Nini suluhisho la Tanzania kwenye mivutano ya kidini na kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini suluhisho la Tanzania kwenye mivutano ya kidini na kisiasa

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Pepombili, Mar 12, 2011.

 1. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Katika kupitia maoni na mada mbali mbali zinazojadiliwa kwenye JF nimegundua jambo moja la msingi amablo watu wengi lazima hulijadili nalo ni la Dini .
  Dini imechukuwa nafasi kubwa kwenye mijadala ya JF hata katika masuala yasiyohusu dini kama vile masuala ya uchumi, naamini ya kwamba ni vigumu kutenganisha dini na siasa japo hilo wajumbe wengi hawalitaki kulisikia tukumbuke ya kwamba watanzania wengi ni wakiristo na waisilamu ambao kwa namna moja au nyengine hawezi kutenganisha moja kwa moja siasa na dini.
  Katika nchi nyingi zenye watu wa imani moja suala hili nadra sana kutoke ila kwenye nchi yenye imani mchanganyiko hili hutokea sana na si ajabu hapa kwetu kutotokea maana Tanzania sio nchi ya malaika ambao wao hawakinzani.
  Nimeona juu ya wakiristo wakilalamika juu ya ya Tanzania kujiunga na OIC na mahakama ya kadhi na pia vile vile nimeona waisilamu wakilalamika juu ya MOU na kuwepo kwa ubalozi wa Vatican na mfumo kristo.(kila kinachojadiliwa kipo wala kisipingwe)
  Wengi wanapinga kuwepo kwa haya na wengi wanakubali kuwepo kwa haya.
  Tumewahi kushuhudia Tanzania ikipeleka wanajeshi wake Nigeria kwenye vita vya Biafra kwa kigezo cha kwamba wakiristo wa kule wanaonewa na waisilamu kwa hio Tanzania ilipeleka wanajeshi kule kwenye ile vita ili Nigeria ijitenge na kuondosha mzizi wa fitna, yaanii wakiristo wawe na nchi yao na waisilamu wawe na nchi yao hilo lingepelekea kukata mzizi wa fitina , na hivi karibuni tumeshuhudia Sudani ikijitenga wala sio dhambi kwa mitazamo yao,
  Mchelea mwiba mguu huota tende ,kwa kuangalia mifano miwili ya Sudan na Nigeria tumeona kwamba Nigeria imeshindikana mpaka sasa kuna fujo kubwa za kidini ila Sudan kunaonekana kumetulia na wanachi wengi wameridhia kugawanywa kwa Sudan (hata kwenye mgawanyo wa Sudan tunae mwakilishi wetu wa Tanzania na ameshuhudia kugawanya kwa nchi hio)
  Je? kwa kigezo hicho vipi na kwetu Tanganyika tukaigawa ili kuepusha mguu kuota tende (Utaratibu wa kuigawa nchi uwe hivi wakiristo wapewe zile sehemu zenye wakiristo wengi na waisilamu wapewe sehemu wenye waisilamu wengi wale wakiristo wenye kuishi maeneo ya waisilamu wengi waende kwenye maeneo yao na wale waisilamu wenye kuishi maeneo ya wakiristo wengi waende kwenye maeneo ya waisilamu.) nadhani hili litasaidia kila mwenye dini aweze kutekeleza dini yake wanaotaka mahakama ya kadhi na OIC watatekeleza na wanaotaka MOU wataendelea nayo na wale wasio na dini watachagua pa kuishi ila kwa kufuata taratibu za sehemu husika.
   
 2. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  1. Somalia,Irak,Yemen,Pakstan kuna Dini ngapi,Je wana amani ?? Waislam wakishapata nchi yao je unadhani wataelewana? Washia na Sunni bado utata mwingine,hata hiyo kuhusu kadhi subiri zitachapwa ngumi za wao kwa wao.Je umesahau Ugomvi wa Maimam na BAKWATA?? Shehe Simba vs RIP Gorogosi??????

  2.Achana na poropoganda za JK alikuwa anatafuta huruma za watu wachache na sasa tayari kapata tulia unyolewe!!!! Jk kama Marais wote wa bara na visiwani wanapenda starehe za Pombe,kitimoto na Kujirusha na totoz.No Uislam nor Uikristo hapa bongo!!!!! Ukijitenga usishangae jk etc wakajiunga na christians.

  3.Kuhusu Elimu,wapo waislam wanapenda kusomesha watoto wao shule za Kiikristo mfano JK,watoto wake wanasoma shule za Katoliki pale Tanga.Ina maana anapenda watoto wake wapate ""malezi ya Masista na Mapadre wa Katoliki.""

  4.Jk hana udini ila uwezo wa kuongoza watu hana!!! Ndo maana alijua hawezi kushinda urais akaamua kutumia dini lakini si Muislam,ndo maana mwaka 2005 Waislam wengi hamkumkubali kama Lipumba wa CUF'' Pombe,kitimoto anatumia.tukijitenga atapata wapi hivi????

  Tusijitenge baadala yake kila mtu ajue Mungu wake.Kuna Waikristo bado wanaamini Uchawi na Waislam bado wengine wanaamini Uchawi.

  Tusisahau Chenge(christian) vs Bunge.Mufti simba vs Gorogosi(moslemz leaderz) walilamikiana kuhusu kutumia ''ushirikina.'' kutafuta nafasi.
  "" DINI KWA WAAFRIKA NI KAMA VIPODOZI''''
   
 3. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mawazo yako yanafaa zaidi mahala ambapo watu wamekata tamaa zaidi kwa kushindwa kutatua migogoro yao ya kidini. Kwa ufupi Tanzania hatuna migogoro ya kidini iliyofikia hatua mbaya kiasi hicho ila kuna watu kama wanasiasa (kwa maksudi), watanzania wenye ugumu wa kuchanganua mambo (kwa bahati mbaya sana) wanaojikuta wakishabikia sana udini kwa maslahi binafsi na wengine ushabiki tu kama ilivyo kwa swali la "Nani zaidi kati ya Simba na Yanga?". Kila mtu atavutia kwake hata mwisho baadhi watataka kupigana.
  Kwa Tanzania hii usishangae sana kukuta mtu anafurahia tu rais kuwa wa imani yake, tena kwa jina pasipokujali ni muumini safi au la na kama anatimiza wajibu wake au hapana. Hii ni tabia ya kawaida duniani kote hasa kwa watu ambao dini waliletewa na wageni maana tunakuwa kama tunakurupukia mambo hivi.
  Bahati mbaya zaidi hatuna kiongozi anayeweza kukemea hilo kwa nguvu ya kutosha kwa kuwa waliopo madarakani ajenda yao ni kupora wakati baadhi ya viongozi wa dini wamekata tamaa na kuanza kuropoka tu bila kujali implication za kauli zao. Kila mtu anataka kufurahisha hadhira yake. Kama Maaskofu wanajua waumini wao wamechoshwa na serikali lazima watasema kwa kuwa ni rahisi kueleweka na Maimamu nao wanaangalia upande wao.
  Tatizo kubwa lililopo; baadhi yetu wanadhani tutaingia peponi kwa kupima ushindi wetu dhidi ya dini nyingine katika maswala ya kidunia wakati hakuna dini au msahafu unaosema hivyo isipokuwa baadhi ya viongozi wa dini, tena wengi wao wanakuwa ni fanatics. Kwani serikali ikishirikiana na dhehebu la dini kuendesha hospitali ya rufaa inayotoa huduma kwa watanzania wote shida ipo wapi? Wakatoliki wakifanya hivyo Mbeya mathalani, Wasuni wakafanya hivyo Mwanza na Songea, KKKT wafanye vivyo hivyo Zanzibar nk..nk... tatizo la MOU sijui liko wapi! Mahakama ya Kadhi ikianzishwa na kuendeshwa na waislamu wenyewe kwa ajili ya waislamu na kugharimiwa na waislamu wenyewe tatizo liko wapi hapo?
  Kama kuna uwezekano wa jumuiya za kidini kama BAKWATA kushirikiana na OIC bila kuitambulisha Tanzania kama nchi ya dini fulani pekee huko nje, binafsi sioni ubaya. Jambo ambalo mie ningependa kuliona ni kuendeleza Nchi yetu kama State, kutokuwa na dini na kupunguza kufanya mambo yake kama taasisi ya Kidini.
  Tanzania ni nchi isiyofungamana na dini yoyote katika level ya Serikali lakini raia wake wanaamini katika dini taofauti ilhali wakiishi pamoja na kwa ushirikianao.
  Wakati mwingine nashindwa kuelewa! Mfano itokee sasa hivi serikali ijae watu wa imani moja tu lakini wachape kazi zao kwa uadilifu na matunda yaonekane na kuwanufaisha watu wote nchini atakayelalamika atakuwa anatafuta nini? Mshahara wa Waziri au Mkuu wa Mkoa unanihusu nini mimi mtumishi wa Benki au Mfanyabiashara halali wa mbogamboga na matunda?
  Amini usiamini Tanzania bado ina watu wanakaa vijiweni muda wote pasipo kujishughulisha lakini ukimwambia dini yake wananyanyaswa kwa kuwa Wakuu wa wilaya ni wachache anaibuka haraka anataka kuandamana ama kulalamika. Huyu alichokosa ni elimu tu ili kutofautisha kazi za taifa/nchi isiyojitambulisha kwa dini na kazi za kueneza dini zinazofanywa na viongozi wa dini. Jukumu hili linapaswa kusimamiwa vizuri na serikali ambayo serikali yenye nia safi.
  Udini unaolalamikiwa katika kipindi hiku unatokana na serikali kushambuliwa sana kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake na ili kuepuka kupambana na hoja wao wakadai udini unaitafuna nchi ili watu wa dini hasa tuliokosa busara na ustahamilivu tushambuliane sisi kwa sisi kwa kauli za kukurupuka wakati wao wana Chukua Chao Mapema na kutulia wakijifanya wanakwamishwa na migogoro ya kidini katika kutekeleza wajibu wao.
   
 4. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Thanks Ndugu,
  Kama atakuwa mtu wa kuelewa atakuwa amenufaika sana. Kama ni kozi basi umemaliza topics zote.
   
 5. p

  peterkaaya New Member

  #5
  Aug 21, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh! kaka nimefurahi kwa mtazamo wako juu ya suala la dini ila kaka mtazamo wako na ushauri wako wa mwisho mh! naomba nicheke kwanza hahahahahaha! umewaza kaka! labda inaweza kusaidia mkuu
   
Loading...