Nini tofauti kati ya rushwa na takrima!

mstahiki

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
308
5
Waheshimiwa wana JF,ningependa kujua Nini tofauti kati ya rushwa na takrima!Je inafaa?Je inamsaidia vipi mwananchi wa kawaida?Je inalisaidia vipi Taifa?Ni kwanini iliwekwa?Je tunahitaji kuendelea kuwa nayo?
 
Zote ni aina ya rushwa, Takrima waliita CCM na kutungiwa sheria katika uchaguzi wa mwaka 1995-2005 na pia rushwa hutolewa kila sehemu, Labda swali waulizwe CCM ndio wanaweza kuwa na majibu mazuri sana
 
Hakuna tofauti zote ni rushwa. CCM walianzisha takrima iwasaidie kuingia madarakani kiulaini kwa sababu waliona hawana jipya kwa watanzania. So takrima ni rushwa ya uchaguzi na ina maslahi kwa CCM haina maslai ya wananchi wa kawaida.
 
Waheshimiwa wana JF,ningependa kujua Nini tofauti kati ya rushwa na takrima!Je inafaa?Je inamsaidia vipi mwananchi wa kawaida?Je inalisaidia vipi Taifa?Ni kwanini iliwekwa?Je tunahitaji kuendelea kuwa nayo?

tofauti ipo tena kubwa sana...........................
rushwa hutolewa kwa nia ya kushawishi mpokeaji afanye kitu fulani kwa mtoaji amabcho ni haki ya mtoaji na alipaswa kupewa bila kulazimika utoa hiyo rushwa

takrima (ukarimu) ni kutoa kitu kwa mtu kwa hiyari bila kutegemea kulipwa chochote. mfano umemtembelea ndugu yako akakupa malazi na asikudai malipo yoyote. au hata unapotoa ofa ya bia mija kwa rafiki yak mliyekutana naye pub ni takrima hiyo. mzizi wa takrima ukokatika mila na desturi za kiafrika.........

japo, vyotevina nguvu ya ushawishi, lakini bado ni vitu tofauti sana............................
 
Tofauti ipo kati ya takrima na rushwa ila kinachofanya ziwe sawa nimtizamo wa wahusika kwa mfano mtu umejitoa utoe takrima kidog yaan ofa mwingine anaweka mtizamo wake kuwa umemhonga yani rushwa kumbe huna maana hio hapo ndio tatizo kwao kunatofauti sana pale
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom