Nini status ya Baraza la Mawaziri la Magufuli sasa na baada ya Samia Suluhu Hassan kuapishwa?

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,356
2,000
Ninajua kuwa Waziri Mkuu akifariki au kujiuzulu basi Baraza la Mawaziri huhesabika kuwa limevunjika.

Pia muda mchache kabla ya Rais mteule kuapishwa Baraza la Mawaziri huvunjika.

Lakini Katiba yetu ipo kimya juu ya nini hutokea pale Rais anapokuwa amefariki. Je, Baraza la Mawaziri huendelea na kazi?

Je, punde kabla ya Samia Suluhu Hassan kuapishwa Baraza la mawaziri halivunjiki? Na pengine je baada ya kuapishwa Baraza la mawaziri la Magufuli litaendelea au Mheshimiwa Samia atatakiwa kuja na Waziri mkuu wake, na Baraza la mawaziri lake?

Wataalamu wa sheria na utawala tupeni mwongozo
 
mzushi

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
3,042
2,000
Katiba haijasema chochote kuhusu baraza la mawaziri maana Rais akiunda Baraza huwa anamshirikisha Makamu wa Rais na Waziri mkuu kwa hiyo Baraza la mawaziri balo lipo hai.

Angalizo :Kutokana na tabia ya Bwana Mkubwa ilivyokuwa si bure asilimia 95 ya mawaziri hakumshirikisha mtu yeyote, kwa hiyo uwezekano wa Mama Samia kuanza upya ni mkubwa sana.
 
ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
10,416
2,000
Makamu wa raisi ni part and parcel ya presidency Sheria inatambua John na Samia ndio waliounda baraza kwa hivyo halivunjwi bali anarithi .........

But as days goes by anaweza kulibadirisha atakavyo akishauriana na makamu wake......ie nyofoa huyu weka yule nk....lakini hawezi kulivunja lote kwa wakati mmoja kwa kuwa hakuna serekali mpya hapo inayoingia madarakani ni ile ile
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
27,723
2,000
crazy-dance-1.gif

Bwashee!!Bwashee!! Ongeza mtori
 
Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,356
2,000
Makamu wa raisi ni part and parcel ya presidency Sheria inatambua John na Samia ndio waliounda baraza kwa hivyo halivunjwi bali anarithi .........
but as days goes by anaweza kulibadirisha atakavyo akishauriana na makamu wake......ie nyofoa huyu weka yule nk....lakini hawezi kulivunja lote kwa wakati mmoja kwa kuwa hakuna serekali mpya hapo inayoingia madarakani ni ile ile
Kama hoja ni kuwa hakuna serikali mpya inayoingia nini logic ya Baraza kuvunjika anapojiuzuru Waziri mkuu au akijiuzuru Waziri mkuu Kuna serikali mpya inaingia?
 
Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,356
2,000
Makamu wa raisi ni part and parcel ya presidency Sheria inatambua John na Samia ndio waliounda baraza kwa hivyo halivunjwi bali anarithi .........
but as days goes by anaweza kulibadirisha atakavyo akishauriana na makamu wake......ie nyofoa huyu weka yule nk....lakini hawezi kulivunja lote kwa wakati mmoja kwa kuwa hakuna serekali mpya hapo inayoingia madarakani ni ile ile
Na Kama anaapishwa kwenda kuwa Rais mwenye mamlaka kamili vipi soon baada ya kuapishwa akitangaza kulivunja baraza lote la mawaziri?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom