Nini tatizo la Taifa Stars kushindwa kila mechi?

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
NINI TATIZO LA TAIFA STARS KUSHINDWA KILA MECHI!?

Leo 12:30hrs 24/01/2021

Nakubaliana na kila Mtanzania kwa 100% na ukizingatia nchi kama Zambia,Namibia,Guinea, Zimbabwe,Rwanda,Burundi,Kenya,Uganda na Burkina Faso tupo sawa tu kiuchumi tena tunaweza kuwa tumewazidi idadi ya watu ikiwa wao wapo Milioni kumi hadi ishirini na Sisi Watanzania tupo watu Milioni 60,sasa tunashindwa nini kupata wachezaji wazuri na kuwaleta makocha wazuri tupate Timu ya Taifa itayotoa Upinzani wa kweli kwa Afrika nzima!? Niulize swali hivi wale vijana wa copa cocacola ya kwanza wameishia wapi? Si walichukua world cup ya vijana wa copa cocacola brazil?Naomba kwanza kudeclare interest,kutangaza maslahi yangu,

Mimi ni shabiki wa "Reli Kiboko ya Vigogo" timu iliyokuwa ikidhaminiwa na Mzee wangu Mh Oscar Mloka na Adolph Ghikhas kutoka mtaa wa Kichangani na Wazee wengine wa Morogoro baada ya Udhamini wa shirika la Reli kukoma,nakiri sijawahi kuwa shabiki wa timu nyingine yoyote zaidi ya Reli kiboko ya Vigogo,japo niliwahi kuwashabikia akina Edibily Lunyamila, Mohamed Hussein.

"Mmachinga" Salvatory Edward lakini bado moyoni niliendelea kuikumbuka "Reli kiboko ya Vigogo", Wazee wa Morogoro waliisupport Reli Kiboko ya vigogo iliyokuwa na Shabiki maarufu "Yamungu" kutoka na historia ya mpira wa Morogoro hasa baada ya timu ya Mseto iliyoanzishwa Mwaka 1965 kuchukua ubingwa wa Tanzania Mwaka 1975 kwa mara ya kwanza ikivunja utamaduni wa timu ya Simba na Yanga kuchukua ubingwa mara tuu baada ya ligi kuanzishwa Mwaka 1965,

Vijana wengi wa sasa kama kina Erick Patrick,Silas Msuya,Benjamin Masumo,Moris John, Sylvester John,Gand Dizo,General Kabaro,Herry Bringbring,Chiko Junior na Leo Afrikanus mlikuwa hamjazaliwa naamini hamumjui hata Mohamed Mwameja,Kikosi hiki cha Reli kiboko ya Vigogo Miaka ya tisini,golini alikuwa anasimama Athuman Msomali,beki wa kulia Mohamed Mtono,beki wa kushoto mara nyingi alikuwa Abdallah Mkali,beki namba nne alikuwa Ramadhani Kilambo,Sentahafu alikuwa Gasper Lupindo,namba 6 alicheza Christopher Michael,Winga namba 7 ni Nassib Abbas namba nane alikipiga Yusuph Macho pamoja na Boniphace Njohole, straika wa kati alikipiga Duncan Butinini,namba kumi David Mihambo,bila kuwasahau Habib Kondo,Wema Juma "Fashanu", Mathias Mulumba,Ramadhani Kilambo, Abdallah Suleiman ‘Kaburu’ na kipa Sahau Said Kambi.

Winga ya kushoto Mbuyi Yondani na Peter Mjata,Kikosi hiki chini ya Kocha John Simkoko kilikuwa kinampiga 3-0 au 2-0 Yanga na Simba kila kinapokutana,kilikuwa kikosi hatari mno hasa kinapokutana na Simba au Yanga,ilifika kipindi Simba au Yanga wakija Morogoro walibadili njia badala ya kupita darajani Shan Cinema walikuwa wanazunguka hadi Lutheran Junior Seminari kukwepa kupita Mto wa Morogoro ambao waliamini kila wakivuka daraja la Mto Morogoro basi walikula 3-0 katika dimba la Jamhuri Mkoani Morogoro,Simba na Yanga walianza kuamini uchawi toka zamani sana,na ndio maana Taifa Stars inayoundwa na Simba na Yanga inashindwa,maana hakuna mpira wa kuchezwa bila uchawi.

-Simba na Yanga na Jiji la Dar es Salaam, kamwe halitatia Taifa Stats imara.

Vikosi zaidi ya Simba na Yanga vilivyotikisa soka la Tanzania ni Mseto Fc na Pamba FC au Tout Poisssant Lindanda,Tangu mwaka 1965 ilipoanza Ligi ya soka ya Taifa Tanzania, ubingwa umekuwa wa timu za Dar es Salaam kutokana na timu za mkoa huo kuutwaa kila mwaka. Hii ni kutokana na uwezo wa kimchezo wa timu hizo, hususan Simba na Yanga,Lakini ubingwa wa Muungano, ligi ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 1982 ikizihusisha timu mbili zilizoshiriki Ligi ya Bara na mbili kutoka Ligi ya Zanzibar, umewahi kutwaliwa na klabu za nje ya mkoa wa Dar es Salaam mara tisa katika miaka ya 1984, 1985, 1986, 1988, 1989, 1990, 1992, 1998 na 1999,

Ubingwa wa Tanzania Bara umetwaliwa nje ya Dar es Salaam mara tano katika miaka ya 1975, 1986, 1988, 1999 na 2000 tangu ligi hiyo ianze mwaka 1965.

Mseto FC ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kuupeleka ubingwa wa taifa nje ya Dar es Salaam mwaka 1975 ikifuatiwa na Tukuyu Stars mwaka 1986, Coastal Union ya Tanga 1988, na Mtibwa Sugar ya Morogoro 1999 na 2000.Katika kipindi hicho Mseto ilikuwa na wachezaji wazuri kama Said Gedegela, Charles Boniface Mkwasa, Hamadan, Vincent Mkude, Ramadhan Matola,

Wengine ni Aluu Ally, Shiwa Lyambiko, Hassan Shilingi, Omar Hussein, Spencer na Jumanne Hassan ‘Masimenti’ waliocheza fainali. Mwingine alikuwa Miraji Salum ambaye alikuwa na timu ya taifa, Taifa Stars,Enzi hizo Mseto ilikuwa chini ya kocha Mohammed Hussein Hassan ‘Msomali’ na baadaye ikaongezewa nguvu na kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Bernard ‘bernt’ Trauttmann ilipokuwa ikijiandaa kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kimataifa.Hiki ni kikosi cha Mseto FC ya Morogoro mwaka 1990, wakati huo inashiriki Ligi Daraja la Pili, ambayo sasa ni Daraja la Kwanza. Mseto imewahi kuwa bingwa wa Tanzania mwaka 1975.

Sasa hivi timu hii haipo kabisa katika ramani ya soka nchini. Timu nyingine maarufu mkoani Morogoro kama Tumbaku na Reli, ambazo pia ziliibua vipaji vya nyota wengine wengi nchini enzi hizo, nazo pia zimepotea katika ramani ya soka.Bila kusahau kikosi cha dhahabu,Kikosi cha Pamba au Tout Poissant Lindanda"Tupwisa Lindanda"Kipa namba moja Madata Lubigisa, Rajabu Msoma , Beya Simba, Nteze John, Kitwana Selemani, Fumo Felician, Paschal Mayala na kipa Paul Rwechungura,George Gole, Khalfan Ngasa, Ali Bushiri, David Mwkalebela, Maonwa Mkami, Alphonce Modesti, Juma Amiri Maftah na Nico Bambaga.

-Historia ya Taifa Stars.

Itakumbukwa Agosti 26,1979 Taifa Stars ilikuwa ikihitaji sare ya aina yoyote dhidi ya Zambia ili ifuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu ilipoanza kushiriki mwaka 1968.Taifa Stars ilikuwa ikicheza mechi hiyo ya marudiano dhidi ya Zambia kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika za mwaka 1980 zilizofanyika Lagos, Nigeria.Katika mechi ya kwanza iliyozikutanisha timu hizo, Taifa Stars iliilaza Zambia bao 1-0 ambalo lilifungwa na kiungo, Mohammed Rishard Adolph.Mechi ya marudiano ilichezwa mjini Ndola, nje kidogo ya jiji la Lusaka na timu ya Zambia ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao mwanzoni mwa mchezo,

Lakini Taifa Stars ilisawazisha bao hilo mfungaji akiwa Peter Tino.Bao hilo la Tino lilinyamazisha umati wa mashabiki wa Zambia waliokuwapo uwanjani kwani liliiwezesha Taifa Stars kufuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika 1980.Fainali za LagosBaada ya kufuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika 1980, katika fainali hizo, Taifa Stars ilichapwa mabao 3-1 na wenyeji Nigeria katika mechi ya ufunguzi, ilitoka sare ya mabao 2-2 na Ivory Coast kabla ya kuchapwa mabao 2-1 na Misri na kutolewa hatua ya makundi.Kwa miaka 35 sasa, Taifa Stars imekuwa ikisaka nafasi kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika, lakini imeshindwa kuwika.

Fainali za CHANMwaka 2009, Taifa Stars ikiwa chini ya kocha Marcio Maximo kutoka Brazil ilifuzu kushiriki Fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya Afrika (CHAN) baada ya kuichapa Kenya 2-1 na katika mechi ya marudiano iliichapa tena 1-0. Mechi iliyofuata Taifa Stars ilicheza dhidi ya Uganda na kushinda 2-0 na ziliporudiana zilitoka sare 1-1. Mechi ya mwisho Stars iliichapa Sudan 3-1 na ziliporudiana iliibuka na ushindi wa 2-1 na hivyo kufuzu fainali za CHAN.

Hata hivyo, katika fainali hizo za CHAN, Taifa Stars ilifungwa na Senegal 1-0, ikaishinda Ivory Coast 1-0 na ilitoka sare ya 1-1 na Zambia hivyo kutolewa katika hatua ya makundi.

@Makocha wa Taifa Stars#

-Kocha Marcio Maximo 2006-2010

Taifa Stars imekuwa ikinolewa na makocha mbalimbali wa kigeni na wazawa,Mwaka 2006 ilinolewa na kocha Marcio Maximo kutoka Brazil ambaye aliiwezesha Stars kushiriki CHAN 2009,Kingine alichofanikiwa kocha huyu ni kurudisha ari,moyo na uzalendo kwa wachezaji,pia Watanzania nao walirudisha moyo wa kuipenda Taifa Stars, walinunua fulana za kuiunga mkono,walifurika uwanjani kuishangilia, tulifungwa,lakini tuliridhika na msingi wa soka ulianza kujengeka chini ya Maximo.Kocha Marcio Maximo aliiongoza Taifa Stars kuanzia 2006 mpaka 2010 na katika kipindi hicho, Taifa Stars ilicheza mechi 43, kati ya hizo Taifa Stars ilishinda mechi 16, sare 15 na ilifungwa mechi 12,Pia Maximo alifanya mapinduzi ya aina yake baada ya kuipandisha Tanzania kwenye viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kutoka nafasi ya 167 mpaka nafasi ya 108.

-Kocha Jan Poulsen 2010-2012

Kati ya mwaka 2010 mpaka 2012, Taifa Stars ikawa inanolewa na kocha Jan Poulsen raia wa Denmark. Kocha huyu alipokuja alikuta Watanzania wamehamasika kuipenda timu yao ya taifa na yeye akaona lipo tatizo ambalo Watanzania wanalifungia macho, tatizo la kuendeleza mchezo wa soka nchini.Kocha Jan Poulsen akasema,”Watanzania ndiyo wenye jukumu la kuendeleza mchezo wa soka nchini hivyo wanatakiwa kutafuta mfumo thabiti utakaosaidia kufanikisha suala hilo na kuacha mtazamo wa kuangalia timu ya Taifa tu.”Wakati wa kocha Jan Poulsen, Taifa Stars ilicheza mechi 22, kati ya mechi hizo, Taifa Stars ilishinda mechi 5, ikatoka sare 7 na ilifungwa mechi 10. Pia aliiongoza Kilimanjaro Stars ya Tanzania Bara kutwaa Kombe la Chalenji kwa mara ya kwanza baada ya miaka 16, alipoifunga Ivory Coast kwenye fainali iliyofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

-Kocha Jan Poulsen atoa maono ya kujenga Academy ya soka kuanzia watoto hadi Vijana,

Kocha Jan Poulsen alisema anafahamu suala kuchagua timu ya Taifa ni gumu kutokana na ukubwa wa nchi, kwani rasilimali za kiuchumi zilizopo zinashindwa kusaidia mchezo wa soka, lakini alisema tunavyozidi kuchelewa kuusaidia mchezo wa soka ndiyo tunavyozidi kurudi nyuma katika mchezo huo,Kocha Poulsen alisema wachezaji wa Kitanzania anaowachagua Taifa Stars na wanaoendelea kuchaguliwa wanatokana na mfumo ambao Watanzania wameutengeneza ambao haujali soka la vijana.

Poulsen alisema wachezaji wa Tanzania wanakosa kufundishwa mambo mengi katika ngazi za chini kwa sababu anaona mambo mengi aliyokuwa anawafundisha wachezaji kwenye timu ya taifa walitakiwa wafundishwe wakiwa watoto au vijana.

Katika kipindi hiki ndiyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likamleta kocha Kim Poulsen kutoka Denmark, ambaye akawa anazinoa timu za taifa za vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) na miaka 20 (Ngorongoro Heroes),Jan Poulsen alikuwa na mipango mizuri, lakini ilionekana kushindikana kutokana na uharaka wa Watanzania,Ni kweli Stars ilishuka kiwango ukilinganisha na kipindi cha Maximo, lakini Jan alikuwa na mipango ya muda mrefu.

-Ujio wa Kocha Kim Poulsen 2012-2014 ni ushauri uliofanyiwa kazi kwa maono ya Jan Poulsen,

Kocha Kim Poulsen alikuwa akivinoa vikosi vya timu za taifa za vijana na alipandishwa na kupewa jukumu la kuinoa Taifa Stars baada ya TFF kumtimua kocha Jan Poulsen.Alipokuwa anavinoa vikosi vya timu za taifa za vijana aliweza kuwaibua nyota wengi kama FrankDomayo,Simon Msuva, Ramadhan Singano, Edward Christopher, Idrissa Rashid ‘Baba Ubaya’, Hassan Kessy, Atupele Green, Jerome Reuben Lembele, Frank Sekule, Hassan Dilunga na wengine wengi,ambao baadaye wengine aliwapandisha kuichezea Taifa Stars.

Kocha Kim Poulsen alikubalika kwa wadau na wachezaji, Kim alikuwa anawajua wachezaji wa Kitanzania na alikuwa anatafuta mafanikio yake na Taifa Stars. Kwa wale waliokuwa wanafuatilia mpira uliokuwa ukichezwa na Serengeti na Ngorongoro walikuwa wanafahamu ni kocha mwenye uwezo gani. Aliibadilisha pia Taifa Stars ikaanza kucheza mpira tuliokuwa tunauota, baada ya miaka miwili kupita ya mkataba wake waliokuwa viongozi wa TFF chini ya rais, Leodeger Tenga wakampa mkataba mwingine.

-Ujio wa Kocha Mart Nooij 2014-2015

Baada ya mabadiliko ya kiuongozi ndani ya TFF kufuatia Tenga kumaliza kipindi cha pili cha uongozi, aliyekuja kuchukua nafasi ya Tenga baada ya uchaguzi alikuwa Jamal Malinzi. Rais huyu mpya wa TFF alifanya mabadiliko na kumfuta ajira ya kocha Kim Poulsen na ajira hiyo kumpa kocha Mart Nooij raia wa Uholanzi ili aiwezeshe Taifa Stars kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2015 jambo ambalo lilishindikana kwani Nooij alishindwa.
Katika kipindi Kim Poulsen alichoinoa Taifa Stars ilicheza mechi 15, kati ya hizo Taifa Stars ilishinda mechi 5, ilitoka sare 4 na ilifungwa mechi 6.
(Kocha Mart Nooij, 2014-2015 )
Kocha Mart Nooij alikuja wakati mbaya kweli kweli, wakati tunaohitaji matokeo, wakati tunaohitaji kushinda, wakati tuliokuwa tunahitaji kufuzu kushiriki Fainali za Afrika 2015, hata hivyo alishindwa kuiwezesha Taifa Stars kufuzu.

-Maoni yangu kuisaidia Taifa Stars.

Mafanikio ya soka yanahitaji kucheza kitimu ‘Team Work’, kama utakuwa na mabeki wazuri halafu huna washambuliaji hilo ni tatizo, kama klabu itakuwa na wachezaji wazawa wazuri kwenye kikosi cha kwanza hakuna shaka timu ya taifa itakuwa nzuri pia,Tatizo jingine baadhi ya wachezaji wanapokuwa timu ya taifa hawajitumi kama wanavyokuwa kwenye klabu zao,wanashindwa kung’amua kuwa mazoezi ya timu ya taifa ni ya muda mfupi hivyo wajitume, lakini wengine wanakuwa wavivu, hilo ni tatizo katika kufanya vizuri,Taifa Stars inapata kila inachohitaji na mdhamini anajitoa kwa hali na mali kuhakikisha hakuna kinachokosekana kwa wachezaji na benchi zima la ufundi,

Taifa Stars inapofanya vibaya ni lazima TFF itafute njia za haraka kutafuta ufumbuzi wa tatizo,Katika mechi dhidi ya Misri ambayo tulifungwa makosa binafsi pamoja na maandalizi ya chini kwa timu hiyo ndiyo yameigharimu,wachezaji walionekana kama hawajaandaliwa vizuri kisaikolojia kabla ya pambano lile jambo liliowafanya waonekane hawajiamini katika muda mwingi wa mchezo,Nchi nyingine wachezaji wa zamani wanakuwa karibu na benchi la ufundi, wanashahuri, lakini Tanzania kitu hiko hakipo, mchezaji wa zamani hupewi nafasi,tena ukionekana unachangia unaanza kubezwa, hili ni tatizo, ndiyo sababu kila siku tunazidi kuporomoka badala ya kupanda, mifumo ya soka letu inapotea,

Kocha Marcio Maximo anabakia kuwa pekee ambaye alionyesha mwanga wa kulitoa soka la Tanzania kutoka hatua moja kwenda nyingine, kocha huyu aliweka msingi imara wa timu ya Taifa kwa kuwaandaa wachezaji wengi wenye umri mdogo ambao baadaye waligeuka kuwa lulu Taifa Stars na kwenye klabu zao,Maximo alitambua udhaifu wa mfumo wetu wa soka na aliamua kuutafutia mwarobaini kwa kukusanya na kuwapa nafasi wachezaji wengi chipukizi kwenye kikosi cha timu ya Taifa, jambo lililowafanya vijana hao kukomaa mapema kiushindani,

Pia aliwahamasisha Watanzania waipende timu yao ya Taifa jambo ambalo wenzake waliofuatia wameshindwa kulifanya,katika makocha wanne ambao wameinoa Stars ndani ya kipindi cha miaka 10 iliyopita, Marcio Maximo bado rekodi zake hazijafikiwa,Maximo alilikuta soka hapa nchini likiwa limedoda,alijitahidi kuliinua na kuwafanya wengi warudishe mapenzi yao kwa mchezo huo hapa nchini,kwenye soka tunapima mafanikio ya timu kwa kuangalia kiwango cha uwanjani na matokeo yanayopatikana,Maximo alijitahidi kuifanya timu yetu ipate matokeo mazuri,Kocha Marcio Maximo alikuwa ni mtu wa matokeo.

Nimalizie kwa kusema tatizo la soka la Tanzania ni la Wachezaji wanaotumia vumbi la mkongo na dawa za kuongeza nguvu kabla ya mechi baada ya kufanya mapenzi usiku mzima,Kocha Marcio Maximo na Kim Poulsen walikuwa chaguo sahihi kwa timu ya Taifa,kuna tatizo kwenye mfumo wa soka letu hali inayowapa wakati mgumu makocha wanaopata fursa ya kuinoa timu ya Taifa,Taifa Stars lakini Kim na Maximo walifanikiwa kwa kiasi fulani kuibadilisha Taifa Stars,Kocha Marcio Maximo na Kim Poulsen kwa wakati tofauti kila mmoja kwa akili yake na idea yake waliifanya Taifa Stars iwe na sura ya kitaifa,

Taifa Stars ilileta ushindani kwa timu ambazo ilikutana nazo.Hata hivyo, wapo wadau wengine wengi ambao wanaona tatizo la Taifa Stars siyo makocha bali ni wachezaji wa Tanzania kwani hawajui mambo mengi ya msingi kama kukokota mpira, kupokea mpira, kutuliza kwa usahihi, kupiga pasi sahihi, kupiga pasi za kichwa, kuulinda mpira, kupiga mashuti sahihi, kunyang’anya mpira, kurusha mpira, upigaji wa faulo zenye ufundi, kuokoa mpira, upigaji wa kona, mbinu za ushambuliaji, ulinzi, ushambuliaji, mfumo wa ufungaji mabao, ukipa mzuri, umakini na matumizi ya juu ya akili uwanjani.

Lipo tatizo lingine la kuchagua wachezaji wa Taifa Stars kwa Random sampling,random selection inamuwia vigumu kocha kujua nani aanze nani atokee benchi,Uchaguzi wa mchezaji kutokana na game tatu au nne!?viwango vya kawaida vya wachezaji vinavyopambwa na Magazeti,tutafute independent consultant ambae atatusaidia kwenye uongozi tumpe management fee,na tutafute consultant mwingine aongoze board ya ligi,

Bila kuwa na biasness ya kumtafuta bingwa kwa mahaba ya Simba na Yanga, Serikali na sekta binafsi viingie makubaliano ya kujenga Academy za soka za watoto na Vijana kila Mkoa na Makocha wenye uzoefu na ujuzi mkubwa kama Charles Boniface Mkwasa wawe wakufunzi,nchi ina vipaji vingi lakini vipaji hivyo vya shule ya Msingi Leo ukiuliza utaambiwa ni Mwalimu Kilosa,mwingine mpiga debe Msamvu Morogoro,mwingine mwendesha bodaboda buguruni,tuwekeze kwe mpira,tusifanye tu starehe na burudani,Wachezaji wa Taifa stars waweke kambi Jeshini wajifunze Uzalendo,

Wachezaji wa Tanzania wanapaswa kuwa na uthubutu katika kutafuta mafanikio,Tazama Wachezaji wa kigeni wanavyomiminika kwetu,jiulize Watanzania Milioni 60 tunakosa kumpata Chama mmoja,au Moussane mmoja au Morrison mmoja,Je si Jonas Mkude,Je si Diatram Nchimbi,Je si Shomari Kapombe,ni muda sasa Taifa Stars ikawa na Wachezaji kutoka vilabu vya nje ya Dar es Salaam,watoto wa Dar es Salaam utozi,vumbi la mkongo na dawa za kuongeza nguvu za kiume, connection na Magazeti ndio kiki wanazotegemea.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Kunahaja ya kujua malipo wanayolipwa, hardworking with reward, pia mchezaji akiumia akiwa mchezoni na asiweze kuhudumia familia inakuwaje. Of coz hata ningekuwa mimi siwezi kujitosa to the maximum afu nilipwe 50k, nikiumia inaachiwa familia yangu. Aaah no, nihaiwezekani
 
Mkuu umeeleza kiundani sana hongera.

Lakini wewe shabiki wa Reli Kiboko ya Vigogo uliyekuwa pia shabiki wa Edibily Lunyamila, Mohamed Hussein Mmachinga na Salvatory Edward Mtaalamu hukuwahi kushabikia Simba wala YANGA kwa roho safi? Umetisha mkuu.
 
Tusimtafute mchawi wa soka letu! Tuwekeze kwa vitendo na siyo kwa maneno. Viwanja vyote vilivyoporwa na Ccm virudishwe kwenye Manispaa na Halmashauri zetu. Na hizo Halmashauri/Manispaa zipewe jukumu la kuvitunza lakini pia kuhakikisha kila Manispaa/Halmashauri inamiliki timu yake! Mbona Kinondoni na Mbeya wameweza!! Kwa nini wengine washindwe.

Tuwekeze kwenye soka la Vijana, na ikiwezekana yule Kim Poulsen arudishwe Nchini! Yule jamaa ana kitu. Kwa bahati mbaya viongozi wa TFF hawakukiona, au waliamua tu kumfanyia majungu kwa kuachana nae na kumkumbatia Mswahili Oscar Milambo.

Serikali itengeneze sera ya kuifanya michezo kuwa ajira rasmi kama zilivyo ajira nyingine! Itenge fungu la kutosha kwenye bajeti yake kwa ajili ya kuboresha viwwnja vya michezo na pia kuzisaidia timu zetu za Taifa.

Serikali itengeneze mazingira ya kuwavutia wawekezaji kuwekeza kwenye michezo ikiwemo soka, tofauti na ilivyo sasa. Ni ligi kuu pekee ndiyo yenye wadhamini wachache, huku zile ligi nyingine za chini zikiwa zinajiendesha kwa dhiki na taabu kubwa.

Serikali iruhusu uwepo wa uraia pacha! Ni muda sasa serikali ya CCM haitaki uwepo wa uraia pacha. Huku wakitoa sababu za kitoto kitoto tu! Uraia pacha ungevutia vijana wengi wenye vipaji na wenye asili ya Tanzania kuja kuchezea timu ya Taifa baada ya kukosa nafasi kwenye timu za Mataifa wanakoishi.

Anyway, ni mtazamo tu. Mbona China na India zina Wananchi zaidi ya bilioni, lakini kwenye soka ni nyanya tu! Marekani ni Taifa kubwa lenye nguvu duniani,lakini timu yake ya soka ni ya kawaida tu! Hivyo Tanzania kuchemsha kwenye soka isiwe kesi! Huenda kipaji chetu kipo kwingine kabisa! Ila tu kwa bahati mbaya hatuja gundua ni wapi.
 
Wampeleke Mahela na Kaijage uone kama hawajashinda mechi zote mapemaa asubuhi kama ya sadaka ya ibada ya kwanza
 
NINI TATIZO LA TAIFA STARS KUSHINDWA KILA MECHI!?

Leo 12:30hrs 24/01/2021

Nakubaliana na kila Mtanzania kwa 100% na ukizingatia nchi kama Zambia,Namibia,Guinea, Zimbabwe,Rwanda,Burundi,Kenya,Uganda na Burkina Faso tupo sawa tu kiuchumi tena tunaweza kuwa tumewazidi idadi ya watu ikiwa wao wapo Milioni kumi hadi ishirini na Sisi Watanzania tupo watu Milioni 60,sasa tunashindwa nini kupata wachezaji wazuri na kuwaleta makocha wazuri tupate Timu ya Taifa itayotoa Upinzani wa kweli kwa Afrika nzima!? Niulize swali hivi wale vijana wa copa cocacola ya kwanza wameishia wapi? Si walichukua world cup ya vijana wa copa cocacola brazil?Naomba kwanza kudeclare interest,kutangaza maslahi yangu,

Mimi ni shabiki wa "Reli Kiboko ya Vigogo" timu iliyokuwa ikidhaminiwa na Mzee wangu Mh Oscar Mloka na Adolph Ghikhas kutoka mtaa wa Kichangani na Wazee wengine wa Morogoro baada ya Udhamini wa shirika la Reli kukoma,nakiri sijawahi kuwa shabiki wa timu nyingine yoyote zaidi ya Reli kiboko ya Vigogo,japo niliwahi kuwashabikia akina Edibily Lunyamila, Mohamed Hussein.

"Mmachinga" Salvatory Edward lakini bado moyoni niliendelea kuikumbuka "Reli kiboko ya Vigogo", Wazee wa Morogoro waliisupport Reli Kiboko ya vigogo iliyokuwa na Shabiki maarufu "Yamungu" kutoka na historia ya mpira wa Morogoro hasa baada ya timu ya Mseto iliyoanzishwa Mwaka 1965 kuchukua ubingwa wa Tanzania Mwaka 1975 kwa mara ya kwanza ikivunja utamaduni wa timu ya Simba na Yanga kuchukua ubingwa mara tuu baada ya ligi kuanzishwa Mwaka 1965,

Vijana wengi wa sasa kama kina Erick Patrick,Silas Msuya,Benjamin Masumo,Moris John, Sylvester John,Gand Dizo,General Kabaro,Herry Bringbring,Chiko Junior na Leo Afrikanus mlikuwa hamjazaliwa naamini hamumjui hata Mohamed Mwameja,Kikosi hiki cha Reli kiboko ya Vigogo Miaka ya tisini,golini alikuwa anasimama Athuman Msomali,beki wa kulia Mohamed Mtono,beki wa kushoto mara nyingi alikuwa Abdallah Mkali,beki namba nne alikuwa Ramadhani Kilambo,Sentahafu alikuwa Gasper Lupindo,namba 6 alicheza Christopher Michael,Winga namba 7 ni Nassib Abbas namba nane alikipiga Yusuph Macho pamoja na Boniphace Njohole, straika wa kati alikipiga Duncan Butinini,namba kumi David Mihambo,bila kuwasahau Habib Kondo,Wema Juma "Fashanu", Mathias Mulumba,Ramadhani Kilambo, Abdallah Suleiman ‘Kaburu’ na kipa Sahau Said Kambi.

Winga ya kushoto Mbuyi Yondani na Peter Mjata,Kikosi hiki chini ya Kocha John Simkoko kilikuwa kinampiga 3-0 au 2-0 Yanga na Simba kila kinapokutana,kilikuwa kikosi hatari mno hasa kinapokutana na Simba au Yanga,ilifika kipindi Simba au Yanga wakija Morogoro walibadili njia badala ya kupita darajani Shan Cinema walikuwa wanazunguka hadi Lutheran Junior Seminari kukwepa kupita Mto wa Morogoro ambao waliamini kila wakivuka daraja la Mto Morogoro basi walikula 3-0 katika dimba la Jamhuri Mkoani Morogoro,Simba na Yanga walianza kuamini uchawi toka zamani sana,na ndio maana Taifa Stars inayoundwa na Simba na Yanga inashindwa,maana hakuna mpira wa kuchezwa bila uchawi.

-Simba na Yanga na Jiji la Dar es Salaam, kamwe halitatia Taifa Stats imara.

Vikosi zaidi ya Simba na Yanga vilivyotikisa soka la Tanzania ni Mseto Fc na Pamba FC au Tout Poisssant Lindanda,Tangu mwaka 1965 ilipoanza Ligi ya soka ya Taifa Tanzania, ubingwa umekuwa wa timu za Dar es Salaam kutokana na timu za mkoa huo kuutwaa kila mwaka. Hii ni kutokana na uwezo wa kimchezo wa timu hizo, hususan Simba na Yanga,Lakini ubingwa wa Muungano, ligi ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 1982 ikizihusisha timu mbili zilizoshiriki Ligi ya Bara na mbili kutoka Ligi ya Zanzibar, umewahi kutwaliwa na klabu za nje ya mkoa wa Dar es Salaam mara tisa katika miaka ya 1984, 1985, 1986, 1988, 1989, 1990, 1992, 1998 na 1999,

Ubingwa wa Tanzania Bara umetwaliwa nje ya Dar es Salaam mara tano katika miaka ya 1975, 1986, 1988, 1999 na 2000 tangu ligi hiyo ianze mwaka 1965.

Mseto FC ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kuupeleka ubingwa wa taifa nje ya Dar es Salaam mwaka 1975 ikifuatiwa na Tukuyu Stars mwaka 1986, Coastal Union ya Tanga 1988, na Mtibwa Sugar ya Morogoro 1999 na 2000.Katika kipindi hicho Mseto ilikuwa na wachezaji wazuri kama Said Gedegela, Charles Boniface Mkwasa, Hamadan, Vincent Mkude, Ramadhan Matola,

Wengine ni Aluu Ally, Shiwa Lyambiko, Hassan Shilingi, Omar Hussein, Spencer na Jumanne Hassan ‘Masimenti’ waliocheza fainali. Mwingine alikuwa Miraji Salum ambaye alikuwa na timu ya taifa, Taifa Stars,Enzi hizo Mseto ilikuwa chini ya kocha Mohammed Hussein Hassan ‘Msomali’ na baadaye ikaongezewa nguvu na kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Bernard ‘bernt’ Trauttmann ilipokuwa ikijiandaa kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kimataifa.Hiki ni kikosi cha Mseto FC ya Morogoro mwaka 1990, wakati huo inashiriki Ligi Daraja la Pili, ambayo sasa ni Daraja la Kwanza. Mseto imewahi kuwa bingwa wa Tanzania mwaka 1975.

Sasa hivi timu hii haipo kabisa katika ramani ya soka nchini. Timu nyingine maarufu mkoani Morogoro kama Tumbaku na Reli, ambazo pia ziliibua vipaji vya nyota wengine wengi nchini enzi hizo, nazo pia zimepotea katika ramani ya soka.Bila kusahau kikosi cha dhahabu,Kikosi cha Pamba au Tout Poissant Lindanda"Tupwisa Lindanda"Kipa namba moja Madata Lubigisa, Rajabu Msoma , Beya Simba, Nteze John, Kitwana Selemani, Fumo Felician, Paschal Mayala na kipa Paul Rwechungura,George Gole, Khalfan Ngasa, Ali Bushiri, David Mwkalebela, Maonwa Mkami, Alphonce Modesti, Juma Amiri Maftah na Nico Bambaga.

-Historia ya Taifa Stars.

Itakumbukwa Agosti 26,1979 Taifa Stars ilikuwa ikihitaji sare ya aina yoyote dhidi ya Zambia ili ifuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu ilipoanza kushiriki mwaka 1968.Taifa Stars ilikuwa ikicheza mechi hiyo ya marudiano dhidi ya Zambia kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika za mwaka 1980 zilizofanyika Lagos, Nigeria.Katika mechi ya kwanza iliyozikutanisha timu hizo, Taifa Stars iliilaza Zambia bao 1-0 ambalo lilifungwa na kiungo, Mohammed Rishard Adolph.Mechi ya marudiano ilichezwa mjini Ndola, nje kidogo ya jiji la Lusaka na timu ya Zambia ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao mwanzoni mwa mchezo,

Lakini Taifa Stars ilisawazisha bao hilo mfungaji akiwa Peter Tino.Bao hilo la Tino lilinyamazisha umati wa mashabiki wa Zambia waliokuwapo uwanjani kwani liliiwezesha Taifa Stars kufuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika 1980.Fainali za LagosBaada ya kufuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika 1980, katika fainali hizo, Taifa Stars ilichapwa mabao 3-1 na wenyeji Nigeria katika mechi ya ufunguzi, ilitoka sare ya mabao 2-2 na Ivory Coast kabla ya kuchapwa mabao 2-1 na Misri na kutolewa hatua ya makundi.Kwa miaka 35 sasa, Taifa Stars imekuwa ikisaka nafasi kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika, lakini imeshindwa kuwika.

Fainali za CHANMwaka 2009, Taifa Stars ikiwa chini ya kocha Marcio Maximo kutoka Brazil ilifuzu kushiriki Fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya Afrika (CHAN) baada ya kuichapa Kenya 2-1 na katika mechi ya marudiano iliichapa tena 1-0. Mechi iliyofuata Taifa Stars ilicheza dhidi ya Uganda na kushinda 2-0 na ziliporudiana zilitoka sare 1-1. Mechi ya mwisho Stars iliichapa Sudan 3-1 na ziliporudiana iliibuka na ushindi wa 2-1 na hivyo kufuzu fainali za CHAN.

Hata hivyo, katika fainali hizo za CHAN, Taifa Stars ilifungwa na Senegal 1-0, ikaishinda Ivory Coast 1-0 na ilitoka sare ya 1-1 na Zambia hivyo kutolewa katika hatua ya makundi.

@Makocha wa Taifa Stars#

-Kocha Marcio Maximo 2006-2010

Taifa Stars imekuwa ikinolewa na makocha mbalimbali wa kigeni na wazawa,Mwaka 2006 ilinolewa na kocha Marcio Maximo kutoka Brazil ambaye aliiwezesha Stars kushiriki CHAN 2009,Kingine alichofanikiwa kocha huyu ni kurudisha ari,moyo na uzalendo kwa wachezaji,pia Watanzania nao walirudisha moyo wa kuipenda Taifa Stars, walinunua fulana za kuiunga mkono,walifurika uwanjani kuishangilia, tulifungwa,lakini tuliridhika na msingi wa soka ulianza kujengeka chini ya Maximo.Kocha Marcio Maximo aliiongoza Taifa Stars kuanzia 2006 mpaka 2010 na katika kipindi hicho, Taifa Stars ilicheza mechi 43, kati ya hizo Taifa Stars ilishinda mechi 16, sare 15 na ilifungwa mechi 12,Pia Maximo alifanya mapinduzi ya aina yake baada ya kuipandisha Tanzania kwenye viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kutoka nafasi ya 167 mpaka nafasi ya 108.

-Kocha Jan Poulsen 2010-2012

Kati ya mwaka 2010 mpaka 2012, Taifa Stars ikawa inanolewa na kocha Jan Poulsen raia wa Denmark. Kocha huyu alipokuja alikuta Watanzania wamehamasika kuipenda timu yao ya taifa na yeye akaona lipo tatizo ambalo Watanzania wanalifungia macho, tatizo la kuendeleza mchezo wa soka nchini.Kocha Jan Poulsen akasema,”Watanzania ndiyo wenye jukumu la kuendeleza mchezo wa soka nchini hivyo wanatakiwa kutafuta mfumo thabiti utakaosaidia kufanikisha suala hilo na kuacha mtazamo wa kuangalia timu ya Taifa tu.”Wakati wa kocha Jan Poulsen, Taifa Stars ilicheza mechi 22, kati ya mechi hizo, Taifa Stars ilishinda mechi 5, ikatoka sare 7 na ilifungwa mechi 10. Pia aliiongoza Kilimanjaro Stars ya Tanzania Bara kutwaa Kombe la Chalenji kwa mara ya kwanza baada ya miaka 16, alipoifunga Ivory Coast kwenye fainali iliyofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

-Kocha Jan Poulsen atoa maono ya kujenga Academy ya soka kuanzia watoto hadi Vijana,

Kocha Jan Poulsen alisema anafahamu suala kuchagua timu ya Taifa ni gumu kutokana na ukubwa wa nchi, kwani rasilimali za kiuchumi zilizopo zinashindwa kusaidia mchezo wa soka, lakini alisema tunavyozidi kuchelewa kuusaidia mchezo wa soka ndiyo tunavyozidi kurudi nyuma katika mchezo huo,Kocha Poulsen alisema wachezaji wa Kitanzania anaowachagua Taifa Stars na wanaoendelea kuchaguliwa wanatokana na mfumo ambao Watanzania wameutengeneza ambao haujali soka la vijana.

Poulsen alisema wachezaji wa Tanzania wanakosa kufundishwa mambo mengi katika ngazi za chini kwa sababu anaona mambo mengi aliyokuwa anawafundisha wachezaji kwenye timu ya taifa walitakiwa wafundishwe wakiwa watoto au vijana.

Katika kipindi hiki ndiyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likamleta kocha Kim Poulsen kutoka Denmark, ambaye akawa anazinoa timu za taifa za vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) na miaka 20 (Ngorongoro Heroes),Jan Poulsen alikuwa na mipango mizuri, lakini ilionekana kushindikana kutokana na uharaka wa Watanzania,Ni kweli Stars ilishuka kiwango ukilinganisha na kipindi cha Maximo, lakini Jan alikuwa na mipango ya muda mrefu.

-Ujio wa Kocha Kim Poulsen 2012-2014 ni ushauri uliofanyiwa kazi kwa maono ya Jan Poulsen,

Kocha Kim Poulsen alikuwa akivinoa vikosi vya timu za taifa za vijana na alipandishwa na kupewa jukumu la kuinoa Taifa Stars baada ya TFF kumtimua kocha Jan Poulsen.Alipokuwa anavinoa vikosi vya timu za taifa za vijana aliweza kuwaibua nyota wengi kama FrankDomayo,Simon Msuva, Ramadhan Singano, Edward Christopher, Idrissa Rashid ‘Baba Ubaya’, Hassan Kessy, Atupele Green, Jerome Reuben Lembele, Frank Sekule, Hassan Dilunga na wengine wengi,ambao baadaye wengine aliwapandisha kuichezea Taifa Stars.

Kocha Kim Poulsen alikubalika kwa wadau na wachezaji, Kim alikuwa anawajua wachezaji wa Kitanzania na alikuwa anatafuta mafanikio yake na Taifa Stars. Kwa wale waliokuwa wanafuatilia mpira uliokuwa ukichezwa na Serengeti na Ngorongoro walikuwa wanafahamu ni kocha mwenye uwezo gani. Aliibadilisha pia Taifa Stars ikaanza kucheza mpira tuliokuwa tunauota, baada ya miaka miwili kupita ya mkataba wake waliokuwa viongozi wa TFF chini ya rais, Leodeger Tenga wakampa mkataba mwingine.

-Ujio wa Kocha Mart Nooij 2014-2015

Baada ya mabadiliko ya kiuongozi ndani ya TFF kufuatia Tenga kumaliza kipindi cha pili cha uongozi, aliyekuja kuchukua nafasi ya Tenga baada ya uchaguzi alikuwa Jamal Malinzi. Rais huyu mpya wa TFF alifanya mabadiliko na kumfuta ajira ya kocha Kim Poulsen na ajira hiyo kumpa kocha Mart Nooij raia wa Uholanzi ili aiwezeshe Taifa Stars kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2015 jambo ambalo lilishindikana kwani Nooij alishindwa.
Katika kipindi Kim Poulsen alichoinoa Taifa Stars ilicheza mechi 15, kati ya hizo Taifa Stars ilishinda mechi 5, ilitoka sare 4 na ilifungwa mechi 6.
(Kocha Mart Nooij, 2014-2015 )
Kocha Mart Nooij alikuja wakati mbaya kweli kweli, wakati tunaohitaji matokeo, wakati tunaohitaji kushinda, wakati tuliokuwa tunahitaji kufuzu kushiriki Fainali za Afrika 2015, hata hivyo alishindwa kuiwezesha Taifa Stars kufuzu.

-Maoni yangu kuisaidia Taifa Stars.

Mafanikio ya soka yanahitaji kucheza kitimu ‘Team Work’, kama utakuwa na mabeki wazuri halafu huna washambuliaji hilo ni tatizo, kama klabu itakuwa na wachezaji wazawa wazuri kwenye kikosi cha kwanza hakuna shaka timu ya taifa itakuwa nzuri pia,Tatizo jingine baadhi ya wachezaji wanapokuwa timu ya taifa hawajitumi kama wanavyokuwa kwenye klabu zao,wanashindwa kung’amua kuwa mazoezi ya timu ya taifa ni ya muda mfupi hivyo wajitume, lakini wengine wanakuwa wavivu, hilo ni tatizo katika kufanya vizuri,Taifa Stars inapata kila inachohitaji na mdhamini anajitoa kwa hali na mali kuhakikisha hakuna kinachokosekana kwa wachezaji na benchi zima la ufundi,

Taifa Stars inapofanya vibaya ni lazima TFF itafute njia za haraka kutafuta ufumbuzi wa tatizo,Katika mechi dhidi ya Misri ambayo tulifungwa makosa binafsi pamoja na maandalizi ya chini kwa timu hiyo ndiyo yameigharimu,wachezaji walionekana kama hawajaandaliwa vizuri kisaikolojia kabla ya pambano lile jambo liliowafanya waonekane hawajiamini katika muda mwingi wa mchezo,Nchi nyingine wachezaji wa zamani wanakuwa karibu na benchi la ufundi, wanashahuri, lakini Tanzania kitu hiko hakipo, mchezaji wa zamani hupewi nafasi,tena ukionekana unachangia unaanza kubezwa, hili ni tatizo, ndiyo sababu kila siku tunazidi kuporomoka badala ya kupanda, mifumo ya soka letu inapotea,

Kocha Marcio Maximo anabakia kuwa pekee ambaye alionyesha mwanga wa kulitoa soka la Tanzania kutoka hatua moja kwenda nyingine, kocha huyu aliweka msingi imara wa timu ya Taifa kwa kuwaandaa wachezaji wengi wenye umri mdogo ambao baadaye waligeuka kuwa lulu Taifa Stars na kwenye klabu zao,Maximo alitambua udhaifu wa mfumo wetu wa soka na aliamua kuutafutia mwarobaini kwa kukusanya na kuwapa nafasi wachezaji wengi chipukizi kwenye kikosi cha timu ya Taifa, jambo lililowafanya vijana hao kukomaa mapema kiushindani,

Pia aliwahamasisha Watanzania waipende timu yao ya Taifa jambo ambalo wenzake waliofuatia wameshindwa kulifanya,katika makocha wanne ambao wameinoa Stars ndani ya kipindi cha miaka 10 iliyopita, Marcio Maximo bado rekodi zake hazijafikiwa,Maximo alilikuta soka hapa nchini likiwa limedoda,alijitahidi kuliinua na kuwafanya wengi warudishe mapenzi yao kwa mchezo huo hapa nchini,kwenye soka tunapima mafanikio ya timu kwa kuangalia kiwango cha uwanjani na matokeo yanayopatikana,Maximo alijitahidi kuifanya timu yetu ipate matokeo mazuri,Kocha Marcio Maximo alikuwa ni mtu wa matokeo.

Nimalizie kwa kusema tatizo la soka la Tanzania ni la Wachezaji wanaotumia vumbi la mkongo na dawa za kuongeza nguvu kabla ya mechi baada ya kufanya mapenzi usiku mzima,Kocha Marcio Maximo na Kim Poulsen walikuwa chaguo sahihi kwa timu ya Taifa,kuna tatizo kwenye mfumo wa soka letu hali inayowapa wakati mgumu makocha wanaopata fursa ya kuinoa timu ya Taifa,Taifa Stars lakini Kim na Maximo walifanikiwa kwa kiasi fulani kuibadilisha Taifa Stars,Kocha Marcio Maximo na Kim Poulsen kwa wakati tofauti kila mmoja kwa akili yake na idea yake waliifanya Taifa Stars iwe na sura ya kitaifa,

Taifa Stars ilileta ushindani kwa timu ambazo ilikutana nazo.Hata hivyo, wapo wadau wengine wengi ambao wanaona tatizo la Taifa Stars siyo makocha bali ni wachezaji wa Tanzania kwani hawajui mambo mengi ya msingi kama kukokota mpira, kupokea mpira, kutuliza kwa usahihi, kupiga pasi sahihi, kupiga pasi za kichwa, kuulinda mpira, kupiga mashuti sahihi, kunyang’anya mpira, kurusha mpira, upigaji wa faulo zenye ufundi, kuokoa mpira, upigaji wa kona, mbinu za ushambuliaji, ulinzi, ushambuliaji, mfumo wa ufungaji mabao, ukipa mzuri, umakini na matumizi ya juu ya akili uwanjani.

Lipo tatizo lingine la kuchagua wachezaji wa Taifa Stars kwa Random sampling,random selection inamuwia vigumu kocha kujua nani aanze nani atokee benchi,Uchaguzi wa mchezaji kutokana na game tatu au nne!?viwango vya kawaida vya wachezaji vinavyopambwa na Magazeti,tutafute independent consultant ambae atatusaidia kwenye uongozi tumpe management fee,na tutafute consultant mwingine aongoze board ya ligi,

Bila kuwa na biasness ya kumtafuta bingwa kwa mahaba ya Simba na Yanga, Serikali na sekta binafsi viingie makubaliano ya kujenga Academy za soka za watoto na Vijana kila Mkoa na Makocha wenye uzoefu na ujuzi mkubwa kama Charles Boniface Mkwasa wawe wakufunzi,nchi ina vipaji vingi lakini vipaji hivyo vya shule ya Msingi Leo ukiuliza utaambiwa ni Mwalimu Kilosa,mwingine mpiga debe Msamvu Morogoro,mwingine mwendesha bodaboda buguruni,tuwekeze kwe mpira,tusifanye tu starehe na burudani,Wachezaji wa Taifa stars waweke kambi Jeshini wajifunze Uzalendo,

Wachezaji wa Tanzania wanapaswa kuwa na uthubutu katika kutafuta mafanikio,Tazama Wachezaji wa kigeni wanavyomiminika kwetu,jiulize Watanzania Milioni 60 tunakosa kumpata Chama mmoja,au Moussane mmoja au Morrison mmoja,Je si Jonas Mkude,Je si Diatram Nchimbi,Je si Shomari Kapombe,ni muda sasa Taifa Stars ikawa na Wachezaji kutoka vilabu vya nje ya Dar es Salaam,watoto wa Dar es Salaam utozi,vumbi la mkongo na dawa za kuongeza nguvu za kiume, connection na Magazeti ndio kiki wanazotegemea.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
Mpelekeni Jecha,Mahera na Jaji Kaijage muone kama hamtarudi na kombe saa nne asubuhi tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom