Je, jina lako/ID unalotumia JamiiForums lina maana yoyote?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Hili swali linawahusu wale ambao hawatumii majina yao ya kweli hapa ukumbini. Je, jina lako lina maana yoyote? Kuna sababu yoyote ile iliyokufanya uamue kutumia jina hilo!?

Nilikuwa nimeamua kutosema lolote kuhusiana na hali ya kisiasa ndani ya nchi yetu (kuwa bubu) pamoja na kwamba nilikuwa siridhiki na mambo mengi sana niliyokuwa nayasikia kwa Watanzania wenzetu, kuyashuhudia kwa macho au kuyasoma kwenye magazeti yetu mbali mbali. Niliamua kuwa kimya kwa sababu nilijua sauti yangu kama zilivyo sauti za Watanzania wengi ambazo hazisikilizwi na walio madarakani, haitafika kokote.

Mpaka nilipoanza kutembelea hapa miezi ya mwisho wa mwaka 2006 nikafurahishwa sana na michango ya baadhi ya wanachama na kuona hapa kuna sauti ya umma ambayo kama itaendelea na kushamiri basi itasaidia sana kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya nchi yetu.

Nilibahatika kuwa Bongo kipindi cha kuapishwa Kikwete, pamoja na kuwa hakuwa amenigusa kama kiongozi mpya wa nchi yetu nilitiwa hamasa kubwa kuwaona Watanzania wenzangu wakiwa na shauku kubwa ya kumpata Kikwete kama Rais mpya wa Tanzania na weng walikuwa na matumaini makubwa toka kwake na wengine kumuita "Mkombozi wetu". Watu walipoanza kulalamika kuhusu utendaji wake kama Rais wa nchi, mimi nilikuwa nawaambia ni mapema mno kuanza kumlaumu. Niliomba apewe angalau kipindi cha mwaka mzima tangu aingie madarakani na hapo ndipo anastahili kuanza kutupiwa lawama mbali mbali kuhusu utendaji wake.

Basi nilipoamua kujiunga nikaamua jina la Bubu maana nilikuwa nimeamua kunyamaza kimya kwa miaka mingi pamoja na kutoridhishwa na mengi. Nikaukumbuka na ule wimbo wa 'Nginde ngoma ya ukae" Bubu ataka kusema mambo yanapomzidia. Ndipo baada ya mwaka na ushee tangu Kikwete aingie madarakani nikaamua rasmi kujiunga ili niungane na Watanzania wenzangu katika mijadala mbali mbali inayohusu hatima ya nchi yetu maana ile miezi 12 ilikuwa imekatika na kuvurunda kwa srikali ya Kikwete kulikuwa kunazidi kushamiri.

Hivi ndivyo jina BAK lilivyozaliwa rasmi na mnamo February 2007 nikajiunga rasmi na ukumbi huu wakati huo ukiitwa Jambo Forums.

Kama kuna baadhi mtapenda kuchangia kuhusu maana ya majina yenu na kama kuna sababu rasmi za kuamua kuyatumia majina hayo basi mnakaribishwa.
 
Mimi ni kichuguu kwa sababu ninatunza mchwa na nguchiro kwa pwamoja. Yaani nina uwezo kutoa pumba na mantiki kwa pamoja bila wasiwasi wowote. UPO Mzee wangu? Leo ni weekend.....

6069d1254630137-je-jina-lako-unalotumia-jf-lina-maana-yoyote-368483.jpg

368483.jpg
 

Naisadiki asili yangu na niliposoma kitabu cha bwana Richard Wright mwandishi mmoja wa fasihi za afrika-amerika kiitwacho, "The Native Son" nikagundua ningekuwa muhusika mkuu katika fasihi ile ni machache yaliyofanywa na weupe dhidi yetu ningeyavumilia bila shaka ningekuwa na mtazamo mkali zaidi nakufanya mambo kadhaa dhidi ya ukandamizaji wa watu wa magharibi na amerika ya kaskazini kwa waafrika. Kwenye JF likaanza jina la "The Native Son" kuashiria kuchukia unyanyasaji unaofanywa na mwafrika yeyote wakiwemo viongozi wetu wa kiafrika na Tanzania ambao wanasahau asili zao na kutukuza ugeni wakigeuzwa vibaraka na kuzidhurumu nchi zao kwa ufisadi mkubwa, bila shaka haibu iwe juu yao.

Nabaki hivyo.
 
Hivi ni kweli asilimia kubwa ya usernames ze2 zina-reflect tabia, hobbies, mionekano na hata profesion ze2?!
Mfano 'Injinia', 'FOE', 'Kenge(Eng.)' kweli nyie ni ma-engineers?!
Mkuu mwenyewe 'The Boss' nakua tempted kuku2mia Job application yangu coz unaonekana ni boss flan sehem flan.
Pia 'Mpenzi wa Islam' na 'Ulamaa' napata hisia nyie ni ma-ustaadhi safi.
Dada 'Pretty' waonekana ni mrembo flan hivi matata halikadhalika dada ye2 'Firstlady1' napata hisia uko kama angle flani na shemeji ye2 ni mkubwa flan somewhere ndo maana u r his 1st lady.
Mkuu 'Arsene Wenger' wewe waonekana mwanamichezo haswa. Huwa 2nakutana kule kwa spesho thread ya Arsenal. Yaonekana Arsnal ikifungwa siku yako imeharibika. :)
'Mahesabu' yaonekana wewe kwa ma-calculus, statistics.... uko balaa si mchezo. Au?!
Hivi 'Bonge' kweli lkn wewe ni bonge yaan mwili mkubwa!
Mzee 'Advocate jasha' yaonekana we ni mtaalam wa mambo ya sheria!
Mkuu 'Dar-es-salaam' wewe waonekana ni mtoto wa mujini, umekaa sana Dar!
'care4all' utakua m2 flan si mbaguzi wa dini, kabila wala rangi. Seems like unajal sana wengine!
Kuna usernames nyingine nacheka sana nikiziona, na ku-comment publically nì noma. mfano 'Semenya' na mkuu 'Chapa kiuno' na nyingine nyiingi.
 
Naam thread nzuri sana inaweza kuwekwa kama thread ya kudumu ambayo kila member mpya anapojitambulisha pia si vibaya kutoa maana ya jina analotumia pia! inaburudisha! kuhusu jina ninalotumia limetokana na mtazamo wangu juu ya hoja mbalimbali, hoja inapotolewa kuna nafasi tatu kuipinga(kwa hoja), kuikubali (bila kufuata mkumbo au kuangalia nani mtoa hoja) au kutokua na lakusema(no comment) juu ya hoja hiyo! hivyo kuzaliwa jina Mawazomatatu. Kila mara kuna kua na mawazo ya aina tatu juu ya hoja yoyote.
 

Naisadiki asili yangu na niliposoma kitabu cha bwana Richard Wright mwandishi mmoja wa fasihi za afrika-amerika kiitwacho, "The Native Son" nikagundua ningekuwa muhusika mkuu katika fasihi ile ni machache yaliyofanywa na weupe dhidi yetu ningeyavumilia bila shaka ningekuwa na mtazamo mkali zaidi nakufanya mambo kadhaa dhidi ya ukandamizaji wa watu wa magharibi na amerika ya kaskazini kwa waafrika. Kwenye JF likaanza jina la "The Native Son" kuashiria kuchukia unyanyasaji unaofanywa na mwafrika yeyote wakiwemo viongozi wetu wa kiafrika na Tanzania ambao wanasahau asili zao na kutukuza ugeni wakigeuzwa vibaraka na kuzidhurumu nchi zao kwa ufisadi mkubwa, bila shaka haibu iwe juu yao.

Nabaki hivyo.

Mambo ya Bigger Thomas siyo?

Mimi Mzee wa ma latest technology, ma singularities, ma black holes, ma white holes,ma time wraps, ma parallel universes na ma movies.

Kwa hiyo Bluray (get it right, no "e") ilipotoka ilini arrest na clarity yake.

Na kwa sababu nafikiri naleta a level of clarity that is above normal -If I can be that modest- up in here, then I gots ta be tha Bluray of this B.I.
 
Che kalizozele ni jina la utani la marehemu babu yangu mzaa baba,alifariki baba akiwa bado mwanafunzi hivyo sikupata bahati ya kumuona babu yangu kipenzi kwani nilikuwa bado sijazaliwa.

Nasimuliwa mengi kuhusu babu yangu huyu,mojawapo ni tabia yake ya kutokutegemea cha mtu na ndipo alipoamua kujipa jina la Che kalizozele,yaani mtu wa kujitafutia.

Baada ya kuamua kuachana na jina la babawatatu ambalo ni jina langu halisi nikaamua kutumia jina hili kama kumuenzi babu yangu ambae alimjengea msingi mzuri wa maisha baba yangu hivyo nae kuwa na uwezo wa kunipa elimu.

On top of all niliamua kulitumia jina hili baada ya kutoka katika arobaini ya marehemu bibi mzaa baba kama ishara ya kumkumbuka nyanya wangu kipenzi.
 
Back
Top Bottom