Nini status ya Baraza la Mawaziri la Magufuli sasa na baada ya Samia Suluhu Hassan kuapishwa?

tenor.gif
 
Mama Samia anamalizia ngwe waliyoanza na John Pombe Magufuli

Yeye ataanza ngwe yake kamili kwake 2025-2035

Mungu wa mbunguni amtunze
Aweke uwanja sawa na Katiba mpya Tume HURU hapo sawa
 
Kama hoja ni kuwa hakuna serikali mpya inayoingia nini logic ya Baraza kuvunjika anapojiuzuru Waziri mkuu au akijiuzuru Waziri mkuu Kuna serikali mpya inaingia?
Waziri Mkuu ni kiongozi wa shughuli za serekali bungeni na ndie bosi wa mawairi kwa hivyo anapojiuzuru anakuwa amepoteza confidence ya baraza zima.....kwa hivyo baraza lazima livunjwe lote.
Kitu kimoja cha kuongeza hapo mawaziri wanapokuwa wanafanya vikao vyao wakikubaliana jambo huwa ni kitu kimoja tunaita collective responsibility.....kwa muntadha huo waziri mkuu akijiuzuru baraza zima linavunjwa
 
Mama kama anataka kweli ajijengee imani kwa Watanzania wengi, alivunje tu hilo Baraza lililojaa wanafiki, wachumia tumbo na waimba mapambio.

Na Majaliwa asiachwe kuendeleza uongo wake! Naye abakie tu na Ubunge wake.
Nilikuwa nataka Kuchangia ila kwa Ukweli mtupu uliouandika hapa sioni haja tena kwani umemaliza kila Kitu Ndugu na Heko sana tu.
 
Ninavyo fikiri ni kwamba, Mama Rais mteule akisha kula kiapo atavunja baraza la mawizi. Na kumteua mwana sheria mkuu wa serikali. Atapeleka jina la waziri mkuu bungeni ambalo litapitishwa na bunge baada ya kuoitishwa hilobjina na la VP ndipo watakaa kuunda serikali. Ni mawazo yangu ya elimu ya darasa la saba Bla zamani. Msinitupie mawe wakuu.
 
Mama Samia anamalizia ngwe waliyoanza na John Pombe Magufuli

Yeye ataanza ngwe yake kamili kwake 2025-2035

Mungu wa mbunguni amtunze
Hapo uliposema 2025 -2035 huna budi kurejea kusoma tena katiba inasema nini, kama atagombea tena basi ni term moja yaan 2025-2030
 
Ninajua kuwa Waziri Mkuu akifariki au kujiuzulu basi Baraza la mawaziri huhesabika kuwa limevunjika.

Pia muda mchache kabla ya Rais mteule kuapishwa Baraza la mawaziri huvunjika.

Lakini Katiba yetu ipo kimya juu ya nini hutokea pale Rais anapokuwa amefariki. Je Baraza la mawaziri huendelea na kazi?

Je, punde kabla ya Samia Suluhu Hassan kuapishwa Baraza la mawaziri halivunjiki? Na pengine je baada ya kuapishwa Baraza la mawaziri la Magufuli litaendelea au Mheshimiwa Samia atatakiwa kuja na Waziri mkuu wake, na Baraza la mawaziri lake?

Wataalamu wa sheria na utawala tupeni mwongozo
Baraza la Mawaziri linabaki hiyo hivyo, ila kama Rais haimzuii kupanga safu yake muda wowote ikimpendeza.
 
Mama Samia anamalizia ngwe waliyoanza na John Pombe Magufuli

Yeye ataanza ngwe yake kamili kwake 2025-2035

Mungu wa mbunguni amtunze
Viongozi wote wakuu lazima wale kiapo mbele ya rais.
Hawa waliopo waliapa mbele ya Magu na sio mama Samia. Hivyo lazima baraza lipigwe chini. Hiyo itashuka hivyo hadi kwa ma Rc, IGP, CDF, TISS..... Hivyo....
 
Back
Top Bottom