Nini tafsiri ya madai ya Polepole, kwamba John Pombe Magufuli alitaka kuhongwa na Wahujumu Uchumi?

Hii inaonesha wazi kuw a rais naye kuna watu anawaogopa maana siku hiyo alidai kuna watu majina anayo waliotaka kukwamisha kamati. Sasa hao watu ni akina nani na anewachukulia hatua gani? Huyo aliyetaka kumuhonga ni nani na kwanini asimkamate?!
 
Kuwa makini mkuu,mleta mada sio Godbless Lema,ni Dr. Godbless. Mpaka hapo umakini wako ni finyu au bashite kabisa.

Nashukuru kwa kupotoka na kiasi Fulani ku-addess asiyehusika.Kuwa Bashite nayo phenomenon ya kutusaidia kuwa makini zaidi pengine bila hivyo tungejikuta tumeharibikiwa sehemu kubwa zaidi.Hongera kwa kuwa kinyume cha Bashite!
 
Acha upuuzi wako wa kutaka kupotosha nini Polepole alichosema kwa kuleta maelezo yasiyohusika katika mazingira haya. Ni vizuri mazingira ya tukio nayo yakatumika kuamua jambo. Si kutuletea maelezo ya jumlajumla ili kutoa uamuzi wa matukio ambayo yametokea katika nyakati na mazingira tofauti na watu tofauti.
Mazingira wakati wa Mkapa yalikuwa tofauti sana wakati wa kutunga sheria na hata kuandika mkataba. Nchi ilikuwa haina mgodi hata mmoja wa mfano na ilikuwa inavutia wawekezaji kwa kuwabembeleza na kwa ushindani na mataifa mengine. Kwa mazingira haya kiongozi hawezi kuwaomba rushwa wawekezaji anaowataka kwa hamu na ghamu. Pia muwekezaji hawezi kumhonga kiongozi au watu waliokuja kumuomba awekeze kwao. Makubaliano yalifanyika na uwekezaji ukaanza. Baada ya utekelezaji kunadosari za utekelezaji zimejitokeza na kuhitaji marekebisho.
Wakati wa Kikwete alikuja na marekebisho ya baadhi ya vipengele kwenye sheria na mikataba kwa baadhi ya makampuni. Haya yalifanyika kwa ushauri wa tume ya Jaji Bomani. mrabaha ukawa asilimia nne 4% badala ya 3%. Pia Mh Kikwete aliona dosari kwenye kukokotoa hasara kunaweza kufanya makampuni kutangaza hasara mpaka siku yanafunga mgodi. Kamati hiyo ilikuja na mapendekezo. Kwa marekebisho hayo GGM walianza kulipa 30% ya kodi. Mazingira ya kushauriana kama haya hayakushawishi kampuni kutafuta mtu wa kumhonga. Baadhi ya watummishi wa umma na walikuwa rahimu kwa migodi kiasi cha kushindwa kufanya wanayopaswa kufanywa. Pia kumiminika kwa misaada na kuwa na projecti chache za maendeleo zinazohitaji fedha nako kulifanya eneo la madini lisichunguliwe sana. Si kwa madini pekee hata maeneo mengine yalikuwa hayalipi kodi ipasavyo. Haya hayakutokea kwa Kikwete kuhongwa bali kwa urahimu wake na kuwaamini wasaidizi wake.
Mazingira ya sasa si rafiki kwa aina yoyote ile ya wakwepa kodi. Kujitokeza kwa baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kumhonga kiongozi kama anahongeka inawezekana.Hivyo kauli ya Polepole inasadifu kabisa katika mazingira haya. Wenye hotel wameshughulikiwa akiwamo Mbowe na sasa migodi. Sababu kubwa ni kiongozi anataka kutekeleza miradi anayoizindua kwa pesa zetu. Misaada iwe ni ziada.
Kwa hiyo, wanapokaa kimya tafsiri ni kwamba Viongozi wamepokea mzigo. Ila Wanapopiga kelele kwamba tunataka kuhongwa aidha fungu ni dogo Au wanatafuta umaarufu wa kisiasa. Kama umekiri kwamba Mkapa alikuwa anawavutia wawekezaji ndio maana akasaini Mikataba kwa nini mnatupigia kelele za Kuibiwa??
 
Ni sawa na kusema majenshi yote yameenda rogue maana yameshindwa kumkamata huyo mtoa rushwa. Raisi ana TISS pale pale magogoni maana msimamizi wake ni waziri wa ofisi ya raisi, ana mkuu wa majeshi, ana mkuu wa polisi, magereza, uhamiaji, ffu,halafu anashindwa kuwakamata hao watu au walimjia kwa njia ya upepo nini?
Ndugu elewa kitu kimoja TISS hawaruhusiwi kukamata mtu wao ni kufanya uchungunzi na magereza na uhamiaji hawana ruhusa ya kukamata JWTZ wanaruhusiwa kukamata kwa sharti la kumkabidhi mtuhumiwa police ili wao wamfungulie mashtaka hivyo sheria zetu ni kituko kuliko mjuwavyo
 
MMadai ya polepole kuwa raisi alikataa hongo ya wahujumu uchumi kwangu mimi ina maana kuwa maraisi wastaafu Mkapa na Kikwete walikuwa wanahongwa na kupokea hizo hongo.
Nasema hivi kwakuwa naamini raisi haongeki na kwamba si rahisi fisadi akaingia ikulu kwa ajili ya kuongea na raisi mambo ya kumhonga.

Na kama inawezekana basi akina Mkapa na Kikwete walipokea hongo ndio maana walikaa kimya japo rasilimali zilikuwa zinaibiwa. Kinyume chake kama ikulu ni mahali patakatifu basi huyu polepole ahojiwe kwa kuidhalilisha ikulu kwa kujua au kutokujua.
 
MMadai ya polepole kuwa raisi alikataa hongo ya wahujumu uchumi kwangu mimi ina maana kuwa maraisi wastaafu Mkapa na Kikwete walikuwa wanahongwa na kupokea hizo hongo.
Nasema hivi kwakuwa naamini raisi haongeki na kwamba si rahisi fisadi akaingia ikulu kwa ajili ya kuongea na raisi mambo ya kumhonga.

Na kama inawezekana basi akina Mkapa na Kikwete walipokea hongo ndio maana walikaa kimya japo rasilimali zilikuwa zinaibiwa. Kinyume chake kama ikulu ni mahali patakatifu basi huyu polepole ahojiwe kwa kuidhalilisha ikulu kwa kujua au kutokujua.
 
Kwa hiyo, wanapokaa kimya tafsiri ni kwamba Viongozi wamepokea mzigo. Ila Wanapopiga kelele kwamba tunataka kuhongwa aidha fungu ni dogo Au wanatafuta umaarufu wa kisiasa. Kama umekiri kwamba Mkapa alikuwa anawavutia wawekezaji ndio maana akasaini Mikataba kwa nini mnatupigia kelele za Kuibiwa??
Majibu yangu yanajitosheleza sana. Hakuna mwenye akili atakayeshinda kunielewa. Kwa kuwa wewe umeamua kujitoa akili basi nami nitafurahi kukuita mjinga.
Mazingira ya sasa kwa wanaokwepa kulipa kinachostahiki kwa serikali lazima watasakamwa. Na kwa kuwa katika mazingira ya sasa wamebanwa katika tatizo hata wao wanaamini litaharibu hadhi yao ndio maana wanahangaika kuhonga ili wajinasue. Mazingira haya hayakuwapo kwa waliotangulia hivyo si busara kuyafananisha kama kichwa chako kinavyokupeleka.
 
Ndio maana nimekuuliza kwa fikra zako alichokifanya Mkapa kilikuwa sahihi simply because ya kuvutia investors. Sasa kwa nini mnatupigia kelele za Kuibiwa? Yaani mlango mmeacha wazi kwa kigezo cha kuvutia wageni halafu mnaanza kupiga kelele za Wezi? CCM imepitisha Sheria ya madini kwa hati ya dharura in favour of investors, mlikuwa mmehongwa? Mikataba bado ni siri, mmehongwa?
 
Takururu walitakiwa wafanye kazi yao kwa tuuma na pole pole ni mzee wa kula matapishi yako always

Swissme
kwanza huyo polple nikumwangaliaga nachekaga sanah...kwanza elimu yake imefikia wapi..maaana mmmhh..kama enzi zile za nape bwanh
 
Ndugu elewa kitu kimoja TISS hawaruhusiwi kukamata mtu wao ni kufanya uchungunzi na magereza na uhamiaji hawana ruhusa ya kukamata JWTZ wanaruhusiwa kukamata kwa sharti la kumkabidhi mtuhumiwa police ili wao wamfungulie mashtaka hivyo sheria zetu ni kituko kuliko mjuwavyo[/QUM
najua hayo yote my point of emphasize ni kwamba huyo ni amiri jeshi mkuu so ana vyote at is disposal
 
Polepole ni kiongozi ndani ya chama ambae ameamua kuwaaminisha walimwengu kama kumfikia Raisi ni rahisi
Huyu jamaa amejiaibisha,ameobesha kwamba kipropaganda ni mbovu
Nashauri Raisi wetu amtake huyu mwenezi athibitishe pasi na shaka na akishindwa basi akae pembeni ili kulinda heshima ya nchi
 
Back
Top Bottom