Nini siri ya kunywa bia na kuzungumza kingereza?

NEW NOEL

JF-Expert Member
May 21, 2011
863
407
Hivi ni kwanini watu wakinywa Bia au pombe nyingine zenye asili ya kizungu uwa wanapenda kuzungumza kingereza,lakini wale wenzangu wakinywa za kienyeji kama ulanzi,mnazi,turbo...wao ni kuzugumza matusi tu?
 
soma chupa ya bia vizuri utaona kwenye ingredients pameandikwa water 50%,malt 20% na english 30%
 
Hivi ni kwanini watu wakinywa Bia au pombe nyingine zenye asili ya kizungu uwa wanapenda kuzungumza kingereza,lakini wale wenzangu wakinywa za kienyeji kama ulanzi,mnazi,turbo...wao ni kuzugumza matusi tu?

Ukilewa unamudu lugha iliyotumika kuandikia formula ya pombe husika! Ukinywa pombe ya kichina ukilewa utaongea kichina; ukinywa ya kihindi utanena kidosi; nk
 
kuna jamaa namfahamu pahala fulani...yeye akilewa(najua ni mataputapu) huongea kizungu sana tu na kisha hudai kuwa yeye hanywi hayo mataputapu bali hunywa bia na ndiyo sababu anaongea kizungu...

suprising...i dont know why!!!!!!
 
Njooni unikute nimekunywa vodka, utadhani nimetoka urusi siku hiyohiyo! There is something divine in alcohol, Wapi Kaizer athibitishe hili
 
nilimshuhudia mtu akilonga kingereza ila kwa fujo unajua kabisa kwa hali ya kawaida haiwezi kuiongea sijui lakin kwanin huwa ivo
 
nilimshuhudia mtu akilonga kingereza ila kwa fujo unajua kabisa kwa hali ya kawaida haiwezi kuiongea sijui lakin kwanin huwa ivo

Nimeitwa kwenye ITAVYUU ya kampuni ya kigeni na nina uhakika interview ni VINGEREZA; kwa hiyo unanishauri nijidunge VALUOR kulainisha lafudhi yangu ya kidhungu nikiwa katika usaili??? Just thinking loudly (sijanywa hapa)
 
Back
Top Bottom