Nini siri ya 'Single Mothers' kujaza social platforms?

mwemweremwemwere

JF-Expert Member
Jan 4, 2016
606
660
Ukiingia insta unakutana kibao, Snapchat wapo, kwenye Dating Apps huko ndo balaa, JF mama na FB ndo usiseme

Nimegundua hata wale maslay queen "wabinua viuno" ni memba wazuri wa kundi hili.

Hii kitu imenifikirisha sana. Ila ni wazi kuwa watu hawa bado wana kiu ya kumiliki wenza wao, lakini nimejiuliza tu;

Je, wameshindwa kabisa kurudisha moyo kwa waliozaa nao hapo mwanzo wakayajenga?

Je huko kitaa au makazini hawapati watu wanaoonyesha hisia kwao au wako busy kiasi hawapati muda wa kujimix wakapata wenza wapya ?

Kuna ticha aliwahi kunambia ukiwa na mtoto wa kike mchunge kwa masaa 24/7 dhidi ya jicho la mwanaume kwani hata pale unapohisi bintiyo yupo salama chumbani kwake, bado kuna mashababi wanammendea kwa kumpigia simu, kumgongea dirishani, kumchimbia vitobo nk. Inakuwaje sasa mwanamke huyu ambaye kwa nadharia ya mwalimu wangu anahitaji ulinzi kwa kuwa anawindwa masaa yote aonekane anahaha kiasi hiki kusaka mwenza?

Wakuu ni kwamba dunia imebadilika kiasi kwamba "seori" za yule ticha wangu hazifanyi kazi tena kwa saivi au?

Karibuni tujadili kwa amani.
 
Mwanaume hajisifii kupachika mimba na kutelekeza mtoto na mama. Zaa kwa makubaliano na mwenza wako sio kwa bahati mbaya. Hizi mimba za bahati mbaya ndiyo chanzo cha usingle mama.
Hivi unajua ishu ya U-single Mom ni pana, Sio kila single mom alitelekezwa/alikimbiwa na Mwanaume
*Wapo wanaomtegeshea Mwanaume mimba ili amuoe
*Wapo waliokua katika ndoa wakaachika wakiwa na watoto
*Na wapo waliotaka tuu kuwa na Mtoto as umri umeenda na anahitaji mtoto
Hata usitupe Sisi Lawama peke etu Mkuu hizo Scenarios zote zpo mtaani

I'm on that good kush and alcohol
 
Hivi unajua ishu ya U-single Mom ni pana, Sio kila single mom alitelekezwa/alikimbiwa na Mwanaume
*Wapo wanaomtegeshea Mwanaume mimba ili amuoe
*Wapo waliokua katika ndoa wakaachika wakiwa na watoto
*Na wapo waliotaka tuu kuwa na Mtoto as umri umeenda na anahitaji mtoto
Hata usitupe Sisi Lawama peke etu Mkuu hizo Scenarios zote zpo mtaani

I'm on that good kush and alcohol
Nimestick hapa kwenye mimba zisizo na mpango au makubaliano. Hapa tunaweza kusaidiana kuondoa japo kidogo hili tatizo. Tuachane na hao watalakiwa.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom