Nini tofauti kati ya Visa na Passport (Hati ya Kusafiria)?

B5nga

Member
Mar 10, 2019
6
3
Naomba kujua tofauti ya Visa na Passport. Pia, ni njia zipi inatakiwa kuzifuata ili upate hati hizo za kusafiria?

Mfano Nataka kwenda Kenya au Marekani!

Asanteni sana.
 
Naomba kujua tofauti ya visa na passport,pia ni njia zipi inatakiwa kuzifuata ili upate hati hizo za kusafiria,Mfano Nataka kwenda Kenya au Marekani! Asanteni sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Andaa passport kwanza
Kuna nchi huhitaji visa kuingia. Ushauri wangu, tafuta passport kwanza ndio uje utuambie unataka kwenda nchi gani tukupe ushauri.
Kila nchi ina mashrti yake ya kukupa visa na nyingine unaingia bila visa cha msingi tu uwe na passport.

Mfano nchi zote za Africa mashariki na SADC unaingia bila visa ila uwe na passport na yellow fever tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Passport:
Hii document ya kusafiria. Hii hutolewa na Nchi husika kwa ajiri ya raia wake wanaotaka kusafiri kwenda nchi nyingini. Simply passport ni kitambulisho cha uraia.

VISA:
Hiki ni kibali cha kuishi. Ukitaka kwenda nchi yoyote kwa shughuli yoyote lazima uwe na kibali cha kuishi huko.

Visa hutofautiana kwa shughuli inayokupeleka nchi husika.

Mfano Kuna visa ya matibabu, Masomo, Holyday, biashara, kazi na nyingine.

Mfano ukitaka kwenda India kutibiwa lazima upate Visa ya matibabu. Utakaa huko hadi utakapomaliza matibabu na visa nayo itakwisha muda wake.

Vrou van samaria give me bit of water to drink
 
Passport inatolewa na nchi YAKO Visa inatolewa na ubalozi wa nchi unayokwenda uliopo nchini kwako, Visa huwa inabandikwa ndani ya passport ,kutegemea na mahusiano na makubaliano Ya nchi yako na huko unakotaka kwenda waweza kutakiwa kuomba Visa ama ukaenda bila VISA mfano nchi zote wanachama wa SADC, hauhitaji VISA kuingia kutokea Tanzania, unagongewa muhuri kwenye passport yako on arrival na unapotoka.
 
Viza ni kibali cha kukaa nchi husika kwa muda tajwa, passport ni pass ya kusafiria tu,

Viza inakuwa katika mfano wa karatasi au kurasa iliyochomwa au kubandikwa ndani ya passport ya kusafiria,

Passport ni kitabu cha kusafiria ambacho Viza zote ubandikwa ndani yake,

Passport inatumika kusafirisa nchi zote ulimwenguni ambazo ukitaka kwenda unaomba visa kwenye balozi zake

Ila Viza ni ya muda mfupi na utumika uendea nchi moja tu uliyoomba, japo kuna baadhi ya visa zinaruhusu kutembelea hata nchi majirani, mfano Schengen Visa, za ulaya,

Passport utolewa na uhamiaji wa nchi ambayo raia wa muombaji wake anatoka

Lakin Visa utolewa na ubalozi wa nchi ambako muombaji anataka kutembelea
 
Niliposoma tu comment ya Jamaa jinsi alivyojibu nikajua tu huu Uzi hauna mwisho mwema!
Mmenichekesha sana aisee
Turekebishane wazoefu wa jamiiforums, kuna kosa lolote au kuna watu maalum wa kuchangia humu???!!!
 
Turekebishane wazoefu wa jamiiforums, kuna kosa lolote au kuna watu maalum wa kuchangia humu???!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli hakuna Watu maalum wa kuchangia humu!

Kosa lipo?
Ndio ukisoma ulichouliza na alichojibu yeye ni tofauti!
Na amejibiwa hivyo Na hao wadau kwasababu ameonyesha ni jinsi gani hayupo makini!
 
Hakuna kosa mkuu, sema tu ulichojibu ni tofauti kabisa na swali la mleta mada. Inaonesha ni kama ulikurupuka hivi ndio maana mdau hapo akakutolea uvivu

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa, siku nyingine sitakurupuka. Ila huyo mdau anaonekana kama hamnazo dizaini fulani, unaanzaje kumtukana mtu usiyemjua badala ya kumrekebisha?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Passport:
Hii document ya kusafiria. Hii hutolewa na Nchi husika kwa ajiri ya raia wake wanaotaka kusafiri kwenda nchi nyingini. Simply passport ni kitambulisho cha uraia

VISA:
Hiki ni kibali cha kuishi. Ukitaka kwenda nchi yoyote kwa shughuli yoyotte lazima uwe na kibali cha kuishi huko.

Visa hutofautiana na shughuli inayokupeleke nchi husika.

Mf. Kuna visa ya matibabu, Masomo, Holyday, biashara, kazi na nyingine.

Mf. Ukitaka kwenda india kutibiwa lazima upate Visa ya Matibabu. Utakaa huko hadi utakapo maliza matibabu na visa nayo itakwisha muda wake

Vrou van samaria give me bit of water to drink
Kwanza umeshampoteza mwenzako.
Viza ni ruhusa inayo kuwezesha kuingia nchi nyengina na kutoka bila kuishi, kwa mfano unakwenda kwa matembezi au kwa biashara.
Kama hio nchi unayokwenda unataka kuishi na kufanya kazi, unahitaji uombe redisent Permit. Sasa hio Resident Permit yako kutokana na lengo lako uliloombea ndio itaaamua kua unaweza kufanya kazi au la?
Ndio maana Watalii wanaokuja tanzania hawaruhusiwi kufanya kazi, ili waruhusiwe kufanya kazi inabidi waombe Resident Permit na wakati huo huo waomba Work permit
 
Simple and clear answer:-

PASSPORT: Identifies WHO YOU ARE - your name, sex, citizenship, birth date. Swali "wewe ni nani"? linajibiwa na passport katika nchi ya kigeni. Hutolewa na nchi yako.

VISA: Inajibu swali "una ruhusa ya kuingia nchi hii"? Lini, kwa muda na sababu gani. Hutolewa na nchi unayotaka kwenda ama on arrival at the airport au kupitia balozi zao. Visa-free manake huhitaji visa kuingia ila PASSPORT is a MUST.

As simple as that.

Anyway, usi-confuse na PASSPORT na VISA ya Mbinguni ambayo ni DAMU YA YESU peke yake ndiyo chapa na utambulisho wa kupaona patakatifu Mbinguni. Kwa bahati mbaya option ya "ON ARRIVAL" haipo. Tafuta sasa jina lako kuandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo. mitale na midimu
 
Naomba kujua tofauti ya visa na passport. Pia ni njia zipi inatakiwa kuzifuata ili upate hati hizo za kusafiria?

Mfano Nataka kwenda Kenya au Marekani! Asanteni sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Thread kama hizi zinanifanya nitambue kuwajibu baadhi ya wana JF wanaokandia nikiweka thread juu ya mtakabali wa nchi ni kupoteza muda wangu!
 
Passport:
Hii document ya kusafiria. Hii hutolewa na Nchi husika kwa ajiri ya raia wake wanaotaka kusafiri kwenda nchi nyingini. Simply passport ni kitambulisho cha uraia

VISA:
Hiki ni kibali cha kuishi. Ukitaka kwenda nchi yoyote kwa shughuli yoyotte lazima uwe na kibali cha kuishi huko.

Visa hutofautiana na shughuli inayokupeleke nchi husika.

Mf. Kuna visa ya matibabu, Masomo, Holyday, biashara, kazi na nyingine.

Mf. Ukitaka kwenda india kutibiwa lazima upate Visa ya Matibabu. Utakaa huko hadi utakapo maliza matibabu na visa nayo itakwisha muda wake

Vrou van samaria give me bit of water to drink
 
Passport:
Hii document ya kusafiria. Hii hutolewa na Nchi husika kwa ajiri ya raia wake wanaotaka kusafiri kwenda nchi nyingini. Simply passport ni kitambulisho cha uraia

VISA:
Hiki ni kibali cha kuishi. Ukitaka kwenda nchi yoyote kwa shughuli yoyotte lazima uwe na kibali cha kuishi huko.

Visa hutofautiana na shughuli inayokupeleke nchi husika.

Mf. Kuna visa ya matibabu, Masomo, Holyday, biashara, kazi na nyingine.

Mf. Ukitaka kwenda india kutibiwa lazima upate Visa ya Matibabu. Utakaa huko hadi utakapo maliza matibabu na visa nayo itakwisha muda wake

Vrou van samaria give me bit of water to drink

Natumae mleta mada utakua umepata muongozo...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom