Nini thamani ya kura ya mtanzania, na je anaijua?


Mabel

Mabel

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2010
Messages
1,029
Likes
35
Points
145
Mabel

Mabel

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2010
1,029 35 145
Katika mchakato wa uchaguzi mkuu uliopita na hata baada ya matokeo kutangazwa na wale ‘walioitwa' washindi kutangazwa katika nafasi ya Urais, Wabunge na Madiwani, kuna mambo mengi yalijitokeza, yanajitokeza na yataendelea kujitokeza kwa siku zijazo. Moja wapo ya matatizo/mambo yaliyojitokeza katika uchaguzi wa mwaka huu ni uchakajuaji wa matokea wa hali ya juu.

Uchakajuaji wa mwaka huu ulikuwa HURU na WAZI kwa walioufanya. Nasema ulikuwa HURU na WAZI kwani ulifanyika kwa uwazi wa kutosha na kwa uhuru zaidi na hata watoto wadogo wanalijua hili, anayebisha juu ya hili sina la kumwambia kwani itakuwa sawa sawa na kufanya kazi ya kukumbatia Mbuyu . Katika hili kuna watu wamepaza sauti zao hadharani wakilaani, kukemea hali hiyo na hata kudai katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na pia wakitaka uchunguzi ufanyike juu ya mchakato mzima wa uchaguzi wa mwaka huu, ili kuondoa matatizo kama haya siku za usoni.

Kinachonishangaza ni wengi wa wapiga kura wenyewe kutoshitushwa na SERA nzima ya uchakachuaji ya chama cha Mapinduzi ambayo inashika hatamu kila chaguzi zinavyoendelea, na hata wengine wanadiliki kuwabeza wale wanaokemea suala hili kwa nguvu zote.

Wasiwasi wangu mimi ni kweli watanzania tunajua maana ya kura zetu na kupiga kura? Umuhimu wake kwetu binafsi na taifa letu kwa ujumla na mstakabali wa kizaji kijacho? Na je, ni nini hatima yetu kama hatutaweza kusimama kama watanzania kwa pamoja kupinga swala hili? Je wale wachache wanaopiga kelele, kweli wataweza kulikomboa taifa letu bila kuwasaidia? Na itachukua mda gani kufika huko? Na je, nini kifanyike ili kila mtanzania ajue thamani ya kura yake anayopiga? Au watanzania tukae kimya tusubili huruma ya watawala wetu? Na je, lini itakuja huruma hiyo?

Mwisho, nawapa moyo wale wote wenye nia thabiti ya kulikomboa taifa hili kutokufa moyo na kuendelea na jitihada zao za kikombozi kwa nguvu zao zote, akili yao yote, uelewa wao, juhudi na utashi wao usio na kikomo na kila mmoja kwa nafasi yake kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kweli. Maana si wakenya wala waganda watatuletea maendelea kupitia jumuia ya Africa Mashariki, wala misaada ya vyandarua vya mbu na vitu vingine kama hivyo kutoka kwa wahisani vitatujengea heshima ndani na nje ya nchi, bali ni sisi kama watanzania kusimama kidete katika kulijenga taifa letu bila kumuonea aibu mtu yeyote anayekuwa kikwazo.


Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki wapiganaji.
 
M

Mopalmo

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Messages
510
Likes
38
Points
45
M

Mopalmo

JF-Expert Member
Joined Nov 11, 2010
510 38 45
Haina thamani kwa kua haiheshimiwi na watawala,vinginevyo tutafute njia mbadala ya kuipa thamani, katiba mpya ni jibu pekee
 

Forum statistics

Threads 1,235,453
Members 474,585
Posts 29,222,574