Lord Diplock MR
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 1,393
- 3,234
Ninajua kuwa Waziri Mkuu akifariki au kujiuzulu basi Baraza la Mawaziri huhesabika kuwa limevunjika.
Pia muda mchache kabla ya Rais mteule kuapishwa Baraza la Mawaziri huvunjika.
Lakini Katiba yetu ipo kimya juu ya nini hutokea pale Rais anapokuwa amefariki. Je, Baraza la Mawaziri huendelea na kazi?
Je, punde kabla ya Samia Suluhu Hassan kuapishwa Baraza la mawaziri halivunjiki? Na pengine je baada ya kuapishwa Baraza la mawaziri la Magufuli litaendelea au Mheshimiwa Samia atatakiwa kuja na Waziri mkuu wake, na Baraza la mawaziri lake?
Wataalamu wa sheria na utawala tupeni mwongozo