Nini tufanye kama JK atamteua e lowassa kuwa waziri mkuu?

Kagalala

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
2,403
1,132
Wana JF na watu wote wenye mapenzi mema na Tanzania, naomba mnijulishe ni nini tunaweza kufanya kama week ijayo Rais akimteua mshikaji wake E Lowasa kuwa Waziri Mkuu. Au je katiba ya nchi hairuhusu Waziri Mkuu aliyejiuzuru kwa manufaa ya umma kurudi tena kuwa waziri mkuu?
Kama katiba inaruhusu sitashangaa kusikia jina la Lowasa au Rostam linatoka kama waziri mkuu au Waziri katika wizara ya fedha. CCM hawana haibu............
 
Tutampongeza maana pale alipoishia kwenye shule za kata atazifanye ziwe na hadhi inayofanana na shule nyingine za serikali kama vile Mawenzi Second, Tambaza, Tabora girls, n.k
 
Cha kufanya ni kumshtaki kwa watanzania, ili 2015 wajue watafanya nini, kwa sasa itakuwa imekula kwetu maana EL atarudi kama simba aliyejeruhiwa, mafisadi ndio watabeba kila kitu. Na kwa JK jinsi alivyo zuzu anaweza kweli kufanya hicho kioja. Mungu atuhurumie sana Maskini wa Tanzania.
 
kwa kweli sioni tabu sana kama Kikwete atamteua Lowasa. ingawa Lowasa amamekutwa na kashfa hizo ukichunguza kwa makini utagundua kuwa ni mtu anayeipenda sana nchi yake, ni jassiri na anachapa kazi. Kwa Lowasa naona Ni kitu. Pia naye ameshajifunza kutokana na upepo wa mabadiliko. tuache kuhukumu kwanza maana nasi tutahukumiwa
 
Bora Lowassa Mwizi mchapakazi kuliko mtoto wa mkulima mr Pinda muadilifu lakini muoga si jasiri.Fisadi mchapakazi ni bora kuliko muadilifu mzembe.
 
Yaani Mungu nipe uzima nione hatima ya Lowassa kisiasa kwa miaka kumi from 2015!!!! Anajiandaa sana kwa sasa ila pigo ni kupoteza kiti cha ubunge AR mjini!!
 
Hakuna la kufanya hadi 2015 adhabu ya upuuzi huo itakapotekelezwa kupitia sanduku la kura.JK alinyaka 80% 2005 lakini juzi kati kaondoka na 61% hiyo ni msg tosha.huitaji utafiti wa kina kujua hitimisho la CCM.So kichocheo cha kuwapeleka motuary 2015 ni hapo EL atakapoanza tena kutumbua kwa nafasi ya PM.
 
tutashukuru sana maana wameshamweka spika wao na atafanya juu chini ili tume huru ya bunge iundwe ili kumchunguza JK na familia yake kwa ufujaji wa fedha za umma na kwenda kuprint yale mabango ya uchaguzi huko CANADA yaliyochafua nchi nzima, itamwaibisha sana, itamdhalilisha sana na haitamtendea haki JK na mwisho atajiudhuru. Then Lowassa atafurahi sana maana ameshaweza kummtoa Sitta madarakani, JK atafuata.
 
mimi binafsi nitafurahi kama lowassa, chenge, rostam, na kinana wakiwa mawaziri......halafu nitasubiria 2015 nifurahie watanzania watakavyoipigia kura ccm na kuwapa ushindi wa kishindo.
 
Wana JF na watu wote wenye mapenzi mema na Tanzania, naomba mnijulishe ni nini tunaweza kufanya kama week ijayo Rais akimteua mshikaji wake E Lowasa kuwa Waziri Mkuu. Au je katiba ya nchi hairuhusu Waziri Mkuu aliyejiuzuru kwa manufaa ya umma kurudi tena kuwa waziri mkuu?
Kama katiba inaruhusu sitashangaa kusikia jina la Lowasa au Rostam linatoka kama waziri mkuu au Waziri katika wizara ya fedha. CCM hawana haibu............

Kwa jopo la CCM la sasa, inawezekana 100% Lowasa kuwa Kilanja mkuu. Cha msingi watanzania tunaona na adabu tutawatia.
 
hata akifanya hivyo hakuna dhara lolote kwake. kwasasaivi kikwete anaweza kufanya lolote like, kwasababu anajua kama urais ameshapata na hauhitaji tena, so ni wakati wake yeye kujiexpress na kufanya chochote atakacho.. anaweza kumweka EL kuwa waziri mkuu, na kuwapiga chini kina sitta na kina mwakyembe etc. anaweza kumweka mhindi mmoja kina RA etc nao pia. na huu ni wakati wake wa kuwapa waislam mahakama ya kadhi na mambo yote watakayotaka, kwasababu alikuwa anaogopa akifanya hivyo kabla angekosa urais. kwake yeye cha maana ilikuwa ni huu urais, sasa kama amepata atafanya lolote bila kipingamizi.
 
Kwa JK sitashangaa kuona akimteua EL kuwa waziri mkuu wake. Alishasema hana ubia na mtu kwenye urais.

MFANO:

1. Edward Lowassa - Waziri Mkuu
2. Andrew Chenge - Sheria na Katiba
3. Rostam Aziz - Waziri wa Fedha na Uchumi
Na warembo wengine kibao wa kula nao mjengoni.

Vilevile ni bora hata huyo Lowassa kuwa waziri mkuu kuliko hata Pinda ambaye hata Riz1 akimtisha ananywea. Lowassa anajua kuwa sisi tunajua yeye ni FISADI kwa hiyo anaweza kutusaidia kwa namna moja ama nyingine.

Lakini vilevile JK atakuwa ameturahisishia kupeleka ujumbe kwa watanzania kuwa yeye yupo kwa ajili ya matajiri sio watanzania.
 
Wala sitashangaa EL akiwa PM....kama wameweza kumtoa Sitta watashindwa Pinda....subiri asiyejua maana aambiwi maana...Sisi m imeishiwa na watu wenye vision na hekima....mwisho wao unaonekana
 
Mie nitaomba uraia wa nchi nyingine. Ni afadhali utawaliwe na mkoloni kuliko mafisadi
 
Back
Top Bottom