Nini tofauti ya Kiswahili SANIFU na FASAHA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini tofauti ya Kiswahili SANIFU na FASAHA?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Konzogwe, Jan 15, 2010.

 1. K

  Konzogwe JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 441
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Nini tofauti kati ya kiswahili SANIFU na FASAHA.
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Jan 15, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Kuongea/kuandika Kiswahili Fasaha ni ile jinsi unavyo andika au kuongea bila kukosea kutamka herufi mfano: Ukiandika Neno Barua (walaka) hapo umeandika au kutamka kiswahili fasaha, kinyume chake BALUA hili neno si Kiswahili fasaha japokuwa unaweza kueleweka.

  Kiswahili Sanifu ni kiswahili kilichofanyiwa marekebisho kutoka lugha nyingine na kuingizwa kwenye lugha husika... mfano neno... password ni nywila, barua pepe (email) nk.

  Kwa ufupi tunaweza kusema kuwa ufasaha na usanifu ni kiswahili kilicho tungiwa kanuni zinazokubalika kwenye uwanja wa taaluma ya lugha.
   
 3. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  X-PASTER,

  Nisaidie hapo,ipi ndiyo fasaha: waraka au walaka?
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Jan 17, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Ni WARAKA...!
   
 5. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Naona fasaha ni Kiswahili kizuri, lugha ya kupendeza.

  Sanifu inalenga zaidi msamiati wake na na mapatano juu za chaguo la maneno na umbo wa maneno.

  Yaani Kiswahili kimezaliwa kutokana na lahaja mbalimbali kama vile Kimrimba, Kimvita, Kiamu. Hapakuwa na staili ya pamoja. Tangu 1930 kazi ya kusanifisha ilileta lugha sanifu kwenye msingi wa Kiunguja.
  Linganisha [ame]http://sw.wikipedia.org/wiki/Lahaja_za_Kiswahili[/ame]

  Maana thenashara au kuminambili yote ni Kiswahili, katika shairi yote yaweza kuitwa "fasaha" lakini "kumi na mbili" ni sanifu.
   
 6. POWER J

  POWER J Member

  #6
  Sep 14, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  nini tofauti kati ya punde si punde na hivi punde?
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Sep 14, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Punde: Soon, in a little while, presently

  Punde si punde: Inatumika kwa kumaanisha: Baada ya muda mchache (soon, in a moment, Thereafter)

  Punde kwa punde: Kidogo kidogo (little by little, gradually)

  Hivi punde: Muda mchache, (Shortly)

  Mifano:

  • Kiswahili: tulikuwa tunamngoja, na punde akaja.
  • English: we waited for him, and he soon came.
   
 8. A

  Albimany JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  PUNDE ni muda mpufi baada ya tukio au maongezi, (baada ya kumwita PUNDE alitokea)

  PUNDE SI PUNDE,ni muda hule hule hatata tukio halijamalizika au maongezi hayajamalizika alikuja,(wakati tunamzungumza punde si punde alitokea,) ni kaka kusema KUFUMBA BA KUFUMBUA:
   
 9. B

  BANDOMA New Member

  #9
  Nov 25, 2012
  Joined: Nov 14, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  kwa kutumia lahaja nne orodhesha maneno matano kutoka kwa kila lahaja na utoe maana yake kwa kiswahili fasaha .naombeni michango yenu
   
Loading...