zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,035
- 28,678
Mimi ningependa niwe neutral kwa faida ya mjadala mpana zaidi..... shida kubwa ni wabunge kuingia kwa tiketi za vyama hivyo mnachokubaliana kwenye kamati kuu ndicho wabunge mnaelekezwa kukisimamia bungeni?? Yaani mwenyekiti wa chama akielekeza kwamba swala hili ni ndio au sio wewe kma mbunge huwezi kwenda kubadilisha msimamo bungeni utaitwa msaliti rejea marehem filikunjombe alipotia saini kuhusu kutokuwa na imani na waziri mkuu!!!!
Hivyo tusiwalaumu sana wabunge ila tulaumu mfumo wa kuingia bungeni kwa udhamini wa chama cha siasa naona ndio mwiba mkali sana maana chama kikikutimua ndio unapoteza sifa ya kuwa mbunge...... warioba aliliona hili na kuweka mfumo mzuri ila naona mapendekezo yalipigwa teke
Uchama uchama unaua bunge