Uchaguzi 2020 Nini siri ya mafanikio ya wagombea wa CCM katika ujazaji na urejeshaji fomu za uteuzi?

Ni chama Dola...

Ukishakuwa wewe ndiye umeshika mpini...upendeleo wa namna fulani fulani hautaukosa.

Lakini pia ndicho chama kikongwe...kina uzoefu....na usikute fomu wanajaza na mkurugenzi
 
Mwandishi ungekua unafikiri vizuri na huna mahaba na chama Fulani na huna unafiki na unafuatilia siasa za Tanzania kwa undani usingeandika hii mada.
Ungeona Soni Sana.
 
Tulishuhudia wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, leo pia tumeshuhudia katika mchakato wa uchaguzi mkuu:

1. Wagonbea wa CCM walijaza fomu vizuri, zimepokelewa bila shida

Baadhi ya wagombea wa upinzani hawakujaza fomu vizuri? Ni nini shida kwa vyama hivi? Hawajui KKK tuwarudisha vidudu?

2. Wagombea wa CCM waliwahi kurudisha fomu katika ofisi za tume...
Siri ya mafanikio ni NEC,jaji ni mtiifu kwa muajiri wake, asilimia kubwa ya wagombea wa ccm ni utopolo ila fomu zao nec hawakagui ni kupitisha tu
 
Chadema hua wana shida moja na inajirudia mara kwa mara. Kuwekeza nguvu na muda kwa watu wa juu wenye uelewa na kwa kiasi fulani wanaweza kujipigania huku wakisahau na kuwatelekeza wa huku chini ambao ni wengi na kama wanapata ushindi ina impact kubwa kwa chama.. Unawekeza attention yote kwa Lissu, unapoteza majimbo 18 by surprize. Kwa tulivo kuwa busy kufuatilia kama Lissu anapita ama la hili la wagombea 18 ni kama hatukuona likiwa linakuja
 
CCM huwa wanasambaza wanasheria wao kuhakikisha fomu zinajazwa vizuri. inawezekana hili linawasaidia sana.

Makandokando mengine ni wagombea wa upinzani kukosa uaminifu kwa vyama vyao hivyo kununuliwa hasa ukizingatia wengi wao husimama wenyewe kwa gharama zao wakati wa kampeni huku ukiwa huna uhakika wa kushinda.

kukwepa hasara, wanaona bora wafanye biashara
Pole kwake Tondu Lissu urais unahitaji maandalizi ya kimkakati na ya muda mrefu.
 
Dhuluma tu na Wizi.
Uongozi wa NEK unahalalisha udanganyifu.
NEC haitaki wananchi watumie haki yao ya msingi kuchagua viongozi wao.
Imejikita katika kuvuruga uchaguzi.

Mtu ni mtanzania halali na analipa ada ya kuchukua basi jukumu la NEK ni kuhalikisha fomu inahazwa vema na si vinginevyo.
 
Jibu ni Tumeccm hao ni kitengo cha maccm sasa unategemea kitengo cha maccm waengue wagombea wao? 😳

Tulishuhudia wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, leo pia tumeshuhudia katika mchakato wa uchaguzi mkuu:

1. Wagonbea wa CCM walijaza fomu vizuri, zimepokelewa bila shida

Baadhi ya wagombea wa upinzani hawakujaza fomu vizuri? Ni nini shida kwa vyama hivi? Hawajui KKK tuwarudisha vidudu?

2. Wagombea wa CCM waliwahi kurudisha fomu katika ofisi za tume.

Wagombea wa upinzani (baadhi) walichelewa, hivyo mgombea wa CCM kupita bila kupingwa. Kwanini wagombea wote wa upinzani wachelewe?

3. Wagombea wa CCM hawana makandokando

Wagombea wa upinzani wana makandokando yanayosababisha kukamatwa na polisi wakati wakirejesha fomu. Kwanini wasingekamatwa siku za nyuma?

Wapinzani jifunzeni kutokana na makosa
 
CCM huwa wanasambaza wanasheria wao kuhakikisha fomu zinajazwa vizuri. inawezekana hili linawasaidia sana.

Makandokando mengine ni wagombea wa upinzani kukosa uaminifu kwa vyama vyao hivyo kununuliwa hasa ukizingatia wengi wao husimama wenyewe kwa gharama zao wakati wa kampeni huku ukiwa huna uhakika wa kushinda.

kukwepa hasara, wanaona bora wafanye biashara
Mnunuzi ni nani?Je,ni hao wanaopita bila kupingwa?Hiyo tafsiri yake katika lugha ya Kiswahili huwa ni...
Kama hayo uliyobainisha hapo ni kweli,kwamba wananunuliwa,hao waliopita bila kupingwa bado wanastahili kuwa viongozi?
 
Leo ni siku iliyowekwa kisheria kuwa uteuzi unafanyika leo. Kulikuwa na hatari kubwa ya kuwahisha fomu maana wangeweza hata kuzichoma moto. Uzuri ni kuwa mtu akijiweka kwenye kundi la wahuni wewe ni kuhakikisha unammalizia huko huko kundini. Awamu hii kamwe hatutaruhusu uhuni!
Hivi,kuna uwezekano wa kukata rufaa/kuweka mapingamizi dhidi ya hawa wahuni wasiokuwa na uzalendo hata kidogo. Kungekuwa na hiyo fursa ya haki kutendeka katika hatua ya pingamizi,sidhani kama kungekuwa na unyama huu unaoendelea nchi nzima dhidi ya wapinzani na hasa CDM.
Watanzania tutimize wajibu wetu tukizingatia Utu,Usawa na Uzalendo ili kupata Haki zetu kwa Usawa.
 
Kisheria ama? Mmekata mapingamizi? Nauliza, hivi kuna sababu gani ya wagombea wa Cdm kusubiri hadi siku ya mwisho wakati inafahamika figisu ni lazima?
Mkuu acha kunishangaza, unajua tangazo rasmi LA tume juu ya tarehe ya kurudisha fomu ni lini?
 
Mkuu kurudisha fomu ilikuwa ni siku yoyote baada ya kuichukua, leo ilikuwa siku ya mwisho, na ndio siku ya uteuzi wa wagombea. Pitia tena sheria vizuri boss.
Husitufanye hatujui kusoma sheria. Leo ndio ilikuwa siku rasmi ya kurudisha form tarehe 25/08/2020 kuanzia saa mbili mpaka kumi jioni. Wewe umeisoma sheria ipo
 
Back
Top Bottom