Nini tofauti kati ya Nyati na Mbogo?

Mbogo ni Nyati aliyejeruhiwa.

Kwa kawaida nyati akijeruhiwa na mnyama mwingine hasa Simba, hubadilika tabia yake ya upole na kuwa mkali na mwenye hasira kiasi cha kujitenga na nyati wenzake.

Akiwa kwenye hali/ tabia hii tunamuita "mbogo" badala ya "nyati".
 
Nyati ni jina la huyo mnyama na mbogo ni jina la tabia yake ya ukali.

Ndiyo maana neno mbogo pia hutumika kama sifa ya ukali wa baadhi ya watu, utasikia ikisemwa mtu fulani kawa mbogo baada ya kufanyiwa jambo asilolipenda.
Sio kweli. Nyati ni jina la jumla la huyo mnyama, mbogo ni nyati aliyetengwa kwenye kundi lao hasa hasa huwa ni dume. Hii hutokea pale dume anapozeeka au kuwa na maradhi hivyo kupigwa na madume mengine ili kuongoza kundi. Akisha tolewa kwenye kundi uishi peke yake na huwa ni mkali kwelikweli.
 
Ndio tabia ya lugha mkuu, kitu kimoja kinaweza kuwa na msamiati zaidi ya mmoja, TEMBO /NDOVU, MOYO / MTIMA, AFYA / SIHA , FAMILIA / AILA...hayo mengine najua vijana wenzangu mtayauliza kama ni Kiswahili , ila ukikaa na mababu unajua mengi.
Na mara nyingi ukichunguza vizuri utakuta kuna uwezekano mkubwa kuwa neno mojawapo kati ya hayo limekopwa na mojawapo ndiyo la kiasili.

Mbogo ni jina la huyo mnyama katika lugha za Kibantu. Katika Kisukuma, kwa mfano, nyati tunamuita mbogo. Yawezekana ikawa ni neno hili hili au linalofanana na hili katika lugha nyingine za Kibantu. Sina uhakika lakini sitashangaa kama nyati ni jina la mkopo kutoka Kiarabu huko au lugha zingine nje ya Kibantu

Na kwa maoni yangu hakuna tofauti kati ya mbogo na nyati. Ni utofauti tu wa asili yake hayo maneno.
 
Kiswahili ni lingua franca.

Lingua Franca - Lugha iliyojitokeza kuwezesha mawasiliano na muingiliano baina ya watu wa jamii tofauti ambao lugha zao pia zimetofautiana.

Hivyo maneno ya mwanzo ya Kiswahili yamekopwa kutoka lugha mbalimbali za Kibantu, Kiarabu, Kijerumani etc. ili kuwezesha huo muingiliano katika Pwani ya Afrika Mashariki.

Kiswahili (Sanifu) - hata kabla hakijawa Lingua Franca kamili kimetokana na lafudhi ya Kiunguja iliyochaguliwa na Waingereza kusanifishwa. Unataka kusema kuwa hiyo lafudhi ya Kiunguja haikuwa na maneno yake ya asili kabla ya ujio wa Waarabu, Wareno, Wajerumani na Waingereza? Ina maana msamiati wote wa Kiswahili ni wa mkopo na chenyewe hakikuwa na maneno yake ya asili? Kiliwezaje kuwa lugha kama hakikuwa na maneno yake kabla hakijakopa?

Unapokopa hukopi maneno ya asili. Unakopa maneno mapya ili kuelezea dhana mpya ambazo huna maneno yake katika lugha yako ili kukidhi maingiliano yako na jamii-lugha mpya katika nyanja mbalimbali (dini, biashara, utawala, elimu n.k).

Au kuna mahali hatuelewani? Mbona jambo tunalojadili liko wazi na halihitaji hata mjadala? Na ndiyo mara ya kwanza nasikia kuhusu lugha ambayo haina maneno yake ya kiasili (native lexicon) labda kama tunazungumzia pidgin au lugha za mseto-changamano.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom