Rack Fikiri
Member
- Oct 13, 2012
- 23
- 1
Kwa uchunguzi mdogo uliofanyika watoto wa maskini hufanya vizuri katika mitihani ya kidato cha nne na sita.Lakini asilimia kubwa hawaendelei na elimu ya chuo kikuu na hii imetokana na kuwa asilimia kubwa hunyimwa mkopo toka bodi ya mikopo ya elimu ya juu mfano mtoto mmoja wa maskini ameshindwa kwenda chuo kikuu kwa sababu mwaka jana alipata chuo MZUMBE UNIVERSITY lakini hakupata mkopo akaacha mwaka huu amepata SOKOINE UNIVERSITY tena hana mkopo ko mwaka huu chuo kwake ndoto huyu ni mfano tu lakini wapo wengi kibao Swala ambalo huwa sielewi ni je hii bodi ya mikopo ni ya wenye nacho au ya kusaidia maskini? Watoto wa matajiri wakubwa, viongozi,viongozi maarufu wastafu wabunge waliopigwa chini na walomo mjengoni wanapewa mikopo hafu maskini ananyimwa wanamanisha nini au ndo kauli ya mwenye nacho ataongezewa na huyu maskini atanyanganywa na hiki kidogo alichonacho? Hatujui 2naelekea wapi nchi hii watoto wa Maskini