Nini tofauti kati ya maneno pesa na hela

Nijuavyo mimi; hela, pesa na fedha ni maneno tofauti yenye maana moja (synonyms).

• Pesa ni neno lililotoholewa kutoka katika Lugha ya Kihindi (Paisa).

• Hela ni neno lililotoholewa kutoka katika Lugha ya Kijerumani (Heller).

• Fedha ni neno lililotoholewa kutoka katika Lugha ya Kilatini.

Yote yana maana moja.
The Most correct answer.
 
Hapo umegeuzia mkuu
"Ndio" ilitakiwa iwe kwenye sentensi ya kwanza
Na" ndiyo" kwenye sentensi ya pili

"Ndio "hutumika kuelezea kitu
Yaani hapo ilitakiwa useme"hiyo ndio nyumba yangu"

Sentensi ya pili alama ya" ndiyo "yaani kukubali
Ungeandika "weka alama ya ndiyo kwa mgombea wetu"

Sent using Jamii Forums mobile app
Mama mchungaji kwa kiswahili uko vizuri
 
Pesa ni kiwango cha hela chini ya 100,000
Hela ni kiwango cha pesa zaidi ya 100,000
 
Nijuavyo mimi; hela, pesa na fedha ni maneno tofauti yenye maana moja (synonyms).

• Pesa ni neno lililotoholewa kutoka katika Lugha ya Kihindi (Paisa).

• Hela ni neno lililotoholewa kutoka katika Lugha ya Kijerumani (Heller).

• Fedha ni neno lililotoholewa kutoka katika Lugha ya Kilatini.

Yote yana maana moja.

Waziri wa hela
Waziri wa pesa
Waziri wa fedha

Hivyo, sio?
 
sarafu (currency) ya wakoloni wa kijerumani iliitwa heller, hivyo kwakuwa tuliitumia jina limebaki tunaendelea kulitumia kumaanisha fedha, pesa inatokana na wareno, nadhani wao fedha yao inaitwa peso, sisi tukaita pesa, kumbuka kuwa mreno aliwahi tawala pwani ya nchi yetu kabla ya waarabu wa omani kukita mizizi ya usultani wao pwani ya afrika mashariki.

kwa hiyo heller na pesa ni majina ya aina za currency zilizokuwa zikitumia na hao wageni walipokuja kutawala ila sisi tunatumia tu kuwa ni mbadala wa neno fedha

ni kama mtu akiamua kutumia neno rupia kumaanisha fedha (mfano: utasikia, penye udhia penyeza rupia, hapa rupia inamaanisha fedha , ila kihistoria ni fedha iliyoletwa na wakoloni wa kijerumani pia sultani wa zanzibar alileta rupia ya zanzibar.
 
Back
Top Bottom