa furaha.

Je, nini ufanye ili uwe na furaha siku zote unapotumia mitandao ya kijamii? Kwanza usitegemee kupewa au kupata furaha kutoka kwa mtu mwingine.

Mitandao ya kijamii imejaa watu wenye msongo mkali wa mawazo, watu wenye chuki, watu walioumizwa na maisha, watu dhalimu kabisa. Je, watu wa namna hii ambao wao binafsi hawana furaha watawezaje kukufurahisha wewe?

1. Jifunze kuongelesha utu wako wa Ndani kwamba wewe una nguvu ya kuvumilia changamoto zozote bila kupoteza furaha.

2. Tegemea matusi, kashfa, kejeli, dharau etc Kisha ujiambie "mbona hamna kitu kipya hapa"?

3. Mpuuze yeyote mwenye kukutusi, usimjibu, au ukimjibu mwambie hilo tusi lako ni la kizamani sana, limeshapitwa na wakati na wala haliumizi tena, nitafutie tusi jipya huenda likaniumiza kidogo. Kwa jibu hilo utamfanya mtukanaji wako apoteze nguvu za kutukana zaidi na ajione mpumbavu. Pia, unaweza kumuuliza, kwa kunitukana account yako bank imeongezeka kiasi gani? Basi leo nitukane hadi uwe tajiri kama Mzee Mengi.

4. Mind your own business. Jukwaani usitegemee kumfurahisha kila mtu. Yesu mwenyewe aliyekuwa anafufua watu hakuweza kumfurahisha kila mtu, akaishia kuuliwa kifo Cha aibu, wewe ni Nani uweze?

5. Fuata kanuni, taratibu, masharti na sheria zinazoendesha huo mtandao wa kijamii. Hii itakufanya uishi maisha mepesi na kujiepusha na adhabu za kupigwa ban etc kitu kinachoweza kukuletea stress. Huwa tunaona watu wakipigwa ban wanavyounda ID mpya na kuja na mapovu.

6. Usimtukane mtu, Wala kumshambulia yeyote. Hii itakuepusha na mifarakano. Hamna mfarakano uletao raha.
Hapa nimeorodhesha machache tu, na wewe unaweza kuongezea nyama na matango pori kidogo ya mbinu unazotumia kulinda furaha yako.

Mtu kama Mshana Jr, anaitwa majina mabaya, anasemwa mchawi etc lakini humuoni akikasirika wala kuhamaki kwenye majibu yake.

Pascal Mayalla amekuwa akishambuliwa Sana, akipewa tuhma nzito za kumchongea Eric Kabendera lakini kwenye majibu yake hukuona hamaki, taharuki, wala kashfa na matusi kwa waliomtuhumu.

Kila bandiko lake ni mlango wa yeye kusemwa vibaya lakini anayashinda yote.
 
Kwanza kuna Majukwaa kama la siasa siwezi pita hata kwa bahati mbaya kwa afya yangu.

Pia Jukwaa hili la Habari na Hoja mchanganyiko. Mambo mengi Sitaki kuyachukulia serious (kwa Wanaokutana na comments zangu wananijua), maana mengi ni changamsha genge na unakuta hata mwandishi wa uzi kaandikia Bar, unakuta mtu anasifia maisha yake, wewe na wivu wako unaumia unaanza kumuwakia, kumbe maskini wa watu anajifariji.

Kupenda ligi nako mara nyingi Huishia kwenye Ugomvi.

Ila kiukweli kuna watu wanapata moto haraka sana humu, yani mtu kitu kidogo tuu anageuka mbogo, Hawa ndio wale unakuta simu zao zimepasuka vioo kumbe ni ku typ kwa hasira.

Unakuta mtu ana typ mikono inatetemeka, kang'ata meno, anasunya mpaka jasho linamtoka. Huku ni kujishushia Immune tu, watu waanike maturubai.
 
Usitegemee kupewa au kupata furaha kutoka kwa mtu mwingine.

Pascal Mayalla amekuwa akishambuliwa sana, akipewa tuhuma nzito lakini kwenye majibu yake hukuona hamaki, taharuki, wala kashfa na matusi kwa waliomtuhumu.
Kila bandiko lake ni mlango wa yeye kusemwa vibaya lakini anayashinda yote
Mkuu Bujibuji, kwanza naunga mkono hoja, raha jipe mwenyewe!
Asante kunianzishia siku yangu vizuri.

It's true mimi ni mtu mwenye furaha wakati wote hata katika magumu ninayopitia sasa. Siri ya furaha yangu ni kuwa mtu wa shukrani kwa kushukuru kwa mazuri yote na pia kushukuru na kwa mabaya pia maana ni muumini wa karma, hivyo kila thread ninayofungua, kitu cha kwanza ni kummwagia thanks thread starter hata kama ameposti utumbo!

Kitu cha pili ni kumwagia thanks kila ataye sema lolote kunihusu, hata ukinitukana vipi, sikasiriki, sana sana unakula thanks.

Kitendo cha kutokasirika kwa lolote na kumwaga thanks za kumwaga toka ndani yako, kupitia kanuni ya karma, ya what you give is what you get, then ukitoa furaha, furaha inakurudia.

"Don't worry, be happy, don't mind, don't care, don't give a dam on what they say about you on what you think, say or do, just keep focused on thinking what you think, saying what you believe and doing what you do, as long as you think, say and do the right thing, at the right time and doing it right"

That is me, Pasco wa JF, ni yule yule juzi jana na leo, hata katika majina ya Pascal Mayalla, Paskali or simply P.

P
 
Ningependa nami kuongeza jambo moja;

Tusipende sana kuwa-block ama kuwa-ignore watu. Hiyo ni ishara ya kuwahofu watu hao. Ni udhaifu!
Lazima ukutane na changamoto ili ukue kimawazo/maamuzi n.k, utawakwepa hapa kwa ku wa block, vipi mtaani?

Mimi Mtu tukipishana Nahakikisha tumeyamaliza iwe kwenye Wall au hata PM nitamfuata, ILA TU kama nitagundua mimi ndio chanzo.

Kwa wale wenzangu wa Matusi nawapendaga, pia siwaachi, naendelea kumchokoza kwa kumkera bila Lugha chafu, atukaneeee Baadae atapoa, tunamalizana.

JF ina Pressure kubwa sana, kama kichwa chako ni pata moto, Utakosana na watu kila comment, Na kuna watu wakikujua mpata moto, anakutafuta kabisa akuchokoze na wewe una jaa.

Wewe unateseka kumbe mwenzako anafurahia.
 
Nafikiri kwa yeyote ambaye atakuwa akitumia nguvu kubwa katika kupambana na vidole kwenye keyboard inabidi apimwe DRE ya ubongo kama itakuwepo
 
Mimi kwanza kuna Majukwaa kama la siasa siwezi pita hata kwa bahati mbaya kwa afya ya moyo wangu...

Pia Jukwaa hili la Habari na Hoja mchanganyiko
Mambo mengi Sitaki kuyachukulia serious(kwa Wanaokutana na comments zangu wananijua), maana mengi ni changamsha genge na unakuta hata mwandishi wa uzi kaandikia Bar, unakuta mtu anasifia maisha yake, wewe na wivu wako unaumia unaanza kumuwakia, kumbe maskini wa watu anajifariji.

Kupenda ligi nako mara nyingi Huishia kwenye Ugomvi..

Ila kiukweli kuna watu wanapata moto haraka sana humu, yani mtu kitu kidogo tuu anageuka mbogo, Hawa ndio wale unakuta simu zao zimepasuka vioo kumbe ni ku typ kwa hasira.
Haha haha haha 😂🤣😅 jamaa wana type kwa hasira Hadi wana haribu vioo vya simu zao.

Humu Ndani wengi Wana msongo mkali wa mawazo. Wengi hawana nguvu za kiume, hawana pesa, hawana kazi, wamejuruhiwa, hapa wamekuja kulipa kisasi.

Ndugu yangu, kumbuka hata ukiwa na shida kubwa kiasi gani, hauko peke yako shidani. Wapo wenye shida kubwa kuliko wewe.

Jifunze kuziambia changamoto zako kuwa Mimi ni mkubwa kuliko tatizo linalonikabili. Hali ya kujiona mshindi kabla hujashinda itakusaidia kukuongezea Hali ya kujiamini na hivyo kukuletea furaha.

NB:- Nimeongea na jamii kupitia reply kwenye comment yako
 
How to handle difficult people. Kiligeuza watu wa namna hii kuwa fursa kwangu.
 
Mleta mada jana tu **** thd fulani humu ulimshambulia mleta mada kwa kejeli halafu eti leo unajifanya Malaika unatoa ushauri! Acha unafiki,halafu wewe utakua ni wakala wa huyo mshana au ni mshana mwenyewe kwa ID nyingine,ndio maana hua huchoki kumpigia kiki humu.
Sikumkejeli Wala sikumshambulia, Mimi Niko crack joke, nilisema meli inatoka DSM inaenda Mwanza, jamaa akajaa upepo kuwa naharibu uzi wake, lakini tayari wakati nafanya utani huo, tayari solution ya tatizo lake ilikuwa imeshapatikana na Hadi Mshana Jr alisema angemtafutia namba ya dalali.
 
Acha unafiki,halafu wewe utakua ni wakala wa huyo mshana au ni mshana mwenyewe kwa ID nyingine,ndio maana hua huchoki kumpigia kiki humu.
Mshana Jr is my Master, my Teacher, my Guru and also my RABI, I love him soooo much and I'm learning a lot of things from him.
I'm proud of him and he is role model.

Hamna mtu amefundisha zaidi ya Mshana Jr humu jukwaani.
 
Back
Top Bottom