Nini tofauti ya Posa na Mahari na ni kipi hupewa uzito?

agprogrammer

JF-Expert Member
Dec 7, 2015
468
362
Habari za muda huu wandugu poleni na majukumu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza naomba kujuzwa kuna tofauti gani kati ya posa na mahari na kipi huwa kinaanza na kipi huwa ni kinapewa uzito. Nawasilisha
 
Posa ni kule kwenda kujitambulisha kwa binti kama unataka kuoa

Mahari ni ile mali{pesa/kitu} ambacho muolewaji huitaji na muoaji hutoa kumpa mkewe mtarajiwa, na muda mwingine twaita ni ZAWADI kwa wanawake

Ktk uislam hakuna ndoa bila mahari kwa maana mahari ndio inatoa uhuru wa kuingiliwa

VYOTE VINA UZITO NA VINATEGEMEANA HUWEZI UKAPATA KIMOJA BILA KINGINE
 
Posa is a islamic language and mahari is a christiaty language but

they all means the same thing but different languageeeee

Hii ni kwa mtazamo wako....yaani ni vile unavyojua wewe...

Kwa ufahamu wangu mdogo juu ya hili, nadhani posa ni pale unapo peleka BARUA ikiambatana na kiasi kidogo cha pesa (wanasema ya maji ya kunywa ama USHAWISHI) na MAHALI ni kile kiwango mlicho kubaliana kulipa baada ya POSA kukubaliwa.

Naomba mjadala UENDELEEEEE (in voice of MANGEKIMAMBI)
 
Habari za muda huu wandugu poleni na majukumu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza naomba kujuzwa kuna tofauti gani kati ya posa na mahari na kipi huwa kinaanza na kipi huwa ni kinapewa uzito. Nawasilisha
Posa ni kuonyesha nia
 
Posa ni barua inayoambatana na kiasi fulani cha pesa au sukari kwa nia ya kukaribisha mazungumzo juu ya Upande wa binti na kijana mwenye nia ya Kumuoa. Na posa, hupelekwa na mtu wa tofauti na wala siyo kijana mwenyewe.

Mahari ni kiasi cha fedha, vitu au wanyama ambao mtu hushurutishwa kulipa upande wa familia ya binti kwa nia ya kumuoa binti yao. Mfano, utaambiwa ulete ng'ombe watatu, blanketi, khanga pamoja na Vingine. Hiyo ndiyo mahari yenyewe na huwasilishwa na kijana mwenyewe.

Huo ni kwa uelewa wangu.
 
Posa Ni;
P
O
S
A
Wakati Mahali Ni;
M
A
H
A
R
I.
Yani Moja Inaanza Na P Nyingine Inaanza Na M.
Umeelewa?
 
Nadhani maana halisi ya maneno Haya hutegemeana na utamaduni na Imani ya watu.

Kuna baadhi ya jamii hutafsiriwa Posa ni "Tendo lenye kuonyesha Nia ya DHATI ya kumuoa binti (mwanamke) “. Barua, pesa na dalali (mshenga) hutumika kufikisha ujumbe. Ni vyema kutambua Kuna baadhi ya jamii (hasa za wafugaji) hawana utamaduni huu.

Mahali ni kitu chochote chenye Thamani kitolewacho na upande wa mwanaume kupeleka kwa upande wa mwanamke kwa Lengo la kapewa idhini ya kumwoa binti (mwanamke). Tafsiri hii imeegamia Katika mila na desturi za Mwafrika bila kuingia tamaduni za wageni.
 
Back
Top Bottom