Maulaga59
JF-Expert Member
- Feb 1, 2021
- 2,989
- 2,954
Kwa Tanzania
1. Zamani Vyuo kama Mzumbe, DIT, IAA n.k vilkua vikitoa Advance Diploma ambayo duration na content yake ni sawa kabisa na Bachelor Degree, hivyo Advance Diploma ni equvalent to Bachelor Degree na hata kwenye Ajira wanapata stahiki sawa kbs na hata kwenye kujiendeleza wote wanapata fursa sawa kbs
2. Kuna mtu hapo juu ametofautisha kuwa Bachelor inataka credit 400+ na kuiita NTA Level 8 na kusema Advance Diploma inataka credit 300+ na kuiita ni NTA Level 7, nataka nfafanue hapa: NTA Level 8 ndio Bachelor Degree, na Hivyo Mwenye NTA Level 8 ya DIT, na mwenye Advance Diploma ya IAA na mwenye Bachelor Degree ya UDSM hawa wote wako sawa kbs.
3. Najazia ya hapo namba 2, NTA Level 7 sio sawa na Bachelor Degree na hivyo wala sio sawa na Advance Diploma, bali NTA Level 7 inaitwa pia Higher Diloma(Usiichanagnye kbs na Advance Diploma). NTA Level 7 iko chini ya NTA Level 8, hivyo utaona haijafikia kuwa sawa nayo na hivyo sio sawa na Bachelor Degree wala na Advance Diploma
4. Postgraduate Diploma ni Diploma itolewayo kwa mwenye Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree au Advance Diploma), PD inakusaidia kwa mfano, umesoma Shahada ya kitu A na unataka kupata uelewa wa kitu B hivyo badala ya kwenda kukaa tena miaka mitatu upate Shahada ya kwanzsa nyingine unafanya hiyo PD ya kitu B kwa mwaka mmoja, na ukipenda inakua imekupa fursa ya kwenda kufanya Shahada ya pili ya hicho kitu B. Lakini unakuta una shahada ya kwanza ya kitu A, na unataka kufanya shahada ya pili ya kitu hicho hicho A unakuata wanataka uwe na GPA ya kuanzia 2.7 ktk shahada yako ya kwanza, ww kumbe una GPA ya btn 2.0-2.6 hivyo inakupasa sasa ufanye PD ya hicho kitu A then ndo uendelee kufanya shahada ya hicho kitu A. Hopefully hapo iko clear kbs kwa wadau wote!!!!
Uliotoa uzi huu product ya hizi shule za Kata au? Maana sijawahi sikia kitu kinaitwa ‘Advance Diploma’ bali najua kitu kinaitwa ‘Advanced Diploma’. Hata kuna baadhi utasikia wanasema ‘Advance Level’ badala ya ‘Advanced Level’. Ama kweli elimu ya sasa kwa vijana mnaomaliza vyuo nsipa heko kwa kweli! Duuh!