Nini tofauti kati ya Annual na unpaid leave?!

costa

Member
Feb 1, 2010
7
1
Wadau,kwa mujibu wa sheria za kazi za Tz,nini tofauti ya annual leave na unpaid leave?Na je vyote ni sawa?Au je,mwajiri anaweza ku'define' anavyojua yeye au tuseme kutumia maneno haya interchangeably?Je,mtu akiwa ktk annual leave hastahili kupewa mshahara,hadi akimaliza hiyo leave??
 
Annual leave kwa kifupi ni likizo, hii inabidi ulipwe. Na kuna kiasi fulani cha likizo mwajiri inabidi atoe kuendana na sheria zaidi ya hapo ni makubaliano.

Unpaid leave ni likizo bila malipo, hii inaweza kutokea kama mwajiriwa anataka likizo zaidi ya ile anayopata kisheria na katika makubaliano au kama mwajiriwa amesimamishwa kazi kutokana na makosa fulani na uchunguzi unafanyika.
 
Kwa kuangalia sheria fasta fast kisheria unatakiwa upate siku 28 za likizo kwa mwaka na unatakiwa ulipwe kwa siku hizo kwa rate ya kawaida.

Pia una siku 126 za sick leave kama unaumwa na kwa hizo unalipwa full kwa siku 63 za kwanza, then nusu kwa siku 63 za mwisho.

Pia kuna siku 84 za maternity leave. Au siku 100 kama ni mapacha zu zaidi.

Siku 84 zengine mtoto akifariki ndani ya mwaka mmoja.

Sioni kitu chochote kuhusu unpaid leave kwenye EMPLOYMENT AND LABOUR RELATIONS ACT, 2004 labda iko covered na sheria nyingine.
 
...Sioni kitu chochote kuhusu unpaid leave kwenye EMPLOYMENT AND LABOUR RELATIONS ACT, 2004 labda iko covered na sheria nyingine.
Kama kwenye sheria "sioni kitu chochote" hayo maelezo ya unpaid leave umetubandikia kutoka wapi, google?

Unpaid leave ni likizo bila malipo, hii inaweza kutokea kama mwajiriwa anataka likizo zaidi ya ile anayopata kisheria na katika makubaliano au kama mwajiriwa amesimamishwa kazi kutokana na makosa fulani na uchunguzi unafanyika.

Kama kwenye sheria "sioni kitu chochote" hayo maelezo ya unpaid leave umetubandikia kutoka wapi, google?

Hiyo ndo definition ya unpaid leave, ila application (details) zinatofautiana na sheria za mahali ulipo so ni kupekua sheria mpaka uipate.
 
Hiyo ndo definition ya unpaid leave, ila application (details) zinatofautiana na sheria za mahali ulipo so ni kupekua sheria mpaka uipate.
Definition kutoka wapi? Mada ni: "Wadau,kwa mujibu wa sheria za kazi za Tz,nini tofauti ya annual leave na unpaid leave." Sio definition za google au kamusi au maoni au popote ulipoipata. Ni kuhusu sheria ya Tanzania.
 
Nashukuru sana,kwa kuanzia nadhani nimeridhishwa na mjadala!It's relly a plus!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom