Nini tatizo? Binti mrembo anajua kuvaa, msomi ila ananuka mdomo

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Wakuu salaam

Sina lengo la kukashfu maumbile ya mtu, bali kutaka kujua sababu ziwe za kisayansi au nyinginezo. Kuna binti nipo naye karibu mazingira ya ofisini kwetu. Huyu binti ni nzuri na anajua sana kuvaa kuendena na wakati

Mara nyingi nikimkaribia na tukiwa tunaongea naskia harufu ya mdomo wake. Nilijua ni tatizo la siku moja ila kadri siku zinavyosonga mbele naona bado ile hali anayo

Sasa wakuu hivi hii usababishwa na Nini? Naamini mswaki anapiga vizuri tu ila sijui chanzo cha yule binti kunuka mdomo kiasi kile

Najisikia noma kumwambia na sijui nitumie njia gani kumfikishia ujumbe kwamba Ananuka mdomo atafute tiba
 
Mtu yeyote anaelala usiku bila kupiga mswaki lazima anuke mdomo.

Mtu unaswaki asubuhi, Siku nzima unakula kila utakacho, afu unalala hivyo hivyo, unategemea nini?

Procedure ni kupiga mswaki asubuhi na usiku umalizapo kula swaki ndo ulale.
Akifanya hivyo ikashindikana mshauri anunue mouth wash.

Ikishindikana jua ana jino bovu limetoboka, halifanyii usafi uchafu umejaa humo.
Ila mtihani unao ni ngumu sana sanaaa kumwambia mtu hicho kitu.

Kuna mwanaume alikuwa ananipenda sana tu,alikuwa na kila kitu mwanamke anachotamani, ila nilishindwa proposal yake, kila akiniuliza kwa nini simpendi namdanganya namchukulia kama kaka.
Kumwambia ilishindikana, ati nae sasa hivi kaoa, hivi wanalala vip kama kuongea tu naskia mmmmh , dah mapenzi upofu.
Halafu wa hivyo wana meno mazuri asikwambie mtu. Na kama ni mdada unakuta ni nzuri balaa.
 
Wasichana wengi wa dar wananuka nuka sana sana midomo na vikwapa. Wengi hawana hela ya kucheki dentists kila miezi sita na pia wengi hawana hela ya kununua chibu pafyumu ya laki na nusu.
Ila ukimkuta demu ana gari nzuri utakuta ananukia vizuri hadi gari linanukia hadi kwenye injini.. Tatizo ni la kiuchumi, wasichana wengi kazi zao ngumu.
Siyo kwamba wavulana hawanuki? Apana ila haipendezi kukuta demu mzurii ananuka mdomo au kwapa.
Msela hata akinuka atajijua na maisha yake hakuna atakayekuwa na time nae, ila mademu watu tunawatamani ndo maana hatupendi mnuke nuke ovyo, mnatupa wakati mgumu tunapofanya michakato ya kuwala.
 
Hii niliwahi kuwaambia.

Tukiwa O Level kuna mshkaji wetu akang'oa pini inaitwa Amina, hii pini ilikua inasoma Perfect Vision basi tulikua tunampa kampani mshkaji wetu kwenda kwa shemeji.

Over time tukajua shemeji ana shida na harufu ya mdomo mshkaji kumwambia hakuweza akatuomba ushauri.
Washkaji wa Class Z tukamshauri amnunulie dawa ya meno na mswaki ampe.

Jamaa akampelekea binti whitedent kubwa na miswaki miwili.

Jamaa akaja kutuambia tatizo halijakata.

Akamuuliza binti "Kama umemaliza zile zawadi nikuletee zingine" binti akajibu "Hapana nimezitunza zawadi zako mpenzi wangu"
 
Jaribu kumshauri awe ana mtembelea daktari wa afya ya kinywa atapata ufumbuzi wa tatizo lake .

Madaktari wa afya ya kinywa wanashauri kuwa una kwenda kufanya checkup ya kinywa kila baada ya miezi 6 .. Pia katika maisha yetu tuwe tuna jiwekea utaratibu wa kutumia dawa za kusafisha kinywa. Asikuambie mtu 1wapo ya mambo ya aibu ni kunuka mdomo .. Ni jambo la aibu sana na fedheha kubwa mnoo
 
Mwili wa mwanadamu huwa ni mchafu kwa ndani, tusiwekeze sana kwenye usafi wa nje tukasahau usafi wa ndani ya mwili
 
Mtu ana tatizo unajisikia noma kumwambia una kwama wapi we muelekeze tu mjue mtatatuaje tatizo
Nina uhakika hata yeye hajui suluhisho, la sivyo angesha mshauri. Aende kwa wataalamu wa masuala ya mdomo/meno au/na ent (ear, nose and throat)
 
Back
Top Bottom