Nini tatizo la kuwa na uhusiano wa kimapenzi na albino? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini tatizo la kuwa na uhusiano wa kimapenzi na albino?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Annael, Jan 31, 2012.

 1. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,400
  Likes Received: 10,513
  Trophy Points: 280
  Samahani sana wana MMU labda ninalotaka kuongelea ni nje ya jukwaa.
  Mimi ninataka kujua mtu akiwa na uhusiano wa kimapenzi na mlemavu wa ngozi (albino) kuna matatizo gani ambayo yanaweza yakatokea pande zote mbili?
  Mimi siyo mtaalamu wa afya ila huwa nina sikia albino wanapungukiwa na melanini kwenye ngozi yao.
  Je haiwezi kuleta madhara mnapokuwa pamoja katika ndoa?

  Ninaomba maelekezo kwa upana.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Jamani!!
  Tatizo alilonalo albino sio mba au chawa useme mkikaa karibu karibu atakuambukiza. Kama umependa endelea kupenda.
   
 3. Mmbande J M

  Mmbande J M New Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mjadala wako kuhusu albino hauna mashiko; nenda kajipange upya. Majadiliano kama hayo hayana nafasi kwenye jamii inayozingatia usawa.
   
 4. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  swali lako nadhani ni swali sahihi. Sisi, tunaofikiria katika anga za haki na usawa, ni wepesi na rahisi kusema kunashida gani kutoka na albino. Nikiri wazi mimi sifahamu ugumu wake - wala unyororo wa ngozi yake, kwani sijakutana naye hata mmoja na kuwa na hisia za mapenzi. Wale niliokutana nao, nimewapenda katika mitizamo yao na utu wao. Kwahiyo, utashi wao si pungufu dhidi yetu. Pia, kitaalamu hakuna tatizo la kiafya kwa kuwa na albion, ugonjwa uliopo ni wa kifikira za idi na imani za ajabu ajabu.
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  Tusubiri wataalamu hapa.
   
 6. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Albino nao ni binadamu na wana feelings kama wewe. Asikuzuie mtu kama anakuvutia. Lakini isiwe unataka kujaribisha tu. Kama unampenda basi mpende kweli na dont break her heart. Sababu utakuwa umefanya makosa ambayo hata muumba hatakusamehe. GOODLUCK/
   
 7. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa nampenda sana mwalimu wangu wa biology nyie wacheni tu...mana alikuwa ni mwanamke mzuri sana kutoka Angola na kipindi chake ilikuwa lazima nikakae desk la mbele....Yule mwalimu alikuwa very smart na alikuwa anafanya maksudi vile kunionyesha chupi alio vaa kwa mastyle yake pale tupo kwenye class...afu ananibania jicho....ahhh zamani wakati nasoma we wachaa tu...haahaha.

  BTW; reason ya kumuongelea huyo mwalimu, kuna siku nilimuliza swali kama hilo akasema fazaa; takufelisha kwenye somo langu....if you sincerely think that, by having kids with an albino will automatically produce one.

  Yani wewe kama umeamua kuoa kachukue mali hakun shida...Mimi nakupa hongera kwa kumpenda huyo kiumbe, mana ni binadamu kama sisi na wenye moyo mzuri kama wewe ndo wanafikiria hatua ya kuwao....Mungu akubarikie sana na muishi maisha mazuri wewe na mke wako.
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,262
  Trophy Points: 280
  Watu wote wanakwepa swali lako:
  Kuoa albino, ambaye ana upungufu wa melanin kwenye ngozi kuna challenges zake ukilinganisha na za kuoa mwanamke asiye albino.
  1 albino kutokana na upungufu wa melanin ana anapaswa kuepuka kukutana na jua direct. Jua litamsababishia kupata kansa ya ngozi endapo hatatumia mafuta maalum kujikinga. Mwalimu wangu mh margareth nkanga alipigania cream hizi ziletwe kwa ruzuku ila nadhani hajafanikiwa bado. Creme hizi ni ghali kidogo lakini pia kutokana na ngozi yake anapata challenge kufanya kazi ya kukaa juani kutwa mfano kulima
  2 mara nyingi huwa na matatizo ya macho kutokana na sensitivity waliyonayo
  3 unyanyapaa kutoka kwa jamii mbali mbali, mfano utahitaji kumtetea na kumlinda wakati wote ili asiumie
  4 kuna uwezekano wa kupata mtoto albino endapo na wewe una recessive gene ya ualbino. Utahitaji kumtunza na kumlinda kwa ziada ukishirikiana na mama yake
  Ukimpenda mwenzi wako, ni rahisi kubebana kwenye udhaifu wowote alio nao kama mengine yote. Jiandae kisaikolojia kuyakabili hayo na utashangaa mtafurahia maisha kama kawa. Just don't break her heart sugar boy, ok? Kama hauko serious be straight from day one!
   
 9. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Huombi ushauri wewe bali umeamua kuweka hadharani namna unavyowanyanyapaa albino. Au ni mganga wa kienyeji wewe?. Tehe
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kuna la kuisaidia polisi
  ikitokea huyo mpenzi wako kakukimbia bila taarifa

  na watu wakafikiri umemuuza kwa wanaotafuta albino
   
 11. Atubela

  Atubela JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 180
  Tuko pamoja na mimi nilitaka kumwambia hivyohivyo.
   
 12. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  he he he the boss umeua hapo...unaweza ukawekwa ndani
   
 13. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #13
  Mar 19, 2014
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,911
  Trophy Points: 280
  thanks sana naamini amesaidika, maamuzi yake sasa
   
Loading...