Nini tatizo haswa kwa halmashauri zetu kiasi cha kufikia kila mahali kugeuka kuwa mzigo?

Mbugi

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,488
257
kupitia J/F ninaomba wataalam mtusaidie nini haswa tatizo kwa halmashauri zetu? kuendelea kuwa tatizo na hata baada ya reform kubwa ya kuanzia mwaka 1999 kufuatia local gvt reform policy ya 1998. kinachonifanya niendelee kuwa na wasiwasi ni kufuatia kushindwa kutimiza wajibu wake, kama vile ilala kushindwa kutoa huduma ya usafi kwenye soko la samaki feri, na kuendelea na mchakato wa zabuni kinyume cha taratibu za manunuzi kiasi cha kumfanya waziri kusimamisha mchakato huo. lakini mbaya zaidi ni mwenendo unaotia shaka na hata baada ya halmashauri zetu kupewa wataalam kama wahasibu wazuri, na wengineo kuendelea kufanya hovyo kama halmashauri ya kishapu ambapo mpaka sasa baraza la madiwani lililazimika kugeuka kamati na kufikia maamuzi ya kwasimamamisha wakuu wa idara na wahasibu karibu 13, unaweza ona pia halmashauri ya Misungwi nk.
 
Back
Top Bottom