Nini suluhisho la wafugaji wa kukosa mahali pa kulishia kwa wilaya za Kahama na Bukombe

kashibaba

Senior Member
Nov 26, 2019
191
269
Kwa wajuvi wa mambo, salaam kwenu wadau,

Limetolewa tangazo rasmi sasa kwa pori Tengefu la Kigosi almaarufu Game lilioko ukanda wa magharibi mwa nchi yetu kuwa Hifadhi ya Taifa.

Binasfi naifahamu mbuga inapatikana kanda ya ziwa,,upande wa kaskazini inapakana na wilaya ya Bukombe kuanzia maeneo ya buntubili mpaka maeneo ya bugelenga,,msasani,,nyakasaluma,,inaenda mkoa wa shinyanga wilaya ya ushetu,,inaingia tabora wilaya ya urambo kidogo n.k. upande wa magharibi inapakana na wilaya ya kakonko mkoa wa kigoma na inaungana nafikiri na pori la myowozi.

Hoja yangu hapa ni kuwa kanda ya ziwa lipo tatizo kubwa la maeneo ya malisho ya mifugo ya jamii inayolizunguka lililokuwa pori hili la akiba na sasa ni Mbuga rasmi,,wafugaji wengi walikosa malisho kbs kutokana na kazi za kilimo na watu wakaanza kuingiza mifugo katika poli la halimashauri na mwisho wa siku wakawa wanachungia ndani ya pori hili ambalo sasa ni Mbuga,, Miaka ya hapa nyuma tumeshuhudia wafugaji wakitaifishwa mifugo yao kwa kosa la kuingiza mifugo game reserve na kwa kweli wengi waliumia kwa maumivu makali na game reserve wa maeneo haya ni wala rushwa wa kutosha.

Kuna operation ya ondoa mifugo amabayo ilifanyika kwa ufanisi miaka ya 2016 na kuendelea,,kiukweli amabao hawayajui haya mambo watayaona kirahisi lakini hali ilivokuwa ni ya kuumiza sana,,wabunge wa mae eo haya waliyapigia kelele sana haya na utaifishwaji huu wa mifugo ya watu,,kwa wanaojua mazingira ya maeneo haya wataelewa kuwa maeneo ya kufugia hakuna kabisa na hakuna njia mbadala wa watu hawa wafanyeje,,tulifikiri labda pori hili lingemegwa japo kidogo kuwapa unafuu wafugaji hawa.

Sasa serikali inawafikiriaje wafugaji wa maeneo haya maana kiuhalisia hawana kabisa maeneo ya malisho, wengi wamekimbilia mapori ya biharamlo,,uvinza na kasulu ambako nako baada ya muda hali itakuwa mbaya. Kwa nini watu wizara hizi zinazoingiliana za mifugo,ardhi na watu wa utalii walio na dhamana ya mbuga hizi wakatafakari kwa kina na kuwasaidia watu wa eneo hili.

Lengo ni kujaribu kuona naman nzuri ya kuwasaidia wafugaji ambao hawana pa kwenda,,
Hapa jukwaani ni mahali ambapo naamini vionvozi wetu wanapata pata data kidgo zinazowasaidia kujua changamoto za jamii kiurahisi pia,,karibuni wadau kwa maoni na michango yenu juu ya hili kwamba tunaweza kuwa na cha kuwashauri viongozi wetu kupitia jukwaa hili.
 
Jambo ambalo eaziri mpina amekutana nalo ushetu leo ni kilio cha wafugaji wengi wanaozunguka hifadhi hii,,uporaji waliousema hapo mheshimiwa waziri ni kidogo tu,,litafakari kwa kina

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karine hii bado wafugaji wanatafuta maeneo ya bure ya kulishia? Je wanapo uxa hizo mifugo pesa hupeleka wapi?

Duniani kwa sasa hakuna aina hii ya ufugaji, na huu ni ufugaji wa enzi za ujima, Communism.

Wanashindwa kiwa na Ranch zao? Wanashindwa kuunganisha mitaji na kununua Ranchi na kufugia?

Hawa sio wa kuonea huruma hata kidogo na pia sio wa kudekezwa, Ufugaji ni biashara wanapo uza Mifugo mbona hawalamiki?

Wanauza mifugo wanaende kuwekeza kujenga Magest House then wanarudi kutaka maeneo ya kuchungia

Ujima sio communism Ni communalism..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi namushukuru binasfi pamoja na management yako waziri mpina kiasi umejionea mwenyewe hali ilivokuwa kwa operation za kuwatoa wafugaji walioingiza mifugo ndani ya kigosi,,kiukweli maeneo haya wafugaji hawana kbs mahali pa malisho,,nilichojaribu kusema ni muhimu watu hawa tutafute namna nzuri kwa mazingira yetu wafanyaje shughuli zao,,kama tunataka wapunguze mifugo tuwekeze nguvu kubwa kwa namna ya kuelimisha watu wetu waone fursa ya kufuga kisasa na kimkakati,,hali umejionea waziri mpina,,nafahamu umetokea familia ya kifugaji unaelewa pia kiundani hali hii inavowaumiza wafugaji,,malalamiko ya mnada wa hapo buntubili umesikia,,japo kidogo lakini utakuwa umeelewa hali halisia,,wizara zetu zinazoingiliana katika hili ni muhimu mkae pamoja na kulitatua kwa pamoja,,,nini suluhisho kwa wafugaji wa kanda hii kikosa mahali pa kulishia mifugo yao? Swali hili waziri wetu wa mifugo bado sijaona kama kwa ziara hii umelijibu,,yawezekana umelijibu katika vikao ulivyokuwa ukifanya na watalaamu na wasimamizi lakini publicly hatujakusikia..pia nikishukuru kbs kuona umuhimu wa kuangalia maeneo haya kwa ziara uliyoifanya...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu namna hii bado ipo sana hapa kwetu Tanzania,,yaani sioninsehemu ambayo watu wanafuga kwa namna tofauti,,ukiangalia mvomero hapa,,kilosa,malinyi kwa upande wa morogoro,,wamsai wamejaa,,pita manyara yote,arusha,tanga,serengeti,mara nzima kwa ujumla,,mwanza,,shy,geita,kigoma,rukwa na mbeya haya maeneo yana idadi kubwa ya mifugo ingawa inatofautiana kiasi na wana mfumo mmoja wa kufuga...serikalivyetu itazame mbeleni sana kuwasaidia permanently hawa watu maana tunazidi kuongezeka wakati ardhi yetu iko vilevile,,,ni muhimu kuchukua hatua mapema
Karine hii bado wafugaji wanatafuta maeneo ya bure ya kulishia? Je wanapo uxa hizo mifugo pesa hupeleka wapi?

Duniani kwa sasa hakuna aina hii ya ufugaji, na huu ni ufugaji wa enzi za ujima, Communism.

Wanashindwa kiwa na Ranch zao? Wanashindwa kuunganisha mitaji na kununua Ranchi na kufugia?

Hawa sio wa kuonea huruma hata kidogo na pia sio wa kudekezwa, Ufugaji ni biashara wanapo uza Mifugo mbona hawalamiki?

Wanauza mifugo wanaende kuwekeza kujenga Magest House then wanarudi kutaka maeneo ya kuchungia

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom